📌 Dkt. Biteko afungua tawi la Exim Benki Kahama 📌 Exim yachangia vifaa vya matibabu vya shilingi milioni 25 Hospitali ya Wilaya Kahama Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Bank Kahama ni uthibitisho wa ukuaji wa sekta ya benki, ushirikiano wa sekta binafsi na Serikali na dhamira ya kukuza uchumi wa wananchi. Aidha, Serikali imekuwa ikihimiza taasisi za fedha kuipeperusha bendera ya Tanzania nje ya nchi kwa kufanya uwekezaji wa kimkakati. Hayo yameelezwa leo Februari 25, 2025 Kahama mkoani Shinyanga na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akizindua tawi la Benki ya Exim. “ Kahama ni kitovu kikubwa cha shughuli za kiuchumi, hasa sekta ya madini ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa. Zaidi ya madini, mji huu pia ni maarufu katika sekta ya kilimo na biashara. Ni wazi kuwa ufanisi wa sekta hizi unategemea upatikanaji wa huduma za kifedha imara na zinazokidhi mahitaji ya wajasiriamali na wafanyabiashara,” amesema ...
Marato tv - Sauti ya Jamii