Skip to main content

Posts

Showing posts from January 3, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Kikwete ashiriki Mazishi ya Mwenyekiti wa Shivyawata

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameungana na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi ya Bw. Ernest Njama Kimaya aliyekuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) na Mjumbe wa Baraza la Taifa la Ushauri Kwa Watu Wenye Ulemavu Leo tarehe 02 Januari, 2025.  Mazishi hayo yamefanyika katika Kijiji cha Mnyuzi Wilaya ya Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.  Akizungumza wakati akitoa salamu za Serikali, Waziri Kikwete alimshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai wa Ndg. Kimaya ambaye alianza harakati za kutetea watu  wenye mahitaji maalum toka akiwa na miaka 19 miaka ya 1990.  Kimaya ambaye amewahi kushiriki katika harakati mbalimbali atakumbukwa kwa kazi nzuri aliyoifanya akiwa Mbunge wa Bunge maalum, mabadiliko ya sera zinazosimamia ustawi wa wenye mahitaji maalum, na mafanikio mbalimbali.  Kwa upande mwengine Mh. Rais wa JMT , Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi Milioni 3 kama ...

Mbunge Esther Matiko Atumia Milioni 85 Kuandaa Matiko Cup Tarime Mjini

 Na Helena Magabe Tarime. Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko ameweka historia na kuvunja rekodi ya kutumia zaidi ya milioni 85 kwenye kuzindua Matiko cup kitendo kilichowaacha midomo wazi mashibiki wa michezo walioshuhudia uzinduzi huo pamoja na Viongozi mbali mbali. Katika uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa mpira wa shamba la bibi Tarime mjini na kuzindunduliwa na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Tarime Meja Edward Gowele amempongeza Mhe Matiko kwa hatua hiyo kubwa ya Matiko Foundation kuzindua Matiko cup kwani michezo ni afya,ajira na starehe. Ametumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbali mbali kujitokeza kumwunga mkono Esther Matiko kupitia na kuiomba serikali kuwaunga mkono wale wote wanaonzisha michezo kwani kupitia michezo Vijana wanakuwa busy na michezo na kusaidia kupunguza uharifu,pia ni ajira na bududani kwa Watazamaji. Jackson Kagonye amempongeza Mhe Matiko kwa hatua hiyo na kusema kuwa kuanzisha michezo si jambo rahisi hata yeye aliwahi kufikiria kuanzisha lakini ...

Dereva wa Basi la Kisire apandishwa Kizimbani, asomewa Mashtala 22

Dereva wa basi la Kisire linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Sirari mkoani Mara, Adam Charles (30) amepandishwa kizimbani leo Januari 03.2025  kisha kusomewa shtaka lenye makosa 22 ikiwemo kusababisha majeruhi kwa abiria na uhalibifu wa mali. Katika kesi hiyo ya Trafiki namba 188/2025, Charles amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani humo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Erick Kimaro. Akimsomea shtaka hilo mbele ya hakimu Kimaro, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nuru Nko, ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa  anakabiliwa na kosa la uharibifu wa mali ambayo ni basi alilokuwa akiendesha namba T 229 DST kinyume na Kifungu namba 61 na 63 (2)(b) cha Sheria ya Usalama Barabarani Sura ya 168 marejeo ya mwaka 2002. Nko ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa akiendesha basi la Kampuni ya Kisire Desemba 19,2024, alisababisha ajali eneo la Kisamba wilayani Magu, mkoani humo na kusababisha majeruha kwa abiria 21. “Mshtakiwa (Charles) ambaye ni Mkazi wa National Jijini Mwanza ukiendesh...

Rais Mwinyi:Smz inaweza kulilipa deni kwa Miaka 2

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali  inatenga kiasi cha Dola za kimarekani Millioni 10 sawa na Shillingi Billioni 300 kwa mwaka  kwa ajili ya kulipa madeni  ya Nchi.  Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa  wakati Serikali inakopa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Ina Akaunti Maalum  inayoweka  Fedha za kutosha  Kulipa Madeni hayo ambayo sasa ina kiasi cha Shillingi Biliioni Mia Sita. Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Kituo cha Mabasi Kijangwani Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi kilichojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii  (ZSSF). Amefahamisha kuwa  deni  ililonalo Zanzibar kwa sasa ni Shillingi Trilion 1.2  linaloaminika na  kuwa  na  uwezo wa kukopesheka  tena  kutokana na utaratibu huo uliopo Serikali inaweza kulilipa kipindi cha miaka miwili.  Aidha ameeleza kuwa Wakati Serikali ya Awamu ya Nane inaingia Madarakani...