Skip to main content

Posts

Showing posts from July 9, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Saidi Yakubu Akutana na Uongozi wa Chama Cha AMICAL

Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu amekutana na uongozi wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na Comoro - AMICAL waliofika kujitambulisha kwake.  Ujumbe huo uliowajumuisha Katibu Mkuu Youssouf Said Ali ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Elimu wa Rais wa Comoro, Msemaji wa AMICAL Bwana Abdoulkader Mahmoud ambaye ni Inspekta Jenerali wa zamani wa Jeshi la Polisi Comoro na Balozi Mstaafu Mohamed Ahmed Thabit ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Ulinzi wa Waziri wa Mambo ya Nje  Comoro.  Uongozi wa AMICAL umepongeza jitihada za kuimarisha uhusiano zilizopo na wameeleza utayari wao katika kusaidia kukwamua changamoto zozote zinazojitokeza hususan katika biashara na masuala ya kijamii. Balozi Yakubu aliwaeleza namna Tanzania inavyothamini uhusiano wake na Comoro na kuahidi kukutana nao mara kwa mara na pia kuwakutanisha na viongozi wa Tanzania wanapotembelea Comoro. Aidha alitumia fursa hiyo kuwakaribisha katika Kongamano la Diaspora linalotarajiwa kufanyika mwisho...

Rais wa Femata Aipongeza Wizara ya Madini Kwa Usimamizi Mzuri

Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini  (FEMATA), John Bina ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa kazi nzuri ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini. Bina ameyasema hayo leo Julai 09, 2024 alipotembelea Banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam ' Sabasaba ' yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.  "Kazi yenu ni  nzuri sana, mnafanya kazi kubwa ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini, niwapongeze Taasisi zote zilizopo chini ya Wizara kuanzia Tume ya Madini,  Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).

TFS Yatakiwa Kuongeza Uzalishaji wa Mbegu za Miti

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)  imetakiwa kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu za miche ya miti ili zifikie  wananchi wengi zaidi na hatimaye kushiriki katika kuokoa misitu iliyotoweka. Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) wakati wa ziara ya kikazi katika Kituo cha Uzalishaji mbegu za Miti leo Julai 9,2024  Mkoani Morogoro. "Tuendelee kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mbegu na vyanzo vya mbegu na pia tuongeze Bajeti kukiwezesha kituo hiki" Mhe. Kairuki amesema. Katika hatua nyingine Waziri Kairuki amewataka kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na wahariri ili jamii ifahamu umuhimu wa mbegu bora za miti. "Ni lazima muwe na maabara ya kisasa na pia mkitangaze kituo hiki kijulikane tuna mbegu za miche aina gani na tuna maabara" ameongeza. Aidha, Mhe Kairuki ametilia mkazo suala la ukusanyaji maduhuli kujifanyia tahmini katika makusanyo na wanachotoa kwa Serikali. Amewataka kutafuta  ushirikiano katika Taasi...

Mbunge Ghati Chomete Awakilisha Madiwani Mkoa wa Mara Kahama

Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete amehudhuria na kuwakilisha Madiwani Mkoani Mkoa Mara kukabidhi zawadi Kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa katika Semina ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. Katika Semina  ambayo imefanyika katika ukumbi wa Sub-Marine iliyoko Manispaa ya Kahama, Mhe Ghati aliongoza zoezi la kukabidhi zawadi mbalimbali za upendo zilizotolewa na Waheshimiwa Madiwani wa Kata Wanawake pamoja na Madiwani wa Viti Maalum Mkoa wa Mara kwa ajili ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi.Mary Pius Chatanda. Zawadi hizo zilizotolewa kwa lengo la kutambua juhudi, ushupavu na umahiri katika usimamizi madhubuti wa Jumuiya ya UWT Taifa.

Jaji Mtungi Avitaka Vyama vya Siasa Kufuata Sheria za Usajili na Katiba Za Vyama

  Msajili wa vyama Vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vyote vya siasa kufuata sheria za usajili na katiba zao za vyama pindi wanapotekeleza majukumu yao Ikiwa ni pamoja na chaguzi za  ndani ya vyama ili kuepukana na Migogoro inayoweza kuwasababishia makundi na kujengeana chuki zisizokuwa na tija. Ametoa Wito huo leo Julai 9,2024 jijini Dar es Salaam  wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo juu ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa vyama hivyo, namna ya kuhimili migogoro inayotokea wenyewe kwa wenyewe pasipo kufikishana katika vyombo vya sheria . Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa ni taasisi hivyo vinapaswa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria ya nchi ili na wanapotenda Majukumu yao yawe yanatambulika . “Haya Mafunzo ni mahusihusi na yamekuja kwa wakati muafaka yatasaidia kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo Mogogoro inayosababishwa ubadhilifu wa fedha za chama, matumizi mabaya ya ...

Majaliwa Awapongeza Rais Samia na Dkt Mwinyi Kwa Sera Bora Sekta ya Fedha

Asema zimekuwa msingi katika ukuaji wa sekta ya fedha_ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewapongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa sera nzuri za fedha na Uchumi ambazo zimekuwa  msingi wa ukuaji wa sekta ya fedha hususan katika kuleta suluhisho la huduma za kifedha kwa Wananchi. Amesema kuwa kupitia Sera hizo kumekuwa na  mabadiliko makubwa  mpaka kwenye ngazi za vitongoji na kusaidia sana kusogeza huduma kwa wananchi kupitia taasisi za fedha. Amesema hayo leo (Jumanne, Julai 09, 2024) wakati alipozindua tawi la benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) mkoani Morogoro. Amesema kuwa uzinduzi wa benki hiyo ni mpango wa kuendeleza dhamira ya Dkt. Samia wa kuleta maendeleo ya haraka kwa Watanzania kupitia uwezeshaji wa wananchi kiuchumi. “Ni azma ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha kwamba huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu kwa kila mwananchi” Ameongeza kuwa ufunguzi tawi hilo katika mkoa wa Morogoro utakuwa ni miongoni ...

Makamu wa Rais Akagua Ukarabati na Upanuzi wa Kiwanja Cha Ndege Kigoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amekagua na kupokea taarifa ya maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma unaoendelea kutekelezwa Mkoani Kigoma. Dkt. Mpango amekagua uwanja huo, leo Julai 09, 2024 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo kazi ya ukarabati na upanuzi inahusisha Ujenzi wa jengo la Abiria, maegesho ya ndege, njia za ndege, mnara wa kuongozea ndege, taa za kuongozea ndege wakati wa usiku na barabara za kuingia na kutoka uwanja wa ndege. Dkt. Mpango ameridhishwa na kazi inayoendelea ya uboreshwaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma ambapo amesisitiza umuhimu wa uboreshaji wa Kiwanja hicho kwa maendeleo ya Mkoa wa Kigoma na Taifa kwa ujumla. “Kigoma tunataka tufanane na wengine, tuwe na Kiwanja kizuri hata wageni wakifika Kigoma sio kale kajengo kalikoandikwa Kigoma Airport, Naamini hapa kitatoka kitu kizuri kwa hii dalili ninayoiona”, amesema Dkt. Mpango. Aidha, Dkt. Mpango amewataka wananchi waliopata fursa...

Jinsi Grumeti Fund Inavyowawezesha Wananchi Ujuzi na Rasilimali Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Serengeti na Bunda.

  Na Emmanuel Chibasa Athari za mabadiliko ya tabia nchini zimeendelea kuathiri shughuli nyingi za kiuchumi hususani kilimo na ufugaji hapa nchini na duniani kwa ujumla na athari hizi pia zimekua zikiwakumba wakazi wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambao pia ni jamii ya wakulima na wafugaji. Miongoni mwa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi inayowakumba wananchi katika eneo hilo ni kupungua kwa malisho ya wanyama kutokana na kubadirika kwa misimu ya joto na mvua na hivyo jamii hiyo kuathirika pakubwa kutokana na kutegemea shughuli za kilimo na ufugaji kujikimu kimaisha. Changamoto hizi kwa sasa zimeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya shirika lisilo la kiserikali la Grumeti Fund linalofanya kazi za kuhifadhi Pori tengefu la Grumeti lililopo magharibi mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuanzisha mradi mpya unaojulikana kama “Climate-resilience and Livelihood Improvement Program” (CLIP) kama mkakati wa kuiwezesha jamii hiyo kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. ...