Skip to main content

Posts

Showing posts from August 26, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

ANATAFUTWA

 

Rais Dkt. Samia Awasili Nairobi Kenya Kuhudhuria Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi tayari kwa kuhudhuria hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mhe. Raila Amolo Odinga, Waziri mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Dkt. William Samoei Ruto. Hafla hiyo itafanyika katika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi mbalimbali, tarehe 27 Agosti, 2024.

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA KIST

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 27, 2024 anamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  Maadhimisho ya  miaka 50 ya  Idara ya Ujenzi ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST). Hafla hiyo unafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “_Uimarishaji wa Taaluma ya Uhandisi Ujenzi kwa Maendeleo Endelevu ya Nchi_”

HISTORIA YA SIMBA TUNDU LISSU YATAJWA

 Fahamu historia ya Simba Tundu Lissu na jinsi ya kumuona baada ya Kizimkazi Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), mnyama anayezidi kuwa maarufu nchini Tanzania kwa sasa ni ‘Simba Tundu Lissu’ ambaye alizaliwa Dar es Salaam Zoo, nje kidogo ya jijini la Dar es Salaam eneo la Mwasonga, Kigamboni. Jina la Simba Tundu Lissu lilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassan Agosti 24, 2024 wakati akitembelea mabanda ya maonesho yaliyopo Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ambapo Rais Samia alieleza kuwa nia kumpa jina Simba huyo ni kutokana na umachachari wa mwanasiasa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Simba Tundu Lissu alizaliwa Januari Mosi, 2018, hivyo kwa sasa ana miaka 7. Simba huyu ana asili ya Hifadhi mchanganyiko za Mapori ya Akiba ya Grumeti na Ikorongo yanayopatikana katika Mfumo Ikolojia ya Serengeti, Kaskazini mwa Tanzania ambako ndiko wazazi wake walikotokea kabla hawajahamishiwa Dar es Salaam Zoo. Hivyo Sim...

Waziri Mkuu Amuwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 ya KIST

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Agosti 27, 2024 anamuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika  Maadhimisho ya  miaka 50 ya  Idara ya Ujenzi ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST). Hafla hiyo unafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar. Kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni “Uimarishaji wa Taaluma ya Uhandisi Ujenzi kwa Maendeleo Endelevu ya Nchi”

MGANGA WA KIENYEJI MIKONONI MWA JESHI LA POLISI KWA MAUAJI YA KINYAMA

Jeshi la Polisi linawashikilia watu saba akiwemo mganga wa kienyeji, Nkamba Kasubi kwa kosa la mauaji ya watu watatu ambao wanadaiwa kuuawa na kufukiwa nyumbani kwa mganga huyo mkoani Singida. Kati ya miili hiyo, miwili imetambuliwa ambapo mmoja ni wa Gedion Samwel Mnyawi (53), aliyeuawa baada ya kuwauzia shamba mara mbili Hawa Hussein Sumwa (54) na Idd Hussein Idd (25) wote wakiwa wakazi wa Makuro. Akitoa taarifa hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema baada ya watu hao kuuziwa shamba hilo mara mbili na baadaye kugundua kuwa shamba hilo tayari liliuzwa kwa mtu mwingine, walikwenda kwa mganga huyo ambaye aliwaambia kuwa ili pesa zao zirudi inabidi mwanaume huyo atolewe kafara.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA RAIS XI JINGPING WAPONGEZWA CHINA

 

RAIS MWINYI AMESEMA CHINA IMEKUWA NA MSAADA MKUBWA KWA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema China imekuwa ikiisaidia Zanzibar katika mambo mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya hospitali.  Rais Dk. Mwinyi Amesifu ukarabati mkubwa wa Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, utoaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa sekta ya afya, msaada wa vifaa vya matibabu na dawa, pamoja na udhamini wa masomo kwa madaktari wazalendo. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 26 Agosti 2024, Ikulu Zanzibar, alipozungumza na timu ya madaktari 29 kutoka kundi la 33, walioongozwa na Kaimu Balozi Mdogo wa China Zanzibar, Chang Ming, chini ya kiongozi wa madaktari hao, Dk. Yuzheng Huang, waliofika kumuaga baada ya kufanya kazi nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja. Aidha, Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya China kwa ushirikiano wake na Zanzibar kupitia sekta mbalimbali za maendeleo, ikiwemo sekta ya afya, unaochangiwa na uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina Zanzibar na China tangu kuasisiwa ...

PROFESA RIZIKI SHEMDOE ATAKA UVUVI HARAMU KUKOMESHWA ZIWA VICTORIA

Rai imetolewa kwa Mataifa ya Kenya, Uganda na Tanzania, kufanya doria ya pamoja katika ziwa victoria, ili kukomesha uvuvi haramu na biashara ya mazao ya uvuvi, inayokiuka taratibu za kisheria ndani ya ziwa hilo. Akifungua mkutano leo Agosti 26,2024 wa kuhamasisha wadau wa uvuvi kudhibiti uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi ziwa victoria kwenye ukumbi wa mikutano Nyakahoja,Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe amesema ziwa linamchango wa asilimia 67% katika sekta ya uvuvi nchini, likiwa limeshuka kwa asilimia 17% kutoka 85%, likiwa na wavuvi 100,002, huku wanufaika wa moja kwa moja wa biashara ya mazao ya uvuvi wakiwa zaidi ya laki mbili. "Serikali kwa kutambua mchango wa sekta hii inaendelea kuiboresha ikiwa pamoja na kutoa boti za kisasa na ukopeshaji wa bila riba kwa makundi maalum wa Ufugaji wa samaki wa vizimba,lakini Pamoja na mchango huo, kikwazo kikubwa kinacholikabili ziwa hili ni uvuvi haramu unaoangamiza mazalia ya rasilimali zilizopo z...