Skip to main content

Posts

Showing posts from December 18, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tamasha la Kwanza la Kihistoria na Utamaduni Mji Mkongwe wa Kigoma ujiji Lafana Sana

Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wameaswa Kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mkoani humo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Gombe ambayo ina wanyama aina ya sokwe mtu pamoja na maporomoko mazuri ya maji. Wito huo umetolewa na Sheikh Hassan Kabeke wakati wa Tamasha la kwanza la kihistoria na Utamaduni wa Mji Mkongwe wa Kigoma ujiji lililolenga  kutangaza mji huo mkongwe pamoja na vivutio kadhaa vya utalii vilivyopo mkoani Kigoma.  Sheikh Kabeke ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tamasha hilo amesema kuwa ni Jukumu la kila mwana Kigoma wakiwemo wa Ujiji,Kasulu,Kibondo,Kakonko,, Buhigwe,Ilagala,Mwamgongo, Mwanga,Bangwe,Gundu,Mwandiga, Kibirizi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kwenye mji huo pamoja na Mkoa Kigoma kwa Ujumla.  " Mji wa Kigoma Ujiji una zaidi ya miaka 300 na Majengo ya ibada na Misikiti yenye zaidi ya karne tano likiwemo Kanisa lenye umri wa miaka Mia Moja sanjari na visima vilivyo chimbwa wakati wa Utawala wa Waingereza"alisema Sheikh Kabeke kwa nyakati tofauti wakati ak...

Kamishna wa TRA Tanzania, Bw. Yusuf Juma Mwenda, afanya Mazungumzo na RC Sendiga

Leo tarehe 18 Desemba 2024, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, ameripoti katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, ambapo amepokelewa rasmi na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga.   Katika ziara hii ya siku moja, Bw. Mwenda ameeleza kuwa lengo ni kukutana na wafanyabiashara wa mkoa wa Manyara, kupitia hali ya ulipaji kodi, pamoja na kujadili fursa za ushiriki wa TRA katika miradi ya maendeleo ya kijamii (CSR).  Aidha, Bw. Mwenda amepongeza juhudi za Mhe. Queen Cuthbert Sendiga kwa kuongoza mkoa ambao umekuwa na historia nzuri ya ulipaji wa kodi kwa mwaka 2024. Hili limekuwa chachu ya maendeleo ya mkoa wetu na taifa kwa ujumla.   RC Sendiga amemuhakikishia Kamishna kuwa Mkoa utaendelea kuweka mazingira mazuri kwa TRA ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo sambamba na kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanapata elimu ya kodi na kuweka mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo endelevu ya mkoa na wananchi wake.

Bashungwa atoa Maagizo Kwa IGP Wambura Kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka

📌 Kuimarisha ulinzi, doria na ukaguzi vyombo vya moto usiku na mchana. 📌  Kuondoa vizuizi na vituo vya ukaguzi maeneo hatarishi barabarani. 📌 Kufanya Operesheni maalum nchi nzima kupambana na wahujumu miundombinu ya Serikali 📌 Awahakikishia Watanzania nchi ipo salama. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa  amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura kulisimamia Jeshi la hilo kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani, kuimarisha doria (highway patrol) usiku na mchana pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye Nyumba za Ibada katika kipindi cha sikukuu za Christmass na Mwaka Mpya. Bashungwa ametoa maagizo hayo, leo tarehe 18 Disemba, 2024 wakati akitoa taarifa kwa Umma kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka ambapo amewahakikishia wananchi na Watanzania wote kuwa nchi  iko salama. “Hatuko tayari kuacha tabia za kizembe ziendelee kupoteza maisha ya watu, na wengine kupata ulemavu, huku Sheria za kudhibiti uzembe zikiwa zipo. Tutachukua hatua ...

Viongozi wa Dini Kagera Walaani Wanaotafuta Utajiri Kwa Ushirikina

 Na Angela Sebastian ;Bukoba VIONGOZI wa madhehebu yote mkoani Kagera wamewataka wananchi wa mkoa huo kutambua kuwa hakuna utajiri na mafanikio yanayopatikana kupitia njia za kishirikiana au kukata viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi. Pia wamekemea baadhi ya wananchi wa mkoa huo ambao uendekeza fitina mioyoni mwao maarufu kama kamunobele ambayo imekuwa jinamizi linaloendelea kuwatesa baadhi ya wananchi mkoani humo na kusababisha kutojifanyia maendeleo na kujiingizia kipato. Viongozi hao walitoa kauli hizo jana wakati wa dua na maombezi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan,wasaidizi wake,Taifa mkuu wa mkoa na wananchi kwa ujumla ambapo ilifanyika katika uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba. Makamu askofu wa kanisa katoriki la Bukoba ambaye pia ni baba paroko wa parokia ya Bukoba padre Samueli Muchunguzi amesema katika kitabu cha Zaburi 127 sura ya kwanza inasema bwana asipojenga nyumba wajengaji wengine wanafanya kazi bure na asipolinda...