Skip to main content

Posts

Showing posts from March 16, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MwanaFA, Kingwendu wafanya mazungumzo ya kimkakati kuhusu sanaa

Na Mashaka Mhando NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amekutana na kufanya mazungumzo na msanii mkongwe wa vichekesho nchini, Kingwendu, yaliyolenga kujadili fursa za kimaendeleo katika sekta ya sanaa. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, Mwinjuma amesema Wizara imejizatiti katika kuimarisha mazingira yatakayowawezesha wasanii, hususan wakongwe, kunufaika na kazi zao kupitia mifumo rasmi ya kibiashara. Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wasanii wakongwe katika kujenga tasnia ya sanaa na vichekesho nchini, hivyo kuna haja ya kuoanisha uzoefu wao na fursa mpya zinazojitokeza katika soko la sasa la kidijitali. “Tumekutana na Kingwendu kujadili namna wasanii wetu wanavyoweza kutumia fursa mbalimbali za kimaendeleo zinazojitokeza hivi sasa ili kusaidia ukuaji wa sekta ya sanaa na mnyororo mzima wa thamani,” amesema Mwinjuma. Kwa upande wake, msanii Kingwendu amepongeza hatua ya Wizara kuwa karibu na wadau wa sanaa, akieleza ...

Waziri Mkuu Asitisha Ziara Kupisha Kumbukizi ya Miaka Mitano ya Hayati Dkt. Magufuli

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ziara yake ya kikazi katika mikoa mbalimbali nchini itasimamishwa kwa muda kupisha kumbukizi ya miaka mitano ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, inayofanyika Machi 17, 2026. Akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Ikulu Ndogo ya Mpanda mkoani Katavi, Jumatatu Machi, 16, 2026 Waziri Mkuu alisema Serikali itaungana na Watanzania katika kumbukizi hizo za kitaifa za kumuenzi kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.  “Kesho hatutaendelea na ziara. Kama mnavyokumbuka ni siku muhimu kwa Watanzania wote, ikiwa ni kumbukizi ya miaka mitano ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Kwa heshima hiyo kesho hatutakuwa na ziara,” amesema. Amesema kumbukizi hizo zinafanyika kwa heshima ya kiongozi huyo aliyegusa maisha ya Watanzania wengi na kuacha historia kubwa katika uongozi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini. Aidha, ...

Makamu wa Rais Mgeni Rasmi Miaka Mitano ya Kifo Cha John Pombe Magufuri

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato mkoani Geita, leo tarehe 16 Machi 2026. Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka Mitano ya Kifo cha Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, itakayofanyika kesho tarehe 17 Machi 2026 Chato mkoani Geita.

Tuhukumu kwa haki kulinda amani-Makamba

NA MASHAKA MHANDO, Tanga MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Januari Makamba, ametoa wito kwa viongozi na wenye mamlaka nchini kutoa hukumu kwa haki, hekima na busara ili kulinda amani, umoja na mshikamano wa kijamii utakaorithishwa kwa vizazi vijavyo. Makamba ambaye alikuwa mbunge wa Bumbuli na Waziri wa zamani, ametoa kauli hiyo Leo Machi 16  jijini hapa wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, viongozi wa dini, na wadau wa maendeleo katika hafla ya Iftar iliyoiandaa na marafiki zake wa jiji hilo kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort. Katika hotuba yake iliyojaa hisia, Makamba amesisitiza kuwa mshikamano ulioonyeshwa na wananchi waliojitokeza kwa wingi ni kielelezo cha "urithi wa Tanga ya zamani" inayozingatia upendo, kutembeleana na kushirikiana bila kujali tofauti zao. "Mmenipa heshima kubwa sana. Huu ni utamaduni wetu watu wa Tanga wa kupendana na kushirikiana. Ombi langu kwa walimu na masheikh ni dua; tuiombee nchi yetu na viongozi wetu, lakin...

Mhe Esther Matiko Ashiriki Mazishi ya Frank Peter Zakaria Mjini Tarime

Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther Matiko ameshiriki mazishi ya Frank Peter Zakaria mtoto wa Chief Peter Zakaria mjini Tarime. Akizungumza na waombolezaji wa msiba huo, Mhe Esther Matiko ametoa salamu za pole na rambirambi kwa familia ya Chief Peter Zakaria kwa kuondokewa na kijana wao mpendwa. Sambamba na salamu hizo za pole Mhe Esther Matiko ameyaelezea mahusiano chanya ya Frank na wananchi wa Tarime, Nyamongo, Mwanza na kwingineko alikopata kuishi siku za uhai wake. “Leo hii tumekusanyika hapa kwa wingi kuomboleza kifo cha Frank umati huu wote ni kwa sababu ya mahusiano chanya Chief Peter Zakaria kwa wananchi wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla. Kata ya Turwa hatukuwa na eneo la kujenga kituo cha afya lakini Chief Peter Zakaria ametupatia eneo zaidi ya hekali 4 bure kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya” amesema Mhe Esther Matiko Akihitimisha salamu za pole na rambirambi kwa wafiwa na waombolezaji Mhe Esther Matiko amewashukuru Wananchi wa Tarime mjini na waombolezaji wote ...

Bodi Mpya ya NCT Yatakiwa Kusimamia Ubora na Ukarimu Kwa Wateja.

Na. Sixmund Begashe, DSM Bodi mpya ya Ushauri ya Wizara ya Wakala wa Chuo cha Utalii Tanzania , imeelekezwa kufanya tafiti na kuboresha mitaala ya Chuo hicho ili kiendelee kuzalisha wataalam wenye sifa na ubora zaidi hususan katika eneo la huduma kwa wateja na ukarimu. Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua bodi hiyo yenye wajumbe 7.  Dkt. Kijaji amesema kuwa, kazi kubwa imefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza vivutio vya utalii, hali inayopelekea watalii wengi kumiminika nchini, hivyo ni vyema chuo hicho kikaliangalia ipasavyo eneo la ubora wa huduma kwa wateja na ukarimu. " Uwepo wa wataalam hao kutaendelea kushawishi watalii kurejea nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio vyetu na hivyo kutuwezesha kufikia lengo tulilowekewa la watalii milioni 8 ifikapo Mwaka 2030". Alisema Dkt. Kijaji Aidha Dkt. Kijaji ameupongeza  uongozi wa Chuo cha T...

Waziri Mkuu Ahitimisha Ziara Yake Mkoani Katavi

_▪︎ Aagiza viongozi kushughulikia kero za wananchi badala ya kusubiri viongozi wakuu_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 16, 2026 amehitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Katavi iliyoanza Machi 13, 2026 ambapo ameelekeza viongozi wa wilaya na halmashauri nchini kuhakikisha wanashughulikia changamoto za wananchi kwa wakati bila kusubiri ziara za viongozi wa kitaifa. Akizungumza na Viongozi hao katika kikao cha majumuisho kilichofanyika Ukumbi wa Katavi Social Hall, Manispaa ya Mpanda, Waziri Mkuu alisema mfumo wa ugatuaji wa madaraka unalenga kuwapa viongozi wa maeneo uwezo wa kutatua changamoto za wananchi katika ngazi zao.  “Sio lengo la muundo wetu wa Serikali ugatuaji wa madaraka kwamba mambo yatatuliwe panapokuwa na ziara za viongozi wa kitaifa. Hoja zote tulizosikiliza zimeandikwa, nendeni mkazifuatilie moja baada ya nyingine na mzifikishe mwisho,” alisema. *Sekta ya Elimu* Katika sekta ya elimu, Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Tanganyika ...

Waziri Mkuu Aagiza Uchunguzi wa Ununuzi Wa Mabati 4,000 Mabovu Katika Ujenzi wa Shule ya Katavi Boys

_Aagiza mkandarasi na watumishi waliohusika wakamatwe mpaka fedha zitakaporejeshwa_ _Ataka viongozi waliohusika na ubadhirifu wa mbolea za milioni 91 waondolewe madarakani_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu ununuzi wa mabati yasiyokidhi viwango yaliyokusudiwa kutumika katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Katavi (Katavi Boys), hatua iliyosababisha Serikali kutoa fedha mara mbili kwa ajili ya ununuzi wa mabati. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Machi 16, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Maridadi, Mpanda Mjini mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alihoji mchakato wa ununuzi wa mabati takribani 4,000 yenye thamani ya karibu shilingi milioni 198, ambayo yalibainika kuwa hayakukidhi viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.  “Takribani milioni 200 imenunua mabati yasiyofaa. Nani a...

Januari Makamba Atoa futari kwa taasisi za dini Tanga.

Na Mashaka Mhando, TANGA MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Januari Makamba, ametoa msaada wa futari kwa taasisi nane za kidini jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono waumini katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Zoezi hilo lililofanyika Leo Machi 16 Jijini Tanga, limenufaisha taasisi za TAMTA, Maawal Chumbageni, Zahara Rashad, Shamsi Maarifa, Sururu, Noor-Hudaa, Abutwalib pamoja na Anisa. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Makamba amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha mshikamano, upendo na utamaduni wa kusaidiana, hususan kwa makundi yenye uhitaji katika kipindi hiki cha funga. “Taasisi za dini zina nafasi kubwa katika kulea maadili mema kwa vijana na jamii kwa ujumla. Ni muhimu kuendelea kuzisaidia na kushirikiana nazo ili zijikite katika kutoa malezi bora,” amesema Makamba. Kwa upande wao, viongozi na wanafunzi wa taasisi hizo wameishukuru hatua hiyo wakieleza kuwa msaada huo utasaidia kupunguza mahitaji ya chakula kwa wanafunzi na waumini wanaofanya ibada...