Skip to main content

Posts

Showing posts from July 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Ashiriki Mbio ya Gruma 2025

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Julai 05, 2025 ameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon (GRUMA 2025) zilizoanzia na kuishia kwenye eneo la Ibuguziwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Akizungumza katika tukio hilo, Mheshimiwa Majaliwa ameto wito kwa waratibu wa mbio hizo kuweka mikakati ya kuzifanya ziwe za kimataifa ili ziweze kukutanisha raia wa mataifa mbalimbali duniani. Lengo la Mbio hizo ni kuhamasisha uhifadhi wa mazingira  wa Mto Ruaha Mkuu ambao ni uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuifanya jamii kuona umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali za asili.

Wahamiaji haramu 800 wakamatwa mkoani Kagera

  Na Angela Sebastian  Bukoba Zaidi ya wahamiaji haramu 800 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kagera ndani ya mwezi Juni mwaka huu ambapo baadhi yao tayari wamerudishwa katika nchi zao na wengine wakifuata taratibu za na sheria za nchi zinavyoelekeza. Mkuu wa Waziri Mkuu wa Habari Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Petro Malima amessema wahamiaji hao wengi wao wanaotumia nchi jirani na huingia kwa njia isiyo rasmi. Amesema kwa kipindi cha mwezi Juni mwaka huu walikamatwa wahamiaji 725,ambao ni raia wa Burundi ni 514,Uganda 59,Rwanda 41,Kenya mmoja DRC sita,Ethiopia mmoja,China watano,Pakistan Watanzania mmoja, 53 na watu wengine ambao walikuwa wanatafuta urahia ni 44. "Unaweza kushangaa kwanini Watanzania, ni wale ambao wanapatikana na makosa kama vile wamekutwa na wahamiaji haramu au makosa ya kawaida ambayo yanaangukia kwenye makosa ya uhamiaji"ameeleza Malima. Amesema wahamiaji wapatao 637 waliondolewa kutokana kutokuwa na shaka nao pia kuhusu waeth...

Rais Ruto:Sitaomba Msamaha kwa Kujenga Kanisa Ikulu

  RAIS wa Kenya Dokta William Ruto amekubali kuwa anajenga Kanisa katika Ikulu ya Harambee Jijini Nairobi akidai kuwa anatumia pesa zake kulijenga. Kiongozi huyo Mkuu wa nchi alisema kuwa yeye anaamini Mungu na kwamba hataomba masamaha kwa kujenga Kanisa la Mungu. Tutajenga kanisa la Mungu, shetani akasirike afanye kile anachotaka,”Rais Ruto alisema. “Ni kweli mimi najenga Kanisa hapa Ikulu kwani nilipata kanisa la mabati.Kanisa la mabati inatoshana na Ikulu? Kwa upande mwingine Dkt Ruto anasema kuwa anatumia pesa zake kujenga hilo kanisa. “Haitagharimu serikali ya Kenya hata shilingi moja kwani najenga na pesa zangu,” akaongeza Dkt Ruto. Haya yanajiri siku moja tu baada ya habari kuhusu ujenzi wa kanisa hilo lenye uwezo wa kusitiri watu 8,000 kufichuliwa kwenye Baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini Kenya”. Kulingana na ufichuzi huo, kanisa hilo, lililopambwa kama ‘Cathedral’, linaundwa na Skair Architects Limited na lina madirisha marefu na picha za setilaiti zinaonyesha ujenzi unaoe...

Ruto: Sitaomba Msamaha kwa kujenga kanisa Ikulu

RAIS wa Kenya Dokta William Ruto amekubali kuwa anajenga Kanisa katika Ikulu ya Harambee Jijini Nairobi akidai kuwa anatumia pesa zake kulijenga. Kiongozi huyo Mkuu wa nchi alisema kuwa yeye anaamini Mungu na kwamba hataomba masamaha kwa kujenga Kanisa la Mungu. Tutajenga kanisa la Mungu, shetani akasirike afanye kile anachotaka,”Rais Ruto alisema. “Ni kweli mimi najenga Kanisa hapa Ikulu kwani nilipata kanisa la mabati.Kanisa la mabati inatoshana na Ikulu? Kwa upande mwingine Dkt Ruto anasema kuwa anatumia pesa zake kujenga hilo kanisa. “Haitagharimu serikali ya Kenya hata shilingi moja kwani najenga na pesa zangu,” akaongeza Dkt Ruto. Haya yanajiri siku moja tu baada ya habari kuhusu ujenzi wa kanisa hilo lenye uwezo wa kusitiri watu 8,000 kufichuliwa kwenye Baadhi ya Vyombo vya Habari Nchini Kenya”. Kulingana na ufichuzi huo, kanisa hilo, lililopambwa kama ‘Cathedral’, linaundwa na Skair Architects Limited na lina madirisha marefu na picha za setilaiti zinaonyesha ujenzi unaoendelea...

TEA kuanza na awamu nyingine mafunzo ya kuendeleza ujuzi

Utekelezaji wa SDF kunufaisha vijana 160,000 Na Mwandishi Wetu.  MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA), imesema mwaka huu wa fedha itaanza utekelezaji wa awamu nyingine ya Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) ambapo unatarajiwa kutumia Dola za Marekani milioni 30 ndani ya miaka mitano. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam  Salaam na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa mfuko huo, Eliafile Solla wakati akizungumza na gazeti hili kwenye maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.  Alisema kwenye mafunzo hayo yatakayoshirikisha vijana wenye umri wa kati pekee jumla ya watu 160, 000 wanatarajiwa kunufaika na mafunzo hayo.  Alisema awali kwenye utekelezaji wa mafunzo kupitia SDF ulioanza mwaka 2017 na kumalizika mwaka 2024 lengo lilikuwa kuwafikia watu 35,000 lakini wakati wa utekelezaji mahitaji yalikuwa makubwa na mpaka unakamilika mwaka jana wanufaika walikuwa 49,000. Alisema baada ya mafunzo kukamilika mamlaka ya elimu ilifanya tathmini (tracer st...

Jwtz Latoa Msaada Kwa Munusura wa Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa msaada wa maboksi mia moja ya vigae na matenki matano yenye ujazo wa lita elfu kumi kila moja kama mchango wake katika ujenzi wa nyumba nane zilizopo Wilaya ya Karongi nchini Rwanda, kwaajili ya manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,Mkurugenzi wa Tiba wa JWTZ Brigedia Charles Emilio Mwanziva amesema kuwa pamoja na kukabidhi vifaa hivyo,pia JWTZ limetoa wataalam wa Tiba ambao wameungana na wengine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushiriki kutoa huduma kwenye hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini humo ikiwa ni sehemu ya mpango wa Majeshi ya Jumuiya kuimarisha uhusiano wao na wananchi kwenye nchi wanachama. Naye Meya wa Mji wa Karongi Mheshimiwa Kazungu amelishukuru JWTZ kwa msaada lililoutoa huku akiainisha kuwa mpango wa kuwapatia makazi bora manusura hao unafanyika nchi nzima kwa kuz...

Jwtz Latoa Msaada Kwa Munusura wa Mauaji ya Kimbari Nchini Rwanda

 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa msaada wa maboksi mia moja ya vigae na matenki matano yenye ujazo wa lita elfu kumi kila moja kama mchango wake katika ujenzi wa nyumba nane zilizopo Wilaya ya Karongi nchini Rwanda, kwaajili ya manusura wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda,Mkurugenzi wa Tiba wa JWTZ Brigedia Charles Emilio Mwanziva amesema kuwa pamoja na kukabidhi vifaa hivyo,pia JWTZ limetoa wataalam wa Tiba ambao wameungana na wengine kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kushiriki kutoa huduma kwenye hospitali na vituo vya afya mbalimbali nchini humo ikiwa ni sehemu ya mpango wa Majeshi ya Jumuiya kuimarisha uhusiano wao na wananchi kwenye nchi wanachama. Naye Meya wa Mji wa Karongi Mheshimiwa Kazungu amelishukuru JWTZ kwa msaada lililoutoa huku akiainisha kuwa mpango wa kuwapatia makazi bora manusura hao unafanyika nchi nzima kwa...

Huduma za Fidia Kwa Wafanyakazi si Suala la Hiari-Majaliwa

_▪️Asema Serikali itaendelea kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa haki na ustawi wa wafanyakazi._ _▪️Atoa wito kwa waajiri kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi._ _▪️Aitaka WCF iendelee kushirikiana na wadau katika sekta ya ajira._   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa huduma za fidia kwa wafanyakazi si suala la hiari bali ni haki ya msingi ya mfanyakazi, inayopaswa kulindwa, kuendelezwa na kusimamiwa kwa weledi na uwajibikaji wa hali ya juu. Amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda sambamba na ulinzi wa haki na ustawi wa wafanyakazi wake. Amesema hayo leo (Ijumaa, Julai 05, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. “Waajiri, wafanyakazi na Serikali tunapaswa kuendelea kushirik...