Skip to main content

Posts

Showing posts from July 14, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

UONGOZI WA JUU IPU WAKUTANA NA SPIKA ZUNGU NEW YORK, WAPOKEA HAKIKISHO LA UENYEJI WA MKUTANO WA 153 JIJINI ARUSHA

Na Prosper Makene New York, Marekani– Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Musa Azzan Zungu, ameuhakikishia Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kuwa Tanzania imejipanga kikamilifu kuandaa Mkutano wa 153 wa IPU utakaofanyika Oktoba 2026 jijini Arusha. Mhe. Zungu ametoa hakikisho hilo wakati wa kikao na Rais wa IPU, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mbunge, pamoja na Katibu Mkuu wa IPU, Balozi Anda Filip jijini New York, Marekani. Kikao hicho kililenga kupitia hali ya maandalizi, mipango ya kilojisti na uhakika wa utayari kabla ya mkutano huo mkubwa wa kibunge duniani. Spika ameeleza kuridhishwa na kazi ya Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi inayoratibu tukio hilo. Amesema mipango yote ya kilojisti, kiprotocol na usalama inaendelea kama ilivyopangwa, na Tanzania imejitolea kutoa ukaribisho wa kiwango cha kimataifa. Mhe. Zungu amesisitiza kuwa kuandaa mkutano huo ni jambo la fahari kwa Taifa na ni fursa muhimu ya kuimarisha nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kibunge duniani. Ameongez...

IPU LEADERSHIP MEETS SPEAKER ZUNGU IN NEW YORK, RECEIVES ASSURANCE OF TANZANIA’S READINESS TO HOST 153RD ASSEMBLY IN ARUSHA

By Prosper Makene New York, USA– The Speaker of the Parliament of the United Republic of Tanzania, Hon. Musa Azzan Zungu, MP, has assured the Inter-Parliamentary Union (IPU) that Tanzania is fully ready to host the 153rd IPU Assembly scheduled for October 2026 in Arusha. Hon. Zungu made the assurance during a meeting with the IPU President, Hon. Dr. Tulia Ackson, MP, and the IPU Secretary General, Ambassador Anda Filip in New York, USA.  The meeting focused on reviewing the status of preparations, logistical arrangements, and overall readiness ahead of the global parliamentary gathering. The Speaker expressed satisfaction with the work of the National Organizing Committee that has been coordinating the event. All logistical, protocol and security arrangements are progressing according to plan, and that Tanzania is committed to delivering a world-class Assembly that reflects Tanzanian hospitality and efficiency. Hon. Zungu emphasized that hosting the Assembly is a matter of national...

KIFUNGO KILICHOBADILI MAISHA: MWENDWA AMSHUKURU HAKIMU ALIYEMHUKUMU

 LAMU, Kenya:  Baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani, mwanamume aitwaye Mwendwa Kilatya alirejea kumtafuta Hakimu Mkazi Eugene Pascal Nabwana, aliyekuwa amemhukumu katika Mahakama ya Mpeketoni, Kaunti ya Lamu, ili kumshukuru na kumuomba msaada wa kuendelea na masomo ya chuo kikuu. Kilatya alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela kwa kosa la wizi wa mifugo. Kabla ya hukumu hiyo, alikuwa ameacha shule akiwa Kidato cha Tatu, licha ya kuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya vizuri darasani. Akiwa gerezani, aliamua kurejea masomoni na kufaulu kwa matokeo mazuri, jambo lililompa matumaini ya kuendelea na elimu ya juu baada ya kumaliza kifungo chake. Baada ya kuachiwa huru, Kilatya alisafiri hadi Mahakama ya Wamunyu, Kaunti ya Machakos, ambako Hakimu Nabwana alikuwa amehamishiwa, ili kumshukuru kwa uamuzi wake ambao anasema ulimsaidia kubadili maisha yake na kumwelekeza katika njia sahihi. Akiguswa na simulizi na juhudi za Kilatya, Hakimu Nabwana aliahidi kuwashirikisha ...

SAKATA LA MAGENDO HOROHORO: WAZIRI WA FEDHA AAGIZA DORIA KALI, AONYA HATARI KWA USALAMA WA TAIFA

Na MASHAKA MHANDO, Horohoro  SERIKALI imeagiza kuimarishwa mara moja kwa doria na msako mkali dhidi ya biashara haramu ya magendo katika mpaka wa Horohoro, uliopo Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, ikiwa ni hatua madhubuti ya kudhibiti uvujaji wa mapato na kulinda usalama wa Taifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, alipofanya ziara ya kimkakati katika Kituo cha Forodha cha Horohoro kujionea shughuli za ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa biashara ya kimataifa kati ya Tanzania na Kenya. Balozi Omar aliweka wazi kuwa udhibiti wa magendo sio tu suala la kuongeza mapato ya Serikali, bali ni msingi mkuu wa kulinda usalama wa nchi na kuhakikisha Taifa linakuwa na takwimu sahihi za kiuchumi. Jukumu Sio Kukusanya Mapato Tu Waziri huyo aliwapongeza maofisa wa forodha kwa kazi wanayofanya, lakini aliwataka kuongeza umakini maradufu kudhibiti bidhaa zilizopigwa marufuku kuingia nchini na zile zinazokwepa kufuata masharti ya kisheria. "Tusipotekeleza jukumu...

SERIKALI YAAHIDI KUTOA SH. MIL 750 KUMALIZA KITUO CHA AFYA

 NA MASHAKA MHANDO, Tanga SERIKALI imetoa ahadi ya kutoa Shilingi milioni 750 ili kukamilisha ujenzi wa majengo yaliyosalia katika Kituo kipya cha Afya cha Maweni, jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha huduma za afya  kwa wananchi. Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar  wakati wa ziara yake ya kikazi jijini Tanga ambapo alikagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kituo cha afya Maweni sambamba na mradi wa mabweni katika shule ya sekondari Usagara na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa. Balozi Omar alibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026, Serikali imejitahidi kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika Mkoa wa Tanga kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo. "Kwa mwaka huu wa fedha uliopita, Mkoa wa Tanga ulipangiwa kutumia Shilingi bilioni 528.1, na Serikali imewasilisha kiasi cha bilioni 487.5. Hii ni zaidi ya asilimia 92 ya fedha zote za maendeleo zilizopangwa," alisisitiza Balozi Omar. Katika hali ya kuonyesha kuridhishwa na usim...