Skip to main content

Posts

Showing posts from September 25, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kikwete apokea msaada wa vifaa tiba na madawati kutoka Nmb

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani amepokea msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya hospitali ya Msoga na madawati 120 kwa ajili ya shule za msingi mbili za Chalinze. "Kwa mujibu wa takwimu za makusanyo na mapato, NMB- Chalinze ndiyo tawi namba moja Tanzania kwahiyo maana yake NMB wanapozungumza tunapata Bilioni 500 ni pamoja na mchango mkubwa wa Chalinze". Alisema Kikwete wakati akipokea vifaa hivyo.  Kikwete amezishauri zaidi sekta binafsi nyingine nyingi kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ili kuwa na uchumi endelevu na kurudisha kwa wananchi ambao ndiyo wateja wakuu. Tukio hilo muhimu la ustawi wa wananchi limefanyika mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Shaibu Ndemanga, Mkurugenzi wa Halmashauri Ramadhani Possi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe. Hassani Mwinyikondo huku benki ya NMB i...

Waziri Mkuu ateta na Mwenyekiti wa Bodi ya Citibank

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT). Amesema hayo jana (Jumanne, Septemba 24, 2024) mara baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani. “Serikali ya Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,” alisema. “Benki hii imekuwa ikikopesha makampuni yanayojenga reli yetu ya SGR na ili kuhakikisha wanachangia ujenzi wa uchumi wa Tanzania, na wao pia wamechukua lot moja ya ujenzi wa reli hiyo na kufadhili ujenzi wake. Hali kadhalika uendelezaji wa uwanja wa ndege wa Pemba.” Alisema Tanzania ilipokabiliwa na uhaba wa mafuta ya kuendeshea mitambo na magari, benk...