Skip to main content

Posts

Showing posts from October 14, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Misungwi kuandikisha wapiga kura 232,128 katika daftari la makazi

Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la makazi linaendelea vyema katika Halmashauri ya wilaya Misungwi Mkoani Mwanza ambapo zaidi ya wapiga kura  elfu thelathini tayari wameandikishwa katika daftari hilo. Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Dickson Kawovela amesema kuwa idadi hiyo ambayo ni sawa na asilimia 33 inajumuisha wanaume 33,234 pamoja na wanawake 35,291. Akizungumza wakati wa kukagua zoezi la uandikishaji katika kata ya misungwi,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya misungwi,Addo Missama amesema kuwa mwelekeo ni mzuri na matarajio ni kufikia malengo ya kuandikisha watu 232,128. Missama amewaasa wananchi ambao hawajajiandikisha kutumia siku zilizosalia kujiandikisha ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umepangwa novemba 27 mwaka huu. ‘’Nahamasisha kila mmoja kutumia haki yake kuanzia zoezi lilipoanza oktoba 11 hadi 20 mwaka huu kuweza kujiandikisha na waweze kuwa katika nafasi ya kupiga kura na kuchagua vio...