Skip to main content

Posts

Showing posts from April 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi kuelekea Uingereza kushiriki mkutano wa CTIS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ataondoka nchini leo kuelekea Jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili 2025 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025). Katika ziara hiyo Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza na Taasisi zake, atakutana na  Diaspora wa Tanzania waliopo nchini Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair , Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi wa Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi wa bluu. Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa  uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu, viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi. Vilevile Rais Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa k...

Tuzo za Malkia wa Nguvu ni Chachu ya Maendeleo Kwa Wanawake ja Jamii - Dkt. Biteko

📌 Clouds Media yapewa heko miaka tisa ya Malkia wa Nguvu 📌 Clouds yaunga mkono jitihada za Rais Samia za kuwezesha wanawake kiuchumi 📌 Wanawake wasisitizwa kutumia Nishati Safi kulinda afya zao Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Jukwaa la Malkia wa Nguvu la Clouds Media lilioanzishwa mwaka 2016 limeendelea kutimiza lengo lake la kuhamasisha na kuunga mkono wanawake katika nyanja za ujasiriamali, maendeleo ya kiuchumi na masuala mengine mbalimbambali ya kijamii kwa kipindi cha miaka tisa sasa.   Akizungumza Aprili 4, 2025 jijini Dar es salaam wakati aliposhiriki katika sherehe za Tuzo za Malkia wa Nguvu kwa mwaka 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema  jukwaa  hilo pia hutambua, huthamini na husherehekea jitihada na michango ya wanawake waliothubutu na kufanikisha maendeleo katika nyanja mbalimbali za kijamii, uchumi na uongozi. “ Tangu kuanzishwa kwake, hadi sasa, jukwaa hili limekuwa ni chachu kubwa ya maendele...

Tra Yavunja Rekodi ya Makusanyo Kwa Miezi 9 Mfululizo yakusanya Trilioni 24.05

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya Sh. Trilioni 7.53 katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25, sawa na ufanisi wa asilimia 101.32 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 7.43. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda imeeleza kuwa ufanisi wa makusanyo ya Robo ya Tatu ya mwaka 2024/2025 ni sawa na ukuaji wa asilimia 13.47 ukilinganisha na kiasi cha Shilingi Trilioni 6.63 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2023/24.  Taarifa hiyo inaeleza kuwa ​makusanyo yaliyokusanywa katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 yanapelekea TRA kuweza kuweka rekodi ya kipekee katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kufikia na kuvuka lengo la makusanyo kwa miezi 9 mfululizo katika mwaka wa fedha 2024/2025. Taarifa ya Bw. Mwenda inafafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Julai – Machi, mwaka wa fedha 2024/25, TRA imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 24.05 sawa na ufanisi wa asilimia 103.62% ya lengo la k...

Meneja wa Shirika la Ndege na Vituko Hivi....

MOJAWAPO ya makosa yaliyowahi kutendwa na mashirika ya ndege barani Afrika, ni tukio la mwaka 1988 ambapo Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Uganda aliachwa na ndege ya abiria na akaamuru irejee uwanjani kumchukua. Meneja huyo alichelewa kufika uwanjani hapo tayari kusafiri kwa ndege hiyo, na ndipo aliwaamuru waongoza ndege kuwaambia marubani kurejesha ndege hiyo aina ya Boeing 747 - Jumbo Jet. Ni katika utawala huu wa Rais Yoweri Museveni ambapo meneja huyo alivurugwa na kutoa amri hiyo ya ajabu, ambayo pia ilimharibia kazi yake siku hiyo hiyo. Wakati huo shirika la ndege la Uganda lilikuwa limekodisha ndege za shirika la ndege la Uholanzi, KLM, kwa ajili ya safari za nje ya Uganda. Katika tukio hilo, ndege hiyo ikiwa na abiria iliondoka uwanja wa ndege wa Entebbe saa 2 asubuhi kwenda Bombay nchini India. Ndege ikiwa inaondoka uwanjani hapo ndipo maneja huyo ambaye alitakiwa asafiri nayo kwenda kwenye mkutano nchini India, aliwasili uwanjani hapo akiwa amechelewa na kuachwa. Meneja hu...

Balozi Dkt. Nchimbi Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu Jukwaa la Wahariri Tanzania

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa mgeni rasmi, leo Ijumaa tarehe 4 Aprili, amefungua Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), unaokutana mjini Songea kwa siku mbili, hadi tarehe 5 Aprili, mwaka huu, kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa jukwaa hilo.