Skip to main content

Posts

Showing posts from September 24, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kabla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79), Jijini New York, Marekani Septemba 24, 2024. Wengine kwenye picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed na kushoto ni Afisa Mkuu wa Masuala ya Umoja wa Mataifa Courtenay Rattray.  UN Photo

Tarura kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Mhadisi Victor Seff amesema wakala huo mikoa mbalimbali inaendelea na kazi za matengenezo kwenye barabara zinazounganisha miji na vijiji nchini.  Matengenezo ya miundombinu yapo kwenye hatua mbalimbali kwa mwaka huu wa fedha ambapo moja ya maeneo yenye ukarabati na matengenezo alilotembelea hivi karibuni ni Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida. Mhandisi Self amesema Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Mkalama mkoani Singida inaendelea na ujenzi pamoja na matengenezo ya barabara na madaraja ili kuhakikisha wananchi wanazifikia huduma za kijamii na kiuchumi kwa urahisi. Naye Meneja wa TARURA katika Wilaya hiyo, Mhandisi Rahabu Thomas amesema kuwa hadi sasa miradi mbalimbali imekamilika ikiwemo ujenzi wa barabara ya Gengerankuru - Moma yenye urefu wa mita 640 kwa kiwango cha lami pamoja na kuweka taa. Mhandisi Rahabu amesema kuwa barabara hiyo imewasaidia wananchi hasa kipindi wanapohitaji kupata hud...

Watumishi Tume ya Madini Wafundwa

Na Dawati la Habari Tume ya Madini Watumishi wa Tume ya Madini wametakiwa kufanya kazi kwa umoja, weledi na kuheshimiana ili kufikia lengo la makusanyo ya maduhuli la kukusanya shilingi Trilioni Moja katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025. Hayo yamesemwa leo Septemba 24, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba katika kikao maalum na watumishi hao jijini Dodoma chenye lengo la kuweka mikakati ya kuboresha Sekta ya Madini. Akielezea hali ya makusanyo ya maduhuli tangu kuanza kwa mwaka mpya wa fedha, amesema kuwa katika kipindi cha mwezi wa saba na wa nane fedha iliyokusanywa haijawahi kukusanywa tangu kuanzishwa kwa Wizara ya Madini na kuongeza kuwa matarajio ya mwezi huu wa tisa mambo yatakuwa mazuri zaidi. “Tunapaswa kukusanya shilingi Bilioni 84 kila mwezi, kwa miezi miwili tumekusanya wastani wa shilingi Bilioni 163.8, bei ya dhahabu kwenye soko la dunia imepanda, lakini haina maana kama hakuna udhibiti wa utoroshaji wa dhahabu,”amesema Mhandisi ...

Rais Samia ataka wawekezaji sekta ya kilimo kurithisha wakulima ujuzi na teknolojia

  Na Dawati la Habari NIRC Ruvuma Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema mafanikio yaliyopo sekta ya kilimo hayatokei kwa bahati mbaya bali ni kutokana na uwekezaji mkubwa unaofaywa na serikali kwenye sekta hiyo   Samia amesema kuwa Uwekezaji huo umewezesha kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la kahawa kwenye shamba la AVIV  kutoka tani 65 hadi kufikia tani 85 katika kipindi cha mitatu iliyopita,ongezeko hilo limeliingizia Taifa dola za kimarekani milioni 250. Ameitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha wawekezaji waliopo mbali wanayoyafanya katika kurudisha kwa jamii pia wahusike katika kurithisha ujuzi na teknolojia hususani za Umwagiliaji zinazotumika katika sekta hiyo ili kuwezesha wananchi kuwa na kilimo chenye tija kwa maslahi ya kizazi cha sasa na  vijavyo.   Rais Samia amesema hayo alipotembelea shamba la uzalishaji wa Kahawa la AVIV mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala 28 ya kuhifadhi mazao ya nafaka yaliyo chini ya Wakala wa hifadhi ya Cha...

Waziri Mkuu aungana na wakuu wa nchi na serikali ufunguzi wa mkutano wa unga 79

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 24, 2024 ameungana na wakuu wa nchi na Serikali katika ufunguzi wa Mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA79) uliofanyika makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani. Mkutano huo ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ambapo Waziri Mkuu ameshiriki kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mheshimiwa Majaliwa anatarajiwa kutoa tamko la  Serikali kwenye mkutano huo Septemba 27, 2024 akiwa ni Waziri Mkuu wa Pili kuhutubia baraza la Umoja wa Mataifa. Septemba 27, 2010 aliyekuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alihutubia baraza la 65 (UNGA65). Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), pamoja na Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Hussein Katanga.

Mkutano mkuu wa nishati barani afrika waikubali Tanzania sekta ya nishati

*Nia ni kukusanya dola za Marekani bilioni 190 za kusambaza umeme *Rais wa Liberia aomba umeme uwe kipaumbele maishani TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa masuala ya nishati barani Afrika utakaotafuta namna ya kukusanya dola za Marekani bilioni 190 ili zitumike kufikisha umeme kwa wananchi milioni 300 barani humo ifikapo mwaka 2030. Hatua hiyo inatokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya sita kupeleka umeme vijijini na vitongojini kwa kasi hali ambayo imezivutia taasisi za Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kuamua kufanya mkutano huo mkubwa ifikapo Januari, 2025. “Wameridhishwa na utendaji kwenye sekta ya nishati, wameridhishwa na mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme mpaka vijijini, siyo tu vijijini lakini mpaka kwenye kila nyumba. Wameamua kuitisha mkutano mkubwa barani Afrika ambao utawakutanisha wadau mbalimbali, taasisi za Kimataifa na taasisi zinazotoa mikopo kwa wajasiriamali na makampuni ili waweze kuwekeza kwenye umeme.”  Hayo yalisemwa jana (J...

Wanafunzi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya chief Zulu wamchangia Rais Samia 1,800

Yeye awachangia Shilingi Milioni 100 ya Ujenzi wa Bwalo. -Awapatia Ng'ombe 2, Mchele kilo 500 na mafuta. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan amechangiwa kiasi Cha Shilingi 1,800 na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu ya Mkoani Ruvuma. Rais Dkt, Samia amechangiwa kiasi hicho Cha fedha wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Shule hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya Shilingi Milioni 600 leo September 24,2024.

Rc Mtambi asema Mbunge Ghati anatisha katika utekelezaji wa ilani ya ccm

Na Shomari Binda-Musoma MKUU wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amepongeza kazi nzuri inayofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete kuwatumikia wanawake na wananchi. Pongezi hizo amezitoa leo septemba 24 baada ya kutembelewa ofisini kwake na mbunge huyo na kufanya nae mazungumzo. Amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na mbunge Ghati Chomete akiwa bungeni na kwenye ziara zake mkoani. Mtambi amesema katika vikao vya bunge amekuwa akichangia masuala mbalimbali yenye malengo ya kusaidia wananchi na kupatiwa ufumbuzi. Amesema licha ya michango yake bungeni lakini amekuwa akifanya ziara kwenye mkoa mzima wa Mara kwa kuzungumza na kuchangia masuala ya kijamii. " Nikupongeze na kukushukuru sana mheshimiwa mbunge kwa kazi nzuri unayoifanya katika kuwasemea wananchi ukiwa bungeni. " Mchango wako tunauona na kuuthamini ukiwa bungeni na hata kwenye ziara zako unazokuwa ukizifanya kukutana na wananchi hongera sana kwa kazi nzuri",amesema. Kwa upande wake mbun...

Rais Samia afungua shule ya mchepuo wa kiingereza songea

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, Songea mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu, Teofilo Mbunda kuhusu matumizi ya Computer shuleni hapo, Songea mkoani Ruvuma tarehe 24 Septemba, 2024.