Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), *CPA Amos Makalla* amesema uchaguzi mkuu mwaka wa huu 2025 utafanyika kwa mujibu wa katiba na sheria kwani mabadiliko yameshafanyika, hivyo hakuna atakayezuia uchaguzi. CPA. Makalla ameeleza hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya Shina, Tawi, Kata na Wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo. “Uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa katiba kwa mujibu wa sheria, nimeona kwenye magroup yao wanaambiana wachangiane tone kwa tone tuchangiane tuende kwenye nguvu ya umma kuzuia uchaguzi, hela zitaliwa kwa sabaau uchaguzi utafanyika,” Amesema Makalla. Akizungumza na Viongozi hao CPA. Makalla ameongeza kuwa kama watabaki na msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi ni dhahiri baada ya uchaguzi mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakitokuwa na nguvu ya kuendelea kuwa chama kikuu cha upi...
Marato tv - Sauti ya Jamii