Skip to main content

Posts

Showing posts from January 25, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Kassim Majaliwa awasili Mpanda

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 26, 2025 amewasili Mpanda mkoani Katavi ambapo atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM jimbo la Katavi unaofanyika katika viwanja vya TARURA. Kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda amepokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Iddi Kimanta,Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwamvua Mrindoko na Mbunge wa jimbo la Katavi Mhandisi Isaack Kamwele.

Serikali yaagiza Mamlaka za Mafunzo Jeshi la Uhifadhi Mlele Kutatua Changamoto

Na Hamis Dambaya, Mlele Katavi. Serikali imeziagiza mamlaka na taasisi zinazosimamia na kutumia kituo cha mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi kilichopo Mlele mkoani Katavi kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho. Maelekezo hayo yametolewa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii mheshimiwa Dunstan Kitandula (Mb) wakati akifunga mafunzo ya watumishi wa taasisi za uhifadhi zinazotoa mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi wa wanyamapori na misitu yaliyofanyika kwa miezi mitatu kwa lengo la kuwabadilisha watumishi waliojiunga na taasisi hizo hivi karibuni kutoka katika mfumo wa kiraia kwenda mfumo wa kijeshi.  Mhe. Kitandula amesisitiza kuwa ni muhimu taasisi hizo kuboresha miundombinu inayoklabili kituo hicho ikiwemo huduma za afya, barabara,maeneo ya kujifunzia,vifaa pamoja na kuhakikisha kituo hicho kinatumia nishati safi ya kupikia. Katika risala yao wahitimu walimweleza mhe naibu waziri uwepo wa changamoto hizo ambapo walisema kwamba ikiwa maboresho hayo yatafanyika yata...

Wizara ya maji yaridhishwa na mradi wa maji Same - Mwanga - Korogwe

  *Uongozi wa Wizara ya Maji umeridhishwa na kazi ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe.* Ukaguzi wa mradi huo umefanyika na timu ya Menejimenti ya Wizara ya Maji ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri. Mhandisi Mwajuma amesema serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe wanaondokana na adha ya huduma ya maji. Amesisitiza kuwa Wizara ya Maji itahakikisha inaendelea kuwekeza katika matumizi ya teknolojia ikiwemo matumizi ya Dira za malipo kabla ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe . Dkt. Samia Suluhu Hassan.hivyo wananchi wa Same Mwanga wategemee matokea makubwa na mazuri.

Mbunge Mavunde awawezesha kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Jijini Dodoma

  ▪️Awapatia miradi ya Kiuchumi na kutunisha mfuko wa Kikundi. ▪️Wafanyabiashara wamshukuru kwa kuwajali na kuwaendeleza kiuchumi ▪️Wampongeza Rais Samia kuboresha miundombinu ya masoko Jijini Dodoma 📍Dodoma Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kuwaendeleza kiuchumi wafanyabiashara wa soko la Sabasaba Jijini Dodoma kwa kuwapatia miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kuongeza kipato chao. Mh. Mavunde kayasema hayo leo wakati wa Mkutano wa Kikundi cha Twiga cha wafanyabiashara wadogo wadogo uliofanyika ndani ya Soko la Sabasaba. “Tunaishukuru serikali chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S . Hassan kwa maboresho makubwa ya miundombinu yanayoendelea ndani ya Jiji la Dodoma. Nipo hapa leo kama Mwanachama mwenzenu wa kikundi cha Twiga ambacho tulikiasisi pamoja. Nina furaha kubwa kusikia mipango iliyopo ya kuongeza miradi ya kujiimarisha kiuchumi,nitajitahidi kuendelea kuwashika mkono ili muweze kusima