Kampuni ya Meli Tanzania(TASHICO)imetoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la kupinduka kwa meli ya Mv.Serengeti lililotokea usiku wa kuamkia Desemba 26 mwaka huu katika Bandari ya Mwanza Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Paul Sebukoto amesema kuwa Meli hiyo imelalia upande wa nyuma baada ya maji kuingia ndani. ‘’Meli hii ilikuwa kwenye eneo la Maegesho,Maji yameingia ndani zikiwa zimepita kama siku mbili au tatu baada ya kufanyiwa ukaguzi uliobaini iko sawa,kwa hiyo ni lazima kutakuwa na chanzo ambacho kimesababisha maji kuingia ndani ya meli na kuipeleka chini upande wa nyuma’’alisema Sebukoto na Kuongeza kuwa ‘’Sasa tofauti na Tafsiri kuwa meli imepinduka au imezama ni kwamba meli hii haijapinduka wala haijazama isipokuwa tunasema imeegemea upande wa nyuma baada ya kulemewa na maji yaliyoingia ndani’’ Sebukoto amesema kuwa shughuli zinazofanyika kwa sasa ni kuinyanyua Meli hiyo kwa nyuma ili iweze kurudi kwenye hali yake ya...
Marato tv - Sauti ya Jamii