Skip to main content

Posts

Showing posts from January 2, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Kawaida aendelee Kuimarisha Uvccm upande wa Zanzibar

02 JANUARY 2025. 🔰 KISIWANDUI  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) Amefungua Mafunzo ya wajumbe wa UVCCM Unguja. #TunazimazoteTunawashakijani #Kijananakijani Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi,  Afisi kuu UVCCM Zanzibar

Mbunge Kembaki achukizwa na Mbunge wa Kenya Kuhamasisha Katiba Mpya Tanzania

Na Helena Magabe Tarime. MBUNGE wa Jimbo la Tarime mjini Michael Kembaki katika kuelekea kufunga mwaka amesema ulinzi na usalama Tarime uko vizuri licha ya kuwa amekerwa na Mbunge wa Kurya Magharibi Nchini Kenya Matias Rhobi kuhamasisha katiba mpya nchini katika Jimbo lake na kuleta uchochezi kwa wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kitendo cha mbunge huyo kuchochoe wananchi kudai katiba mpya akiwa kwenye sherehe aliyoalikwa na Moja ya mtia nia ,akihoji kwanini Mbunge hakufika na kudai kuwa hakuna maendeleo Tarime ,hakuna bara bara za rami ni kitendo ambacho kimemkera na ni uvunjifu wa sheria za Nchi. Amesema Mbunge huyo anatakiwa kufanya maendeleo Nchini kwake hasa kwenye Jimbo lake ambalo yeye si mgeni anazijua bararabara za jimboni kwake zilivyo mbovu hasa njia ya Kehancha ambayo ilijengwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita hakuna maendeleo aliyofanya na Bungeni kwake ni Mbunge Bubu ambaye haongelei Jimbo lake na hayuko kwenye rekodi ya vyombo vya hab...

Wakili Mbedule aomba Wananchi Kujitokeza Kuhakiki Taarifa zao Katika Daftari la Wapiga Kura Iringa

Wakili Mbedule ataka wananchi Ikuvilo kuhakiki taarifa zao Mwandishi Wetu ;Iringa WANANCHI wa kijiji cha Ikuvilo kata ya Luhota wilaya ya Iringa vijijini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao. Hayo yamesemwa na mdau wa maendeleo na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wakili Sosten Mbedule mara baada ya kuhakiki taarifa zake. Amesema, ni vema kila mwananchi kuhakiki taarifa zake ili aweze kutumia haki zake za msingi kuchagua viongozi wanaowataka  "Wananchi wa kijiji cha Ikuvilo wanatakiwa kutumia fursa hii, kwenda kwenye kituo cha kupiga kura na kuhakiki taarifa zake, kuepuka usumbufu hapo badae," amesema na kuongeza "Wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea ofisa uchaguzi atawasaidia taratibu za kufanya ili wapate kadi mpya," amesema Wakili Mbedule  Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba 2025, wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Dkt. Biteko ahimiza upendo, Kuvumiliana Katika Kuleta Maendeleo Nchini

*📌Asema Rais Samia anaendelea kuweka Historia Nchini* *📌Asema Rais amenuia kupunguza changamoto za Watanzania* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Dkt. Doto Biteko amewahimiza Watanzania kuendeleza upendo mshikamano na kuvumiliana zikiwa nyenzo muhimu za kufikia maendeleo na ustawi wa Taifa. Dkt. Biteko amesema hayo Kijijini kwao Bulangwa, Wilayani Bukombe Mkoani Geita alipojumuika na maelfu ya wananchi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2025. Amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi makubwa na mazuri ambayo yanahitaji kuenziwa na kuendelezwa ili kupata maendeleo ya kweli. "Maono ya Rais Samia yamewezesha upatikanaji wa maendeleo katika sekta mbalimbali kama ujenzi wa miundombinu ya barabara, shule, vituo vya Afya na maji na hatua hii imetambuliwa kitaifa na kimataifa" amesema Dkt. Biteko Amesema pia kuwa maendeleo yaliyof...

Waziri Mkuu amwakilisha Rais Dkt. Samia Kuaga Mwili wa Marehemu Jaji Werema

_▪️Rais Dkt. Samia asema Jaji Werema alikuwa kiongozi mwenye misimamo_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Januari 02, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuaga mwili wa marehemu Jaji Fredrick Werema ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2009-2014. Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia amesikitishwa na kifo cha Jaji Werema na amemtaja kama kiongozi shupavu aliyekuwa anazingatia maadili wakati wote na mwenye misimamo katika utendaji kazi wake. Tukio la kuaga Mwili wa Jaji Werema limefanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.  “Mheshimiwa Rais anajua kwamba Marehemu amefanya kazi katika mihimili yote na anauzoefu mkubwa wa utendaji katika mihimili yote, mengi mazuri ameyatenda, Rais Dkt. Samia anawasihi wote muwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na ametusihi tuendelee kumuombea na kuyaenzi yote aliyoyafanya katika utumishi wake”. Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amewataka amewataka wana...