Skip to main content

Posts

Showing posts from March 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nyansaho Awapa Tumaini Jipya Wananchi wa Tarime

>>Ni kuhusu barabara ya TANROADS iliyogeuka mashimo NA MWANDISHI WETU, Tarime  MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara, Dkt. Rhimo Nyansaho, amewapa matumani wakazi wa wilaya Tarime kuhusu matenegenezo ya barabara ya Tarime-Mogabiri ambayo imechimbika mashimo kwa muda mrefu sasa. Ni barabara inayotumiwa na maelfu ya wasafiri wakiwemo watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti na magari ya biashara kati mji wa Tarime, Nyamongo na Serengeti. Barabara hiyo ipo chini ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), lakini imebaki kulalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu sasa wakiomba itengenezwe bila mafanikio.  “Naona nilisemee jambo hii, uhakika ni kwamba barabara hii imewekwa kweye mpango wa matengenezo na mkandarasi alishapatikana,” Dkt. Nyansaho ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alisema Jumatatu iliyopita. Dkt.  Nyansaho aliyasema hayo mjini Tarime wakati akitoa salamu za pole kwenye mazishi ya Frank Peter Zakaria (41), kijana wa mf...

Balozi Dkt Nchimbi Mgeni Rasmi Maadhimiho Siku ya Misitu Diniani, Kitaifa Mkoani Lindi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wakati akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, ili kuelekea mkoani Lindi, leo tarehe 18 Machi 2026.   Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Kampeni ya Upandaji Miti Kitaifa, itakayofanyika mkoani Lindi, kesho tarehe 19 Machi 2026.

Kongole Wizara ya Maji kwa mafanikio ya programu ya WSDP

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Wizara ya Maji inatekeleza programu mbalimbali za kimaendeleo zenye lengo la kuboresha usambazaji wa maji kwa wananchi wake na kufanikisha miradi mingine ya umwagiliaji ambayo ni kichochea muhimu kwa ustawi wa shughuli za kiuchumi kama kilimo, viwanda na huduma nyingine za kijamii. Miongoni mwa mipango inayosimamiwa na Wizara ya Maji yenye lengo la kuchochea kasi ya usambazaji wa maji kwa wananchi ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (Water Sector Development Programme - WSDP) ambayo sasa imetimiza miaka ishirini tangu ilipozinduliwa mwaka 2006.  Machi 16 hadi Machi 22, 2026, Wizara ya Maji inaadhimisha Wiki ya Maji ambapo kilele chake ni Machi 22 ambayo ni Siku ya Maji Duniani. Katika Wiki ya Maji, Wizara ya Maji inaratibu makongamano, mijadala na maonyesho mbalimbali yenye lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya maji na kuonyesha mafanikio yaliyofikiwa katika usambazaji wa huduma ya maji. Machi 17, 2026, Waziri wa Fedha, Baloz...

Watoto 832,448 Mkoani Mara kupatiwa Chanjo ya polio ya Matone

 Na Ada Ouko, Musoma. JUMLA ya watoto 832,448 walio na umri chini ya miaka 10, Mkoani Mara wanatarajiwa kupata chanjo ya polio ya matone kupitia kampeni maalumu itakayofanyika kuanzia march 24 hadi 27 mwaka 2026, katika mikoa ya kanda ya ziwa. Hayo yamebainishwa march 17,2026 na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Zabron Masatu wakati akiendesha mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mkoa huo juu ya uelewa wa magonjwa 14 yanayozuilika kwa chanjo ukiwemo ugonjwa wa polio. "Tunatarajia kuwa na kampeni ya chanjo ya polio ya matone ambayo tutaitoa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri mkuu Tamisemi na wadau wa maendeleo ambao tunafanya nao kazi hapa nchini.. "Kampeni hii itafanyika katika mikoa saba ya kanda ya ziwa ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora, Kampeni hii itaanza march 24-27 mwaka huu 2026" Amesema kuwa kampeni ya chanjo ya polio itazinduliwa kitaifa katika mkoa wa Mwanza na Waziri wa afya Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ma...

Wamiliki wa leseni za madini wafundwa, Tume yasisitiza utekelezaji wa sheria

Dodoma, Machi 18, 2026 Serikali kupitia Tume ya Madini imeendelea kusisitiza utekelezaji wa sheria na kanuni katika sekta ya madini, ikiwataka wamiliki wa leseni kuhakikisha shughuli za uchimbaji zinawanufaisha watanzania na kulinda maslahi ya taifa. Akizungumza jijini Dodoma kwenye kikao cha wamiliki wa leseni, Kamishna wa Tume ya Madini, Mhandisi Theonestina Mwasha, amesema kipaumbele cha Serikali ni kuwawezesha wamiliki wa leseni wazawa huku ikiweka msisitizo kwa wawekezaji wa kigeni kufuata taratibu zote za uwekezaji kabla ya kuanza shughuli zao. Amesema ni lazima kwa mwekezaji wa kigeni kupata idhini kupitia Afisa Madini wa eneo husika kabla ya kuanza shughuli yoyote, sambamba na kuwa na utaalam maalum unaohitajika katika sekta hiyo. “Ni wajibu wa mmiliki wa leseni kulinda utu na maslahi ya watanzania katika maeneo ya uchimbaji. Ni aibu kuona Mtanzania anadhulumiwa katika leseni inayomilikiwa na Mtanzania mwenyewe. Kanuni zipo, zifuateni,” amesema Mhandisi Mwasha. Ameongeza kuwa w...