Skip to main content

Posts

Showing posts from March 11, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Aweka Jiwe la Msingi Mradi Wa Maji Makoremo-mgongoro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Machi 12, 2025 ameweka jiwe la msingi la Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa Majisafi ya Ziwa Victoria kutoka Makomero - Mgongoro, uliopo kijiji cha Mwamayoka, Igunga mkoani Tabora ambao umegharimu shilingi milioni 840.8 Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo, ambao unatarajia kuhudumia wananchi 5,402, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaendelea kusimamia utoaji wa huduma za maji safi na salama nchini ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji inawafikia wananchi kwa asilimia 100. “Ndugu zangu wananchi, mradi huu ni matokeo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, kuweni na uhakika kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni akiongozi   anayewajali, anawapenda na anasikiliza changamoto zenu, endeleeni kutekeleza majukumu yenu ipasavyo kwasababu tunaye kiongozi madhubiti” Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza RUWASA kuongeza na kusogeza vituo vya kuchotea maji karibu na wananchi “RUWASA hakikisheni miradi hii inatoa maji w...

Rais Samia Aagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa Kupambana na Migogoro ya Ardhi Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa serikali za  mitaa kote nchini kujiepusha kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao, akiwataka kuwa sehemu ya masuluhisho ya migogoro hiyo. Wakati wa Mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Alat katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma leo Machi 11, 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo ameitaja migogoro ya ardhi kama donda sugu kwenye jamii, akiitaja kama chanzo cha uhasa na mauaji kwenye ngazi ya jamii. Katika hatua nyingine Rais Samia amewataka watendaji wa Serikali za mitaa kuendelea kusimamia watumishi na watendaji wa mamlaka zao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuwapokea na kuwasikiliza kwa busara sambamba na kuimarisha mifumo ya ushughulikiaji wa kero za wananchi kwa wakati. Rais Samia pia katika hotuba yake amesisitiza kuhusu kuainisha mipango ya ngazi ya Halmashauri na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa pamo...