Skip to main content

Posts

Showing posts from October 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAWEKEZAJI WATAKIWA KUCHANGIA FURSA ZILIZOPO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUHEZA.

 Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina ardhi kubwa na yenye retuba ya kutossha inayofaa kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuifanya wilaya hiyo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji katika kilimo na biashara. Hayo yameelezea na Mkurungenzi wa Halmashauri ya hiyo Naima Chondo kufuatia ushindi wa kitaifa  waliopata katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya usagara jijini Tanga. Hivyo basi Chondo amewakaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo katika halmashauri hiyo ikiwemo katika sekta ya Kilimo kwa kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kisasa na kujenga viwanda vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza thamani na kipato kwa wakulima. Chondo ameendelea kusema kuwa maandalizi mazuri na juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kushiriki maonesho ya siku ya chakula duniania pamoja na  kujifunza teknolojia mpya za kilimo na kupata fursa ya kuonesha ubora wa mazao wanayozalisha na mnyororo mzima wa thamani...