Skip to main content

Posts

Showing posts from April 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

TRC Yatolea Ufafanuzi Video ya 'Mlio usio wa Kawaida' Kwenye Treni ya SGR

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa rasmi kwa umma likikanusha picha mjongeo (video) inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuonyesha kichwa cha treni ya SGR kikiwa kinatoa mlio usio wa kawaida. TRC imethibitisha kuwa taarifa hizo ni za uzushi na zinalenga kupotosha umma, kwani baada ya ufuatiliaji wa kina, imebainika kuwa hakuna tukio kama hilo lililotokea katika mifumo yao ya uendeshaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Aprili 2026 na Kitengo cha Uhusiano, Shirika la Reli Tanzania (TRC) Shirika hilo limehakikishia umma kuwa treni zote za mwendokasi (SGR) zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na ziko katika hali salama kabisa.  Aidha, hakuna hitilafu yoyote ya kiufundi iliyoripotiwa na wataalamu wanaoendesha na kusimamia mitambo hiyo kama inavyodaiwa kwenye video hiyo ya uzushi. "TRC inasisitiza kuwa usalama wa abiria na mali zao ni kipaumbele cha juu. Mifumo yote ya uendeshaji hukaguliwa mara kwa mara na wataalamu wetu ili kuhakikisha huduma zinatolewa kw...

Tanzania Kuendelea Kujitangaza Kimataifa Kwa Kunadi Fursa za Kiuchumi-Makonda

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Paul Makonda amesema Tanzania itaendelea kuingia kwenye macho na masikio ya Dunia, kwa kuendelea kuonesha fursa zote zilizopo katika sekta ya Utalii , Madini na kilimo pamoja na uwepo wa vipaji mbalimbali. Hayo amebainisha mapema hii leo, Aprili 20, 2026 katika hafla fupi ya utilianaji saini wa makubaliano ya kuandaa mashindano ya Miss World 2027 ambapo waziri Makonda amesema kuwa zaidi ya wageni elfu ishiriki kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki jijini Dar es Salaam. Aidha, Makonda amewataka waandaaji wa mashindano mbalimbali ya walimbwende kutimiza ahadi wanazoziahidi kwa washiriki jambo ambalo linaweza kupunguza migogoro katika jamii kuhusu madai ya zawadi au vitu vilivyoahidiwa kwa washindi katika mashindano husika. Sambamba na hilo Waziri Makonda amesema kuwa Tanzania inaenda kuandika historia ya kuwa ni nchi ya kwanza kuandaa mashindano hayo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati huki ikiwa nchi ya pili kuandaa bar...

Serikali Kuboresha Mazingira ya Uchimbaji na Biashara ya Madini ya Metali Nchini

▪️  Waziri Mavunde asikiliza na kutatua changamoto za wadau wa madini ya metali ▪️ Aagiza kuanzishwa kwa Jukwaa la kudumu kati ya Serikali na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ▪️ Maabara ya kisasa ya madini inayojengwa Dodoma kutatua changamoto ya uchunguzi wa sampuli za madini ▪️Mfumo wa malipo ya mrabaha kuangaliwa upya ▪️ Wadau waahidi kushirikiana na Serikali kuongeza tija na mapato ya Taifa 📍Dodoma Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amewataka wadau wa madini ya metali (base metals) kujipanga kimkakati na kuifanya sekta hiyo kuwa kichocheo kipya cha ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini, akisisitiza kuwa usimamizi madhubuti wa rasilimali, uwekezaji katika teknolojia za kisasa, uongezaji thamani, pamoja na kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uwazi ni nguzo kuu za kuongeza tija, thamani na ushindani wa madini hayo katika soko la madini hayo.  Amesema kuwa kupitia mbinu hizo, sekta ndogo ya madini ya metali ina uwezo mkubwa wa kufungua fursa za ajira, kuongeza mapato...

Waziri Mkuu Atimiza Ahadi ya Kumpatia Kitimwendo Helena Joseph

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Aprili 20, 2026) amemkabidhi kitimwendo Helena Joseph Mwandu (mwenye mahitaji maalum), Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.   Waziri Mkuu aliahidi kumpatia Helena kiti hicho katika mazungumzo waliyoyafanya baada ya mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Msanga wilayani Chamwino Dodoma, jana (Aprili 19, 2026). Akizungumza baada ya kupatiwa kiti hicho, Helena amemshukuru Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu kwa kumpatia kitimwendo hicho kwani kitamsaidia katika shughuli zake.

Dkt. Mwigulu Awakutanisha Viongozi wa Serikali na Wakazi wa Mahomanyika na Ipala

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumatatu, Aprili 20, 2026) ameendesha kikao cha kutafuta suluhu ya mgogoro wa Mahomanyika wilayani Dodoma mkoani Dodoma uliodumu kwa karibu miaka 10. Kikao hicho kilichofanyika Ofisini kwake, Mlimwa jijini Dodoma, kimehudhuriwa na Waziri wa Ardhi, Dkt. Leonard Akwilapo, Naibu Waziri (OWM – TAMISEMI) Dkt. Jafar Seif, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Khatibu Kazungu na  uongozi wa Wilaya ya Dodoma na baadhi ya viongozi na wakazi wa Kata za Nzuguni na Ipala. Kikao hicho ni matokeo ya ziara ya kikazi ambayo Waziri Mkuu aliifanya jana, (Jumapili Aprili 19, 2026) wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambapo akiwa katika mkutano wa hadhara katika kata ya Msanga, baadhi ya viongozi na wakazi wa Mahomanyika walieleza kutoridhishwa na utaratibu unaotumika kupima maeneo yao jambo lilowafanya kuwa na mgogoro na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Wanaitende Mtaoga Maji Mpaka Mtachubuka-Mwalunenge

MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, amezindua rasmi mradi wa uchimbaji wa visima vya maji katika Kata ya Itende, Wilaya ya Mbeya, mkoani Mbeya, ikiwa ni hatua ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa eneo hilo ambapo amesema wataoga maji mpaka wachubuke. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwalunenge amesisitiza dhamira yake ya kuleta mabadiliko ndani ya kipindi chake cha uongozi, akibainisha kuwa hatarajii kuacha ahadi yoyote bila utekelezaji. “Nataka miaka yangu mitano Itende ibadilike. Mkataba mlionipa ni wa miaka mitano, na mambo yote niliyoahidi lazima niyatekeleze ndani ya kipindi hicho,” amesema Mwalunenge. Ameeleza kuwa kila kisima kitagharimu takribani shilingi milioni 12 hadi kukamilika kwake ambapo amewataka wananchi kushiriki katika utunzaji wa miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwahudumia ipasavyo. “Tukitunze hiki kisima ili hata tukipata fedha nyingine tuweze kuongeza visima vingine zaidi,” ameongeza. ...