Skip to main content

Posts

Showing posts from April 11, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Zoezi la Kubadilisha Tahasusi na Kozi za Vyuo Lafunguliwa Rasmi

Na OWM - TAMISEMI, Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa, zoezi la kubadilisha tahasusi na kozi za vyuo vya kati kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2025 limeanza rasmi leo Aprili 11, 2026 na litahitimishwa  Mei 10, 2026.  Prof. Shemdoe amesema hayo leo Aprili 11, 2026 jijini Dodoma, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2025 kufanya mabadiliko ya Tahasusi za kidato cha tano na kozi za vyuo vya kati kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa kielektroniki wa uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na Vyuo mwaka 2026. “Ninawahimiza wanafunzi, wazazi na walezi kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya mabadiliko ya tahasusi au kozi,” amesisitiza Prof. Shemdoe. Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amewataka wahitimu kufanya marekebisho ya machaguo ya tahasusi na kozi kulingana na ufaulu wao, kwa kuingia kwenye Mfumo wa Uchaguzi wa Wanafun...

Zaidi ya Watalii Tisini Watembelea Hifadhi ya Taifa Mkomazi Kufuatia Ufunguzi wa Tamasha la Same Utalii Festival

Na. Calvin Katera - Same Zaidi ya Watalii 90 wametembela Hifadhi ya Taifa Mkomazi kuvinjari na kufurahia utalii wa ndani leo Aprili 11, 2026 kufuatia ufunguzi wa tamasha la utalii lijulikanalo kama Same Utalii Festival msimu wa Tatu katika viwanja vya stendi wilayani Same, Mkoani Kilimanjaro. Watalii hao walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hifadhi ikiwemo Mbula, Kisima na Njiro na kujionea wanyamapori aina ya faru weusi, kivutio kinachowavutia wazawa na wageni lukuki toka nje na ndani ya mipaka ya Same kushuhudia ikolojia ya wanyama hao. Akizindua rasmi tamasha hilo Waziri Mkuu (Mst.) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyelitumikia Taifa kwa kipindi cha Awamu ya Nne kati ya mwaka 1990 hadi 1994 Mhe. John Malecela alisema kuwa matamasha haya ni kichocheo kikubwa cha utalii na hifadhi pia zina nafasi kubwa ya kuibua mazao mapya ya utalii yatakayochagiza kuongeza idadi ya watalii  kutembelea hii kwa kuwa na vionyo tofauti. Aidha, Mhe. Malecela aliongeza kuwa utalii wet...

Waziri Nyansaho Achangisha Zaidi ya Milioni 640 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Kanisa

 Na Mwandishi Wetu, Tarime  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Ryimo Nyansaho, ameongoza harambee iliyokusanya shilingi milioni 641 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Jimbo jipya la North Mara Field. Waziri Nyansaho ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na ujumbe wake, wamechangia shilingi miloni 82 katika changisho hilo ambalo limefanyika leo Aprili 11, 2026 katika Kanisa la SDA Kibumaye, nje kidogo ya mji wa Tarime. Washiriki kutoka makanisa yote ya SDA ya jimbo hilo na wadau wengine wamechangia shilingi milioni 559. “Inaonekana nimekuja na mibaraka, kwa jinsi matoleo ya leo yalivyokwenda, ujenzi wa jengo la ofisi ya SDA North Mara Field utakamilika na jengo litasimama,” Waziri Nyansaho amesema katika sehemu ya hotuba yake fupi. Waziri Nyansaho amefuatana na viongozi mbalimbali, wakiwemo mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mara, Chri...

Makamu wa Rais Afungua Kongamano la Vijana Katika Kumbukizi ya Kuzaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.K Nyerere

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa vijana kusimama imara na kulinda umoja, kujenga uadilifu, kutumia elimu na ubunifu katika kukuza maendeleo ya nchi ili kuweza kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Kongamano la Vijana katika Kumbukizi ya Miaka 104 ya Kuzaliwaa Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, lililofanyika Ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma, leo tarehe 11 Aprili 2026. Amesema ni muhimu kwa vijana kutambua wajibu wa msingi wa kizazi hiki, kwa kuhakakikisha wanafanya kila jitihada kuimarisha misingi ya kujitegemea kiuchumi, kiakili na kimaamuzi ili kuijenga nchi. Makamu wa Rais amesema Hayati Baba wa Taifa alikuwa kiongozi aliyeunganisha Taifa na kutoa mchango mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika. Amesema Taifa la Tanzania lilipata bahati ya pekee kuwa na Hayati Mwl. Nyerere kwa kuwa alichukia rushwa, ubadhirifu na matu...

Prof. Shemdoe Aelekeza Wafanyabiashara Soko la Simu 2000 Kuendelea na Biashara

 Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameelekeza hatua za haraka zichukuliwe kuwarejesha wafanyabiashara wa Soko la Mawasiliano (Simu 2000) ili kuendelea na shughuli za biashara katika soko hilo ambalo lilipata ajali ya moto iliyoteketeza soko hilo Aprili 04, 2026. Prof. Shemdoe ametoa maelekezo hayo Aprili 10, 2026 alipolitembelea soko hilo na kuridhishwa na utekelezaji wa Maelekezo ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoyatoa Aprili 6, 2026, alipofika kukagua madhara ya tukio hilo la moto na kuelekeza soko hilo kusafishwa mara moja ili kuruhusu wafanyabiashara kuanza taratibu za kurejesha shughuli zao. “Nimeridhishwa na utekelezaji wa maelekezo aliyotupatia Mhe. Rais na Mhe. Waziri Mkuu, hivyo naelekeza haraka iwezekanavyo wafanyabiashara warejeshwe kuendelea na shughuli zao lakini wasijenge vibanda na badala yake waweke meza pamoja na miamvuli ili kujikinga dhidi ya jua na mvua,” amesisitiza Prof. S...

Rais Samia Atunukiwa Shahada ya Uzamivu Nchini Nigeria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwa njia ya mtandao na Chuo Kikuu cha Jimbo la Nasarawa, Keffi nchini Nigeria ambacho kimemtunuku Shahada ya Uzamivu ya Heshima , tarehe 11 Aprili, 2026 Ikulu, Dodoma.