Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM, Taifa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe, Ndugu Doto Mashaka Biteko amewahimiza wananchi wa Jimbo la Sumve, wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kuwa Chama hicho kimefanya jitihada kubwa ya kuwaletea maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 21, 2025 Kwimba - Mwanza wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve kwa tiketi ya CCM, Moses Bujaga ikiwa ni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Amesema Serikali ya CCM imeendelea na jitihada zake za kujenga Kituo cha Reli ya Kisasa ya SGR kwa ajili ya kupokea mizigo itakayosafirishwa kwenda maeneo mbalimbali pamoja na kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Mwanza ili kufungua uchumi wa mkoa huo kwa ujumla. Aidha, imehakikisha wananchi wa vijiji vyote katika Jimbo hilo wanapata umeme ikiwa ni pamoja na usambazaji umeme katika vitongoji. Dkt. Biteko ameendelea kusema Dkt. Samia Suluhu Hass...
Marato tv - Sauti ya Jamii