Skip to main content

Posts

Showing posts from February 8, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

" Wasira"Tunaelewa Tatizo La Bajeti Tanroads Kukamilisha Barabara za Mkoa Wa Mara

Na Shomari Binda-Rorya MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Bara Stephine Wasira amesema wanaelewa tatizo la ki bajeti kukamilisha ujenzi wa barabara za mkoa wa Mara. Kauli hiyo ameitoa wilayani Rorya wakati wa ziara yake inayoendelea mkoani Mara baada ya kusikiliza maelezo ya meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS) mkoa wa Mara Vedastus Maribe. Amesema kazi ya CCM ni kuwasemea watu na suala la ukamilishwaji wa ujenzi wa barabara zikiwemo za Wilaya ya Rorya watafikisha taarifa Wizara ya Ujenzi ili zifanyiwe kazi. Wasira amesema mkoa wa Mara una barabara kubwa 4 ambazo zipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi katika kuunganisha mkoa wa Mara nazo zitafikishiwa taarifa. Amesema ipo barabara ya Mika-Utegi-Shirati-Kirongwe yenye urefu wa kilomita 56.8,Tarime-Serengeti-Sanzate-Serengeti na Musoma-Busekera ambazo zikikamilika zitafungua zaidi mkoa wa Mara kiuchumi. Wasira amesema TANROADS mkoa wa Mara inafanya kazi nzuri na msukumo wa kusaidiwa masuala ya bajeti ya miradi yao ndio i...

Rais Samia Ameleta Mabadiliko Makubwa Kimaendeleo Nchini,Ikiwemo na Tarime-wasira

 Tarime.  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan serikali imeleta mabadiliko makubwa nchini ikiwemo wilayani Tarime ambako imejenga madarasa bila ya kuwachangisha wananchi kama ambavyo ilikuwa ikifanyika awali. Wasira ameyasema hayo mjini Tarime leo Jumamosi Februari 8,2025 alipokuwa akizungumza na wanachama na wa chama hicho. Amesema chama chake kimedhamiria kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi kwa kuendelea kuwatoa katika hali duni na kuwajengea misingi ya maisha bora kwa kadiri inavyowezekana huku akiwaomba wananchi kuendela kukiamini na kukipa nafasi ya kuendelea kushika dola na kuwatumikia. “Tunaendelea kufanya mapinduzi ya maisha ya watu na ndiyo maana watu wa Tarime sasa ni watu tofauti na waliokuwepo miaka 60 iliyopita nawashangaa wanoasimama na kunasema hatujafanya kitu, tumefanya, tumesomesha watu wengi sana hata wanaosema hatujafanya chocho...

Balozi Dkt Nchimbi azungumza na Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Taifa

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akizungumza kwenye Kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Wazazi, Jumuiya ya CCM, ambacho alialikwa na kushiriki akiwa mgeni maalum, leo Jumamosi tarehe 8 Februari 2025, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Mwanamke Initiatives Foundation (Mif) Yagawa Ambulance 4 Na Viti 50 Kwa Wenye Ulemavu

Siku ya tarehe 27 Januari 2025, kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, *Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)* chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) iliandaa matembezi maalum ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.  MIF iliandaa matembezi katika Kiwanja cha Ofisi ya Sheha wa Shehia ya Kizimkazi Dimbani Kusini Unguja kwa lengo la kuwashajihisha wananchi kuimarisha Afya na kupambana na maradhi nyemelezi ambayo yamekuwa yakienea kwa kasi nchini.  Katika matembezi hayo, MIF ilishirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar Pamoja na Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) katika zoezi la uchangiaji wa damu na upimaji wa moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja Kizimkazi Dimbani ambapo maadhimisho hayo yalifanyika.  Aidha, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) na Mwenyekiti wa Taasisi ya MIF alisema kuwa Kauli Mbiu ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni "M...

Jk:Bukombe Yatekeleza Ilani Ya Ccm Kwa Kishindo

📌 Rais Samia aleta mapinduzi ya maendeleo Geita 📌 Rais Mstaafu Kikwete asema Watanzania wana deni kwa Rais Samia mwezi Oktoba  📌 Wanachama wa CCM waaswa kuzingatia maslahi ya Chama 📌 Dkt. Biteko apongezwa usimamizi wa miradi ya maendeleo Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameupongeza uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bukombe kwa Mkutano Mkuu Maalum wa kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Bukombe kwa mwaka 2020-2025. Rais Mstaafu Kikwete ametoa pongezi hizo leo Februari 8, 2025 wakati akihutubia katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliofanyika katika Kata ya Igulwa, Wilaya ya Bukombe, Mkoa wa Geita. “ Nawapongeza kwa kuandaa Mkutano huo kwa kuwa unakidhi takwa la katiba ya CCM kwa kuwa inawezesha kupima mlipotoka, mlipo na mnapokwenda. Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la 2022 katika Ibara ya 72 (1) inatambua kuwa Mkutano Mkuu ni kikao kikubwa cha Chama katika ...

Waziri Mavunde ampokea Rais wa Afrika Kusini Dar es salaam

 Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde (Mb.) amempokea Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa ambaye amewasili chini Tanzania kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Februari 8, 2025. Jumuiya zote mbili zinakutana kujadili kwa lengo la kupatia ufumbuzi hali ya ulinzi na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rais Samia ameomba Eac Na Sadc Kuchukua Hatua za Kumaliza Vita Nchini Congo