Skip to main content

Posts

Showing posts from January 20, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri wa Ulinzi na Jkt afanya Ziara Makao Makuu ya JWTZ

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Rhimo Simeon Nyansaho, Leo tarehe 20 amefanya ziara katika Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ( MMUT), Kikombo pamoja na Hospitali Kuu ya Rufaa ya Jeshi Msalato, Jijini Dodoma.  Mhe. Nyansaho alianza kwa kutembelea MMUT ambapo alipokelewa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman. Akiwa MMUT, Waziri Nyansaho alitembelea ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo na kupokea taarifa ya maendeleo ya mradi huo wa ujenzi ulioanza rasmi mwaka 2020. Baada ya kumaliza ziara yake MMUT, Waziri Nyansaho alielekea katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Kijeshi iliyoko Msalato ambapo pia alipata wasaa wa kuona ni kwa namna gani mradi huo umefikia katika hatua nzuri. Mhe. Waziri Nyansaho, amefurahishwa na ujenzi wa Hospitali hiyo ya Jeshi na amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Hospitali yenye uwezo wa kutoa huduma nzuri na za kiwango cha juu za matibabu hasa katika Jiji la Dodoma na hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutahakikisha upatikanaj...

Jkt Yaita Vijana Kujiunga Mafunzo ya Kujitolea

Mkuu wa Jeshi ya Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametangaza nafasi kwa vijana kwa ajili ya kushiriki mafunzo ya kujitolea yanayotarajiwa kufanyika Februari mwaka huu.  Wito huo umetolewa na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye amesema utaratibu wa kujiunga na mafunzo hayo ni vijana kuomba na kuchaguliwa katika ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambao wanawaratibu vijana hao maeneo yao. ”Usaili wa vijana hao kujiunga na mafunzo hayo kwa kujitolea januari 26 mwaka huu katika mikoa yote bara na visiwani kabla ya kuanza kuripoti makambani februari 27 hadi machi 4 mwaka huu,” amesema Brigedia Jenerali Hassan Mabena Mkuu Tawi la Utawala JKT. Aidha Mabena amesema vijana wenye taaluma kama diploma in information technology, diploma in businessinformation systems na vijana wenye vipaji vya michezo wanahitajika katika mafunzo hayo. Brigedia Jenerali Mabena pia amesema JKT inawataarifu vijana hao watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajirawala kuhusika...

Shina La Makunduchi Mmedhihirisha Kwa Vitendo Kuwa Maendeleo Hayana Chama-.Dkt.Migiro

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dkt.Asha Rose Migiro,amezindua Shina la wakereketwa wa CCM Makunduchi lililopo Mtaa wa Uhuru Wilaya ya Dodoma Mjini,na kuwapongeza kwa kutumia shina hilo kama sehemu ya kujiongezea kipato bila ya kujali itikadi zao. Akizungumza na wajumbe hao Januari 20,2026,kabla ya kuzungumza na Mabalozi wa Mashina wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Migiro,amesema hatua hiyo inaonyesha umoja na kudhihirisha kuwa kuna shughuli lazima ziwalete pamoja. "Shina hili niwapongeze sana,mmetuthibitishia kuwa shughuli za kiuchumi hazina itikadi lakini katika kushirikiana hivi tunawavuta na kuwaleta pamoja watanzania,wanajamii wenzetu bila ya kujali itikadi kwa sababu maendeleo ya nchi hayana itikadi,umoja wa nchi hauna itikadi na umadhubuti wa Taifa pia hauna itikadi,"amesema. "Ni jukumu letu kuhakikisha tushiriakana na jamii yote maana kura tulizopigiwa zimepigwa na wana CCM na wasio wana CCM.Na Rais wetu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama chetu ni Rais wa wote hivyo na si...

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yakamilisha ujenzi jengo jipya

  ………Shule ya sekondari ya amali Mwambasha nayo yakamilika.  ……….Halmashauri ya Wilaya Shinyanga yampongeza Rais Samia kwa bilioni tatu Na  Mwandishi Wetu HALMASHAURI ya Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga imesema kukamilika kwa jengo lake lililogharimu shilingi bilioni tatu kumeboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa halmashari hiyo kwa kiwango kikubwa. Halmashauri hiyo imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kufanikisha kukamilika kwa ujenzi wa jengo lake pamoja na shule ya sekondari ya Amali Mwambasha iliyoko kwenye halmashauri hiyo. Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Kalekwa Kasanga wakati akizungumzia mafanikio ya ujenzi wa jengo hilo na namna ulivyosaidia kuboresha kazi zake za kila siku. Alisema mwaka 2021 walianza  kuipokea fedha kutoka serikalini kujenga jengo la halmashauri hiyo ambalo limeshakamilika kuanza  kutumika rasmi kuanzia tarehe  16.4.2025. “Kwa dhati kabisa tunamshukuru Rais wetu Sami...

Katambi Akutana na Uongozi wa Kampuni ya Condor Kutoka Brazil

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi akizungumza na Wawakilishi wa Kampuni ya Condor, kutoka nchini Brazil, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusiana na kudhibiti uhalifu, ambapo nchi mbili hizo, Tanzania na Brazil walibadilishana uzoefu  katika masuala ya udhibiti wa uhalifu.                                                                                                                                                              Mazungumzo hayo  yamehudhuriwa na Meneja Mauzo ya Kimataifa kutoka Kampuni ya Condor,Renani Annize, Mkuu wa Mauzo ya Kimataifa, Ka...

Dkt. Mwigulu Afanya Mazungumzo na Mhandisi Masauni

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 20,2026 amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira, Mhandisi Hamadi Masauni, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Viongozi wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Naibu Waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais -  Muungano na Mazingira, Dkt. Festo Dugange na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  - Muungano na Mazingira, Dkt. Richard Muyungi.

Dkt. Mwigulu Akutana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 20,2026 amefanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Emmanuel Tutuba, ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.