Skip to main content

Posts

Showing posts from September 18, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WANAMICHEZO ARDHI SPORTS WATAKIWA KUZINGATIA NIDHAMU, KUIPIGANIA WIZARA SHIMIWI

 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Salome Kessy, amewataka wanamichezo wanaoiwakilisha Wizara katika Michezo ya SHIMIWI 2026 mjini Moshi kuzingatia nidhamu, uwajibikaji na maadili ya Utumishi wa Umma, akisisitiza kuwa kila mmoja abebe taswira ya Wizara katika kipindi chote cha mashindano. Bi. Kessy ameyasema hayo Septemba 18, 2026 jijini Dodom akizungumza na wanamichezo watakaoshiriki michezo inayotarajiwa kufanyika mkoani Kikimanjaro kuanzia Septemba 20 hadi Oktoba 7, 2026. Ameongeza kuwa, mafanikio katika michezo hayawezi kutenganishwa na nidhamu, akiwataka wanamichezo kutunza utimamu wa miili yao, kuzingatia ushauri wa madaktari, kula vizuri na kupumzika kwa wakati badala ya kutumia muda wa mapumziko kuzurura.  Aidha, amewataka viongozi na walimu wa timu kuhakikisha kila mchezaji anatumika ipasavyo kulingana na uwezo wake, huku akisisitiza kuwa vitendo vya utovu wa nidhamu havitavumiliwa na hatua stahiki zichukuliwe kwa watakaokiuka ta...

MBUNGE AGNES ATOA ELIMU KWA WASAFIRISHAJI KUHUSU MIKOPO YA BODABODA NA BAJAJI

  Na Ghati Msamba, Musoma. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes, ametoa elimu kwa wasafirishaji wa bodaboda na bajaji kuhusu fursa za mikopo inayolenga kuwawezesha kupata vitendea kazi na kujikwamua kiuchumi, huku akiwataka kutumia fursa hizo kwa uaminifu na kurejesha mikopo kwa wakati. Akizungumza katika mkutano na wasafirishaji hao, Mbunge Agnes alisema mikopo hiyo ni miongoni mwa fursa zinazolenga kuwawezesha vijana kuongeza kipato, kuboresha maisha yao na kutoka katika kiwango cha chini cha kiuchumi kwenda kwenye kiwango cha kati. Alisema vijana hao wana nafasi ya kunufaika na mabilioni ya fedha yanayotolewa kupitia programu mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi, ikiwemo kupata bodaboda na bajaji zitakazowawezesha kujiajiri na kuongeza kipato. Mbunge huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya jitihada za kuwawezesha vijana, akieleza kuwa ana faraja kubwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuinua wananchi kiuchumi. “Rais Samia amefanya mambo mengi katika kuwa...

MBUNGE AGNES ATOA ELIMU KWA WASAFIRISHAJI KUHUSU MIKOPO YA BODABODA NA BAJAJI

Na Ghati Msamba, Musoma. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes, ametoa elimu kwa wasafirishaji wa bodaboda na bajaji kuhusu fursa za mikopo inayolenga kuwawezesha kupata vitendea kazi na kujikwamua kiuchumi, huku akiwataka kutumia fursa hizo kwa uaminifu na kurejesha mikopo kwa wakati. Akizungumza katika mkutano na wasafirishaji hao, Mbunge Agnes alisema mikopo hiyo ni miongoni mwa fursa zinazolenga kuwawezesha vijana kuongeza kipato, kuboresha maisha yao na kutoka katika kiwango cha chini cha kiuchumi kwenda kwenye kiwango cha kati. Alisema vijana hao wana nafasi ya kunufaika na mabilioni ya fedha yanayotolewa kupitia programu mbalimbali za kuwawezesha kiuchumi, ikiwemo kupata bodaboda na bajaji zitakazowawezesha kujiajiri na kuongeza kipato. Mbunge huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya jitihada za kuwawezesha vijana, akieleza kuwa ana faraja kubwa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kuinua wananchi kiuchumi. “Rais Samia amefanya mambo mengi katika kuwawezesh...

WANANCHI NJOMBE WAFIKIWA NA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA BILA MALIPO

  Wizara ya Katiba na Sheria, imeanza kutoa Huduma za Msaada wa Kisheria kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe, 18 Septemba, 2026 kwa Lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata haki kwa wakati na Usawa. Akizungumza katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Njombe, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ambaye pia ni mratibu wa zoezi la utoaji wa huduma za kisheria Geofrey Mwachai alisema kuwa huduma hizi zinatolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Awamu ya Pili lengo kuu ikiwa ni kuwafikia wananchi wote na kuhakikisha wanapata haki zao. ‘’Wananchi wengi hawafahamu wapi wanaweza kupata haki zao ama namna gani wanaweza kuzitunza, ila kupitia Kampeni hii ya Msaada wa Kisheria awamu ya pili tutatoa elimu ya kisheria katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu ya haki, wajibu na uraia, ndoa, mirathi, ukatili wa kijinsia na matunzo ya Watoto ili kuwawezesha wananchi kutambua haki zao na pia kufahamu nini wafanye pale wanapodhulumiwa haki hizo”alisema Wak...

PSPTB: WATAHINIWA 275 WAFAULU, 21 WAFELI MITIHANI

 Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza matokeo ya Mitihani ya Kati Awamu ya Pili ya Taaluma ya Mnyororo wa Ugavi, ambapo watahiniwa 275 kati ya 528 waliofanya mitihani hiyo wamefaulu, sawa na asilimia 52.1. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Sept 18,2026 Jijini Dodoma wakati wa kutangaza matokeo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu WA ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi, amesema jumla ya watahiniwa 567 walidahiliwa kufanya mitihani hiyo iliyofanyika kuanzia Agosti 30 hadi Septemba 4, 2026. "Kati yao, watahiniwa 528 walifanya mitihani, huku 39 wakishindwa kufanya kwa sababu mbalimbali". Amesema Mbanyi amesema watahiniwa 232, sawa na asilimia 43.9, wamepata nafasi ya kurudia baadhi ya masomo (referral), huku 21, sawa na asilimia 4.1, wakifeli na hivyo kulazimika kuanza upya masomo yao katika ngazi husika. "Tunawapongeza watahiniwa waliofaulu katika ngazi mbalimbali, wakiwemo waliokidhi sifa za kutunukiwa vyeti vya Professional Diploma,...

MAGANYA: SERIKALI ISIPUUZIE MCHAKATO WA KATIBA MPYA

 NA GHATI MSAMBA, Musoma. MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya, ameiomba Serikali kuendelea na mchakato wa marekebisho ya Katiba, akisema wananchi na vyama mbalimbali bado wanahitaji Katiba Mpya. Maganya alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara. Alisema Serikali haipaswi kusikiliza sauti za watu wanaopinga mchakato huo bila kutoa mawazo chanya, akisisitiza kuwa mchakato wa Katiba Mpya unapaswa kuendelea kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025. “Serikali iendelee na mchakato wa Katiba Mpya kwa sababu wapo wananchi na vyama vingine vinavyohitaji Katiba Mpya. Ni chama kimoja pekee ambacho hakihitaji,” alisema. Alisema suala la Katiba linahitaji utulivu, busara na maridhiano, hivyo kuwataka wanaharakati na wanasiasa kuepuka kutumia nguvu kubwa katika kushinikiza madai yao. Maganya alisema katika kipindi cha takribani wiki mbili kumekuwa na mijadala katika majukwaa mbalimbali kuhus...

MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE, KERO ZA WANANCHI ZITATULIWE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake kuhakikisha hali ya Dampo la Pugu inaboreshwa, huku akielekeza maeneo ya makazi yanayozunguka dampo hilo kupuliziwa dawa ili kuwalinda wananchi dhidi ya wadudu na kupunguza hatari ya magonjwa, hususan katika kipindi cha mvua. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 18, 2026, alipofanya ziara katika Dampo la Pugu linalotumika kukusanya taka za Mkoa wa Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya eneo hilo na kusikiliza kero za wananchi wanaoishi maeneo ya jirani. Aidha, ameelekeza kuandaliwa kwa mpango kazi wa pamoja utakaoainisha hatua za haraka na za muda mrefu za kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa Dampo la Pugu pamoja na kero zinazowakabili wananchi wanaoishi katika maeneo yanayolizunguka, ikiwemo kutopuliziwa dawa za kuua wadudu. Akiwa katika dampo hilo, Mhe. Ndejembi ameonesha kutoridhishwa na kutofautiana kwa takwimu kuhus...

CHATANDA: ZBAR IMETHIBITISHA KUWA INAWEZEKANA KUFIKIA MUAFAKA WA KITAIFA

NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Wananchi na viongozi wa Zanzibar wamepongezwa kwa kufikia muafaka wa kitaifa kwa kuimarisha umoja na mshikamano kuelekea ujenzi wa taifa lenye maendeleo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu (MCC), Mary Chatanda, Septemba 18, 2026, Jijini Dodoma. Chatanda amesema, hakuna shaka kuwa, wananchi na viongozi wa Zanzibar, wamesukumwa na dhamira ya dhati ya ujenzi wa taifa lao badala ya kutanguliza tofauti zao za kisiasa na maslahi binafsi. "Niwapongeze wananchi na viongozi wa Zanzibar ambao waliangalia maendeleo badala ya tofauti zao za vyama, waliangalia Zanzibar waitakayo yenye neema na ustawi badala ya misuguano isiyokwisha, ndiyo maana wakaona wakae pamoja, waelewane ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo," amesema Chatanda. Aidha, Chatanda amempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuwa n...