Skip to main content

Posts

Showing posts from September 13, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kikundi Cha Vijana Wa Kilimo Cha Parachichi Chaonyesha Mfano Ngara

 Na Angela Sebastian; Ngara Kikundi cha vijana wapatao nane wa Kata ya Kabanga Wilayani Ngara mkoani Kagera ambao wamejiunga pamoja na kuanzisha kilimo cha matunda aina ya Parachichi wamekuwa kichocheo cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi ambapo huwaingizia kipato. Utekelezaji wa Sera ya vijana ya mwaka 2017 hadi 2034 imeisukuma Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kutenga shilingi milioni 52.6 na kati ya hizo ml.40 ikiwa ni asilimia 10 itokanayo na mapato ya ndani huku vijana wenyewe kutokana na Sera hiyo wakichangishana fedha taslimu kupitia kikundi chao na kupata shl.mil 200. Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Kabanga matunda group,Livingstone Shedrack ametoa taarifa kwa Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ismail Ali Ussi na kusema kuwa lengo la vijana hao kwa kushirikiana na Halmashauri ya Ngara ni kuhakikisha vijana wanajipatia ajira na kipato pia mradi huo hutumika kujinfunza kilimo cha parachichi kutafuta masoko ili kuuza na kupata faida.  Shedrack amesema mradi huo weny...

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Yaiwakilisha Tanzania Mkutano Wa 63 wa Aalco

 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeiwakilisha Tanzania kushiriki Mkutano wa 63 wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) uliofanyika tarehe 8 hadi 12 Septemba, 2025 Jijini Kampala Uganda. Nchi wanachama wa Shirika hilo zilikutana kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kisheria hususani Kinga kwa Wakuu wa nchi dhidi ya jinai, Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Uhalifu wa Mitandao na ripoti ya utekelezaji wa majukumu ya vituo vya usuluhishi vya AALCO. Akizungumza kuhusiana na Mkutano huo Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Florentina Sumawe amesema kuwaTanzania imeshiriki mkutano huo kwa kuwasilisha mada juu ya hatua zilizochukuliwa katika Utekelezaji na Uzingatiaji wa Mikataba ya Kikanda na Kimataifa inayohusu Biashara na Uwekezaji, Sheria ya Bahari, Mazingira na Maendeleo Endelevu, Urejeshaji wa Mali zinazotokana na Uhalifu, na Utatuzi wa Migogoro kwa njia mbadala. Katua hatua nyingine, Bi. Sumawe a...

Wana-Lindi Tunasababu ya Kumchagua Rais Dkt. Samia-Majaliwa.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Wana-Lindi wanakila sababu ya kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 Mwaka huu. Amesema kuwa Rais Dkt. Samia amegusa matamanio ya Wana-Lindi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa imegusa maisha ya kila siku ya wakazi wa mkoa huo. Amesema hayo leo Jumamosi (Septemba 13, 2025) katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Lindi na Wilaya ya Ruangwa zilizofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Likangala, Ruangwa mkoani Lindi. “Tunayo sababu ya kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi, sote tunafahamu namna Rais Dkt. Samia alivyotekeleza miradi katika mkoa huu, kwenye sekta za elimu, afya, maji, barabara, uwezeshaji wananchi kiuchumi. Mkoa huu tunamiradi mikubwa itakayoufanya uchangamke na kuchachua uchumi wetu” Ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wa  Rais Dkt. Samia ipo miradi amba...

Mapokezi ya Dkt.Nchimbi Siha, Kilimanjaro Yanoga

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amewahutubia Wananchi  kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM,Kata ya Sanya Juu ndani ya jimbo la Siha, Wilayani Siha,akiendelea na mikutano yake ya Kampeni  leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro. Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi Wagombea Ubunge wa Mkoa huo akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Siha Ndugu Godfrey Mollel pamoja na Madiwani. Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na  sasa ameingia mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo ...

Othman wa Act Azindua Kampeni za Urais Zanzibar

 Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Septemba 13, 2025, azindua rasmi kampeni za ACT-Wazalendo Zanzibar katika viwanja vya Tibirinzi Kisiwani Pemba.