Skip to main content

Posts

Showing posts from January 8, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Kijaji Aipa Tano Bodi ya Tawa

Na, Sixmund Begashe, Arusha Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imepongezwa  kwa ubunifu wake katika utekelezaji wa majukumu yake  yaliyosababisha mafanikio katika uhifadhi na Utalii nchini.  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa pongezi hizo Jijini Arusha wakati akipokea taarifa ya  utekelezaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA inayomaliza muda wake.  Dkt. Kijaji amesema ubunifu katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo, umeendana sambamba na maono ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uhifadhi endelevu wa urithi wa  rasilimali kwa maslahi ya vizazi vijavyo na Taifa kwa ujumla.  Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, Bodi hiyo  imewezesha  kuongezeka kwa  wawekezaji na mapato kusababisha kuimarika kwa uhifadhi, kupungua kwa uvamizi katika maeneo ya hifadhi na mapori tengefu pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia licha ya...

Dkt. Mwigulu Anazungumza na Machinga, Madereva Pikipiki na Bajaji

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 08, 2026 anazungumza na Wamachinga, madereva pikipiki na bajaji za kubeba abiria katika kongamano la mwaka linalofanyika kwenye kituo  cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini (JNICC) Dar es Salaam. Kongamano hilo lina lengo la kuwakutanisha wadau wote wakuu wa sekta ya wamachinga na usafirishaji wa pikipiki na bajaji ili kutafakari  mustakabali wa kazi zao katika maendeleo ya jamii na Taifa letu.