Skip to main content

Posts

Showing posts from March 10, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mama Tabu Peter Afikisha Mwanae Mwenye Ulemavu Kwa Waziri Mkuu

 Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Bi. Tabu Peter, Mama mzazi wa mtoto John Peter ambaye anaulemavu wa miguu wakati alipohitimisha Mkutano wake wa hadhara uliofanyika Sumbawanga mkoani Rukwa leo Machi 10, 2026.

Mbunge Nassirya Ally Awataka Wazazi na Walezi Kutunza Watoto Bila Ubaguzi

Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Nassirya Nassir Ally amewataka wazazi na walezi kuwatunza watoto wote bila ubaguzi, hususan watoto wenye ulemavu, huku akisisitiza kuwa kuwaficha watoto hao kunawanyima haki zao za msingi na fursa za kuonesha vipaji na uwezo walionao katika jamii. “Nitoe wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu, Watoto hawa wana uwezo mkubwa kama watoto wengine na wakipewa malezi bora, elimu na mazingira rafiki wanaweza kufanya mambo makubwa na kuisaidia jamii na Taifa letu.” Kongamano hilo limewakutanisha wanawake kutoka makundi mbalimbali, viongozi wa Serikali, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi kwa lengo la kujadili masuala ya haki za wanawake, usawa wa kijinsia, ujasiriamali na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Makamu wa Rais Akutanisha Wizara Kukabiliana na Uhifadhi wa Mazingira Nchini

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Wizara zinahusiana na Sekta ya Mazingira, kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwa na mpango wa pamoja utakaowezesha uhifadhi endelevu wa mazingira. Makamu wa Rais ametoa wito huo, wakati akifanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Festo Dugange, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi pamoja na wataalamu kutoka Wizara hizo, katika kikao kilichofanyika mkoani Dodoma.   Amesema Wizara hizo zinategemea zaidi uhifadhi wa Mazingira, mathalani Wizara ya Maji itafanya kazi kwa ufanisi kama vyanzo vya maji havitaaribiwa, vilevile mpango wa matumizi ya nishati safi ya kupikia utawezesha kuokoa ukataji miti ovyo na hivyo kuli...

Mheshimiwa Ghati Chimete ashiriki mazishi ya marehemu Sunzy Mwita Chambiri wilayani Butiama, Mkoani Mara

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe.Ghati Zephania Chomete Leo tarehe 10 Machi, 2026 ameungana na mamia ya waombolezaji waliojitokeza kushiriki Mazishi ya Marehemu Sunzy Mwita Chambiri aliyekuwa Mtumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TMDA) Makao Makuu Dodoma. Mazishi hayo yamefanyika katika Kijiji cha Wegero, Kata ya Buswahili, Wilayani Butiama, Mkoani Mara na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama, Serikali, Watumishi wa TMDA, Ndugu, Jamaa na Marafiki. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. AMINA  Mhe.Ghati Chomete (Mb),  Viti Maalum Mkoa- Mara,  Butiama (Wegero) -Mara,  Machi 10, 2026.

Dkt. Mwigulu Aagiza Takukuru Kuchunguza Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo

_Asema Serikali haitavumilia uzembe katika utekelezaji wa miradi ya Dkt. Mwigulu Aagiza Takukuru Kuchunguza Ujenzi Wa Hospitali Ya Wilaya Ya Kalambo* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina kuhusu makadirio na matumizi ya fedha za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa. Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Machi 10, 2026) wakati akizungumza na wananchi wa Kasanga, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo, ambapo baadhi ya majengo bado hayajakamilika licha ya fedha kutolewa na Serikali. Serikali ilitoa zaidi ya Sh. bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo ambapo katika awamu ya kwanza majengo saba ya huduma za afya yalijengwa, ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mama na mtoto, maabara, duka la dawa pamoja na miundombinu mingine ya huduma za hospitali. Hata hivyo, licha ya fedha hizo kutolewa na baadhi ya ma...

Nchi Wanachama Umoja wa Mataifa Wakutana Kujadili Hali ya Wanawake Duniani.

📌 MKUTANO WA HALI YA WANAWAKE DUNIANI (CSW 70) WAFUNGULIWA RASMI JIJINI NEW YORK. 📌 WAZIRI GWAJIMA KUTOA TAARIFA YA TANZANIA  Na WMJJWM- New York Marekani  Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekutana Jijini New York nchini Marekani kwa lengo la kujadili hali ya Wanawake katika nchi hizo.  Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres Machi 09, 2026 na utamalizika Machi 19, 2026. Mkutano huo ni wa 70 kuhusu Hali ya Wanawake Duniani unaoongozwa na Kaulimbiu isemayo "Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo", (Ensuring and Strengthening access to justice for all Women and Girls, including by promoting inclusive and equitable legal system, eliminating discriminatory laws, policies, and practices and addressing structural barriers”). Mkutano utajadi...