Skip to main content

Posts

Showing posts from December 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mavunde, Perseus Wajadili Maendeleo Mradi wa Nyanzaga

📍 Dar Es Salaam Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Desemba 2, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni mama ya Perseus na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga, Bi. Lee-Anne de Bruin ambao ni wawekezaji kwenye mgodi wa uchimbaji wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilayani Sengerema. Bi. Lee-Anne de Bruin aliongozana na Bw. Matt Cavedon, Meneja Mkuu na Mkurugenzi wa Bodi ya Mradi wa Nyanzaga na Bw. Isaac Lupokela, Afisa Mkuu wa Fedha wa Mradi wa Nyanzaga. Mazungumzo hayo yaliangazia hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa uanzishwaji wa mgodi huo ambao unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Nchi yetu na wananchi wa Sengerema. Aidha, Waziri Mavunde aliwahakikishia wawekezaji wa Perseus kuwa Wizara itaendelea kuwa bega kwa bega na wawekezaji katika kufanikisha uendelezaji wa Mgodi wa dhahabu wa Nyanzaga ili uweze kuleta mafanikio kwenye uchumi wa Tanzania na kusaidia upatikanaji wa Ajira kwa Watanzania wengi. *#InvestInTanzania*...

Azania Bank Yazindua Huduma Mbili Kuwanufaisha Wanavyuo na Wafanyakazi

Benki ya Azania hii leo imezindua huduma mbili mpya zitakazonufaisha Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu pamoja na Watumishi wa Umma na wale wa sekta binafsi zinazojulikana kama “Boom Advance” na “Salary Advance.” Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa Benki hiyo Bi.Elizabeth Nyattega alisema kuwa hatua hiyo ni muitikio wa mahitaji halisi ya wateja na ni ukombozi mkubwa kwa Wanavyuo na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi. “Boom Advance” ni huduma inayowalenga Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaopata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) ambapo sasa hawatalazimika kusubiri hadi mikopo yao iingie kwenye akaunti, bali wataweza kupata mkopo wa muda wenye masharti nafuu ili kujikimu wakati wakisubiri fedha kutoka Bodi ya mikopo”, alisema Nyattega huku akiongeza kuwa huduma ya “Salary Advance”yenyewe ni mahsusi kwa Watumishi wa Umma au sekta binafsi ambapo kupitia huduma hii mwajiriwa huyu ataweza kukopa sehemu ya mshahara wake kabla ya ta...

Katibu Mkuu wa Ccm Ashiriki Mkutano wa Wazee na Rais Samia

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro ameshiriki mkutano wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), leo Jumanne,Desemba 2,2025 Jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo maalum,mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Azania Bank yazindua Huduma mbili kuwanufaisha wanavyuo na wafanyakazi

Benki ya Azania hii leo imezindua huduma mbili mpya zitakazonufaisha Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu pamoja na Watumishi wa Umma na wale wa sekta binafsi zinazojulikana kama “Boom Advance” na “Salary Advance.” Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa Benki hiyo Bi. Elizabeth Nyattega alisema kuwa hatua hiyo ni muitikio wa mahitaji halisi ya wateja na ni ukombozi mkubwa kwa Wanavyuo na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi. “Boom Advance” ni huduma inayowalenga Wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaopata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) ambapo sasa hawatalazimika kusubiri hadi mikopo yao iingie kwenye akaunti, bali wataweza kupata mkopo wa muda wenye masharti nafuu ili kujikimu wakati wakisubiri fedha kutoka Bodi ya mikopo”, alisema Nyattega huku akiongeza kuwa huduma ya “Salary Advance” yenyewe ni mahsusi kwa Watumishi wa Umma au sekta binafsi ambapo kupitia huduma hii mwajiriwa huyu ataweza kukopa sehemu ya mshahara wake kabla ya ...

Tafiti na machapisho vyaipaisha CBE kimataifa

Na Mwandishi  Wetu SERIKALI imekipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kwa kuanzisha program atamizi ya biashara ambayo itawatengeneza wahitimu wa chuo hicho kuwa wafanyabiashara mahiri siku za baadae. Pongezi hizo zilitolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashill Abdalah, wakati wa mahafali ya 60 ya wanafunzi wa chuo hicho alipomwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga. Alipongeza kuanzishwa kwa program bunifu ambapo wanafunzi wenye mawazo ya biashara huyawasilisha chuoni hapo kwaajili ya kufanyiwa kazi yamekuwa na mchango mkubwa kuwafanya wanafunzi wasome biashara kwa vitendo na si nadharia. “Hawa wanafunzi wakihitimu watakuwa wafanyabiashara wakubwa ambao watajiajiri na kutengeneza ajira kwa wenzao, na kuongeza pato la taifa, mnaomaliza leo na mnaoendelea na wale ambao hamjajiunga na CBE mfahamu kuwa ndani ya chuo kuna fursa nyingi sana zitakazowakomboa kiuchumi,” alisema “Eendeleeni kuitumia elimu miyopata hapa CB...

Mkoa wa Katavi Wafungua Fursa Mpya za Uwekezaji Sekta ya Madini

Katavi, Desemba 02, 2025  Mkoa wa Katavi umeendelea kuwa kivutio cha wawekezaji kufuatia maboresho makubwa ya miundombinu, usalama na kasi ya utoaji leseni katika Sekta ya Madini.  Afisa Madini Mkazi wa mkoa huo, Mhandisi Andrew Mwalugaja, ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa zinazopatikana katika dhahabu, shaba, risasi, fedha, nikeli, manganese na madini ya ujenzi. Amesema kuwa ofisi yake imeongeza kasi ya utoaji leseni, ikiwemo leseni tatu za utafiti na zaidi ya leseni 300 za uchimbaji mdogo na wa kati ndani ya miezi minne. Katika biashara ya madini, leseni 82 tayari zimetolewa kati ya Julai na Oktoba 2025, hatua inayodhihirisha mwamko mkubwa wa uwekezaji. Serikali imeanzisha masoko mawili ya madini Mpanda na Karema ili kuhakikisha wachimbaji, hususan vijana, wanapata soko la uhakika na kufanya shughuli zao kwa uwazi zaidi. Hadi sasa, mkoa umefanikiwa kuongeza makusanyo ya maduhuli hadi Shilingi bilioni 3.80 ndani ya miezi minne tu. Wachimbaj...