Skip to main content

Posts

Showing posts from May 23, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Hatifungani ya miundombinu ya barabara kusaidia kukamilisha ujenzi wa barabara

Dodoma Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara (Samia Infrastructure Bond) inaenda kuondoa changamoto ya kutokamilika kwa wakati  kwa ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara kutokana na ucheleweshaji wa malipo kwa makandarasi. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Wakala ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA), Bi. Catherine Sungura wakati akijibu katika kikao kazi cha Maafisa Habari wa Mikoa, Halmashauri na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma. Alisema katika bondi hiyo, TARURA kwa kushirikiana na Benki ya CRDB imefanikiwa kukusanya bilioni 323 ambazo zitaenda kutumika kuwakopesha Makandarasi wazawa ili waweze kukamilisha ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa wakati. Katika hatua nyingine, Bi. Sungura alisema TARURA itaendelea kushirikiana na maafisa habari kwenye Halmashauri katika kutangaza kazi kubwa ya ujenzi na matengenezo ya miundumbinu ya barabara nchini.

Wananchi Lindi watakiwa kuchangamkia fursa za madini

  *Waaswa kuacha uvivu* · *Mgodi wa Elianje, injini ya maendeleo Namungo* WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha uvivu na badala yake wachangamkie fursa zilizopo kwenye sekta ya  madini hususani katika mgodi wa kati  wa Elianje uliopo kitongoji cha Namungo, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti  wa  Kijiji  cha  Chingumbwa, kilichopo Kata ya Namungo, Abdallah Rashid akielezea fursa zilizopo mkoani humo kupitia Sekta ya Madini. “Fursa zipo nyingi ni uvivu tu wa wananchi wetu, ukiangalia kwenye mgodi huu unaotuzunguka wa Elianje Genesis kuna fursa ya usambazaji vyakula, vinywaji, usafi, kupika, kusambaza vifaa vya usalama migodini, uchimbaji na uchenjuaji lakini ndio hivyo,”amesema Abdallah Aidha, Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa mgodi huo umetoa manufaa makubwa kwa wananchi kwa kuchimbiwa kisima cha maji ambacho kwa sasa kinahudumia kaya 918, awali kulikuwa na shida ya maji na wananchi walilazimika kutembea umbali mrefu k...

Lindi watakiwa kuchangamkia fursa za madini

  · *Waaswa kuacha uvivu* · *Mgodi wa Elianje, injini ya maendeleo Namungo* WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kuacha uvivu na badala yake wachangamkie fursa zilizopo kwenye sekta ya madini hususani katika mgodi wa kati wa Elianje uliopo kitongoji cha Namungo, Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chingumbwa, kilichopo Kata ya Namungo, Abdallah Rashid akielezea fursa zilizopo huko kupitia Sekta ya Madini. “Fursa zipo nyingi ni uvivu tu wa wananchi wetu, ukiangalia kwenye mgodi huu unaotua wa Elianje Genesis kuna fursa ya kuchunguza masuala, usafi, kupika, kusambaza vifaa vya madini, uchimbaji na uchenjuaji lakini ndio hivyo,” amesema Abdallah. Aidha, Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa mgodi huo umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi kwa kuchimbiwa kisima cha maji ambacho kwa sasa kinahudumia kaya 918, awali na shida ya maji na wananchi walilazimika kutembea muda mrefu kuchota maji. “Pia, mwekezaji ametujengea shule ambayo kwa sasa ina wanaf...

Madini ya Almasi yenye thamani ya Bilioni 1.7 yakamatwa uwanja wa ndege Mwanz

Waziri Mavunde awapongeza RC Mtanda,Kamati ya Usalama,Uwanja wa Ndege na Kikosi kazi Madini ▪️Aelekeza uchunguzi zaidi kubaini mtandao wote wa wahusika ▪️Atoa rai kwa wadau wa madini kuzingatia sheria ya biashara ya madini nchini ▪️Raia wa Kigeni mwenye asili ya India ashikiliwa  *Mwanza* Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya. “Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na tar...

Kesi za Kupinga Kuondolewa Kwa Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua Kuanza upya

  JAJI Mkuu wa Kenya Martha Koome amedumisha jopo la majaji walioteuliwa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kusikiliza kesi zinazopinga kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Kupitia taarifa rasmi, Jaji Koome alimteua Jaji Eric Ogola kuwa mwenyekiti wa jopo hilo, akishirikiana na Majaji Anthony Mrima na Dkt. Freda Mugambi. Kesi hizo zitatajwa Mei 29 kwa mwelekeo. “Mheshimiwa Jaji Mkuu ameteua jopo la majaji wafuatao kusikiliza kesi hizi: Mheshimiwa Jaji E Ogola (mwenyekiti), Mheshimiwa Jaji A. Mrima na Mheshimiwa Jaji Dkt  F Mugambi,” ilieleza notisi kwa mawakili. Bw Gachagua alipinga uteuzi wa majaji hao uliofanywa na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, akidai kuwa mamlaka ya kuteua majaji ni ya Jaji Mkuu pekee. Mnamo Mei 9, Majaji Daniel Musinga, Mumbi Ngugi na Francis Tuiyott wa Mahakama ya Rufaa walikubaliana naye, wakisema kuteua majaji ni jukumu la kikatiba la Jaji Mkuu na haliwezi kuhamishiwa Naibu Jaji Mkuu. “Ni lazima tukumbuke kuwa wajibu wa ku...

Wananchi Wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Waipongeza Rea Kwa Usambazaji Wa Mitungi Ya Gesi Ya Kilo Sita Kwa Bei ya Ruzuku

📌REA yaendelea na usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilaya ya Handeni mkoani Tanga. 📌Mitungi ya gesi ya kilo sita 26,040 kusambazwa mkoani Tanga.  📌Mitungi ya gesi ya kilo sita 3,255 kusambazwa kila wilaya. Wananchi wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga waipongeza REA kwa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku.  Mitungi hiyo inasambazwa kila wilaya kwa bei ya ruzuku ya shillingi 17,500 na kila wilaya  idadi ya mitungi 3,255 kusambazwa. Usambazaji wa mitungi hiyo, unaunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia suluhu Hassan, ya kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka 2034 asilimia themanini (80) ya watanzania wawe wanatumia Nishati safi ya kupikia. Mitungi hiyo inasambazwa kwa bei ya ruzuku ili kumuwezesha kila mtanzania wa hali  yoyote kuwa na uwezo wa kutumia Nishati nishati safi na salama ya kupikia. Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dk. Samia suluhu Has...