Skip to main content

Posts

Showing posts from August 31, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mzee Joseph Butiku alivyoibukia katika mkutano wa kampeni wa Dkt.Emmanuel Nchimbi Rorya

MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amekutana na kusaliamiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere Joseph Butiku wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu . Dk.Nchimbi ambaye alikuwa akiendelea na kampeni katika Mkoa wa Mara, alifanya mkutano katika Uwanja wa Ubwere Jimbo la Rorya,ambako alipokelewa na Butiku aliyekuwa moja ya viongozi waliokuwepo eneo la mkutano ambapo walisalimiana na kuteta kidogo kabla ya Dk.Nchimbi kuzungumza na maelfu ya wananchi waliofika kumsikiliza. Akihutubia wananchi wa Rorya mkoani Mara katika muendelezo wa mikutano ya kampeni Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rorya, Jafari Chege sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo. Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika ...
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Agosti 31, 2025 amewahutubia Wananchi wa Rorya waliofurika katika uwanja wa Ubwere, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya Kampeni kwenye mikoa ya kanda ya ziwa. Balozi Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea Mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Rorya, Jafari Chege sambamba na Wagombea Ubunge wengine pamoja na Madiwani wa Mkoa huo. Dkt. Nchimbi anaendelea na kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania  kuwaongoza katika awamu nyingine ya miaka mitano, katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.

Balozi Dkt Nchimbi Aomba Kura Kwa Wananchi wa Tarime Mjini

 Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akiwahutubia Wananchi wa Tarime mjini ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Kampeni zake ndani ya mkoa wa Mara. Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Tarime mjini,Balozi Dkt.Nchimbi akiwa ni mgombea mwenza wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pia alimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Tarime mjini, Esther Matiko,Wagombea Ubunge na Madiwani wa Mkoa huo. Dkt.Nchimbi ambae ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni katika harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.

Othman Achukua Fomu ya Urais Zanzibar

 Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Taifa, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Agosti 31, 2025, akisindikizwa na Viongozi wenzake Wakuu na Waandamizi wa Chama hicho, amefika huko Maisara Mijini Unguja, katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (ZEC), na kuchukua Fomu ya Kugombea Nafasi ya Urais wa Zanzibar. Mara baada ya kupokea Fomu hiyo, Mheshimiwa Othman,ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amepokelewa na pia kuwahutubia Umati wa Wanachama, Wapenzi na Wafuasi wake, pamoja na Wananchi kutoka Maeneo mbali mbali, huko Ofisi ya Makao Makuu ya ACT-Wazalendo Vuga, ndani ya Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja.

Nchimbi aomba kura Nyamongo na kumnadi Waitara kwa wananchi

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi leo Jumapili Agosti 31 ,2025 ameendelea na kampeni zake kwa kufanya mkutano mkubwa katika mji wa Nyamongo, jimbo la Tarime vijijini mkoani Mara. Balozi Dkt.Nchimbi pia aliwanadi Wabunge wa majimbo ya Mkoa huo ni pamoja na Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijini,Mwita Waitara Pamoja na Madiwani. Dkt.Nchimbi ameanza kampeni zake mkoani Mara jana Agosti 30, 2025 akitokea mkoa wa Mwanza, ikiwa ni harakati za kuomba ridhaa ya Watanzania walioko Kanda ya Ziwa katika Uchaguzi unaotarajiwa Kufanyika Oktoba 29, 2025.