Skip to main content

Posts

Showing posts from October 14, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Nchimbi Aendelea Kuchanja Mbuga Akisaka Kura za Ccm Singida Vijijini

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi  ameendelea kuchanja mbuga kwa ajili ya kuomba kura za mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan. Leo Oktoba 14,2029 Dk.Nchimbi anafikia mkoa wa 23, akifanya mkutano mkubwa wa kampeni katika Uwanja wa CCM uliopo Kata ya Ilongero, jimbo la Ilongero katika Wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida. Akiwa katika mkutano huo Dkt.Nchimbi ameendelea kumuombea kura Mgombea Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili ashinde kwa kishindo, kuomba kura za wabunge na madiwani. Mbali ya kuomba kura za wagombea wa CCM, pia akiwa katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jimbo hilo pia ametumia nafasi hiyo kunadi sera na Ilani ya CCM ya 2025-2030. Wakati huo huo Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ilongero, Ndugu Haidary Gulamali na Madiwani.

Dkt Tulia Ashiriki Ibada ya Muombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere

 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea Ubunge Jimbo la Uyole kupitia CCM , Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Oktoba, 2025 ameshiriki katika ibada maalum ya kumuombea hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere katika siku ya kumbukumbu ya Mwl. Nyerere. Ibada hiyo imefanyika Mkoani Mbeya katika kanisa la Hija Parokia ya Mwanjelwa ambapo mgeni rasmi katika Ibada hiyo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na kuongozwa na Askofu mkuu Gervas Nyaisonga wa jimbo kuu la Mbeya.

Dkt. Biteko Amshukuru Mama Samia Kwa Maendeleo Bukombe

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Doto Mashaka Biteko amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na maelekezo yaliyowezesha utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wilayani, mkoani na Taifa kwa ujumla. Dkt. Doto Biteko amesema hayo mbele ya Mgombea Urais kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika Wilaya ya Bukombe, ikiwa ni sehemu ya Kampeni zake Mkoani Geita Oktoba 12, 2025.  “ Mgombea umetufundisha mengi, kupitia kauli mbiu yako ya kazi na utu tunasonga mbele, unatenda zaidi na kusema kidogo. wewe unazungumza matatizo ya watu na maisha yao wakati wote, Utu kwako ni kipaumbele na Kazi kwako ni msingi wa maendeleo” amesema Dkt. Biteko Ametaja miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika  kipindi cha miaka mitano iliyopita ikiwemo Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, Daraja la JPM, Barabara ...

MIAKA 26 YA KUMBUKIZI YA KIFO CHA BABA WA TAIFA: Rais Dkt. Samia anavyomuenzi kwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji kodi

  Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Oktoba 14, 1999, ilikuwa ni siku ya simanzi kubwa nchini kwetu Tanzania baada ya kutangazwa kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Leo, Jumanne ya Oktoba 14, 2025, imetimia miaka 26 tangu kutokea kifo chake. Kimsingi, Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa ni hazina kubwa kwa Taifa letu, hazina ambayo hakuna maneno wala kitabu kitakachotosha kuelezea maisha yake. Moja ya dhamira ya Mwalimu Nyerere tangu akiwa Rais na hata baada ya kustaafu, alitamani kuona Watanzania wakiishi maisha ya ustawi, mbali na umaskini. Aliweka mkazo mkubwa kwa serikali kufanya kila liwezekanalo, lililo katika uwezo wake kuhakikisha tatizo la umaskini linatatuliwa. Aliweka mkazo katika ukusanyaji kodi ili fedha hizo zitumike katika kutekeleza mipango mbalimbali ya serikali kwa ajili ya ustawi wa wananchi.  Alitaka kila Mtanzania mwenye sifa za kulipa kodi alipe. Hakutaka serikali ikusanye kodi kwa uonevu wala mabavu. Alitaka raia wote wa ngazi za chini, kati na j...

Makamu wa Rais Ashiriki Ibada ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

*ASISITIZA WANANCHI KUENDELEA KUMUOMBEA NA KUENDELEZA MEMA ALIYOFANYA* Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasihi Watanzania kuendelea kumuombea Baba wa Taifa hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere ili aendelee kupumzika kwa amani na awe mmoja wa Watakatifu. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati alipoungana na Viongozi, Waumini pamoja na Wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya. Amesema ni vema kila mmoja wetu hususani viongozi kufuata mfano mwema wa Baba wa Taifa ambaye alikuwa mwaminifu kwa Taifa la Tanzania na kulitakia mema wakati wote. Aidha kwa niaba ya Serikali, Makamu wa Rais amewashukuru waumini na wananchi wa Mkoa wa Mbeya kwa kujitokeza kumuombea Baba wa Taifa wakati wa kumbukizi ya miaka 26 tangu kifo chake. Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu G...

Waziri Mkuu Ameshiriki Katika Ibada ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere Mkoani Mbeya

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Oktoba 14, 2025 ameshiriki katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya.  Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango pia ameshiriki katika ibada hiyo. Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga.