Skip to main content

Posts

Showing posts from June 6, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Mwinyi Ashiriki Sala ya Eid Al Adha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Eid Al Adha iliyosaliwa Masjid Taqwa, Wilaya ya Kati,  Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar leo tarehe 7 Juni 2025. Mapema baada ya sala hiyo, Rais Dkt. Mwinyi alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kuchinja mnyama(Udh-hiya) ikiwa ni sehemu ya Ibada  na kutoa mkono wa Eid kwa Masheikh wa Mkoa huo.

Sheikh Abubakar Mkama Aongoza Dua Kuombea Uchaguzi Mkuu wa Amani

Na Shomari Binda-Musoma  SHEIKH wa Wilaya ya Musoma Abubakar Mkama ameongoza dua baada ya swala ya Eid el Hajj kuombea uchaguzi mkuu wa amani mwezi oktoba. Dua hiyo iliyomwa kwenye Msikiti wa Taqwa uliopo Songe Kata ya Bweri manispaa ya Musoma licha ya kuombea uchaguzi wamemuombea pia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan afya njema na kuisimamia nchi. Sheikh Abubakar amesema yanapotokea machafuko kwenye uchaguzi wanaoathirika zaidi ni watoto na wanawake hivyo ni muhimu kuombea amani. Amesema kama viongozi wa dini wanalo jukumu la kusisitiza umuhimu wa amani na kuomba dua ili lolote lenye kuvuruga amani lisiweze kutokea. Sheikh huyo amesema ipo mifano kwenye nchi ambazo kupitia uchaguzi kumeibuka machafuko na kusababisha adha kwa wananchi. Amesema kila mmoja anapaswa kulinda amank iliyopo iendelee kuwepo na ujio wa uchaguzi usipelekee kuvuruga amani. " Ndugu zangu katika imani napenda kuzungumzia umuhimu wa kuwa na amani tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba na tusikubali ama...

Kongamano la Usalama wa Kitaifa Lafanyika Chini ya Jwtz

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania limeandaa Kongamano kuhusu Usalama wa Kitaifa lililofanyika katika hoteli ya Gran Meria Jijini Arusha tarehe 6 Juni 2025. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othman amekipongeza Chuo hicho kwa kutengeneza jukwaa muhimu kwa wanataaluma ili kujadili maswala mtambuka hasa wakati huu ambapo kuna matishio mbalimbali yanayoikabili Dunia. Aliwataka washiriki wa Kongamano hilo kujadiliana kwa kina mada zinazowasilishwa ili kuja na suluhisho la changamoto zinazolikabili taifa kwa sasa na kwa siku zijazo. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Tanzania Meja Jenerali Justice Steven Mnkande amesema kuwa Kongamano hilo ni la kwanza kuandaliwa na Chuo hicho likilenga mada tatu ambazo ni matumizi ya Akili Mnemba katika Ulinzi wa Taifa,Usalama wa Chakula kama Msingi wa Uimara wa Taifa na Usalama wa Nishati kwaajili ya Maendeleo Endele...

Tuzuie Huu Mgogoro Kabla Haujawa Janga La Taifa

-Kigwangala Atoa Ushauri Ili "Derby" Ya Kariakoo Ichezeke Juni 15 Yanga Na Simba Na Shomari Binda-GMTV  WAZIRI wa zamani wa Maliasili na mdau wa michezo Hamis Kingwangala ametoa ushauri ili mchezo huo. Uweze kuchezeka kama ulivyopangwa juni 15. Moja ya eneo la ushauri wake alioutoa ni kumalizwa  kwa mgogoro wa Yanga na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa Nchini( TFF).  Amesema mgogoro kati ya Yanga na TFF imefikia kiwango cha hatari anbapo Yanga wametangaza kutocheza mechi hiyo wakidai kunyanyaswa na TFF na Simba wanajipanga kushiriki.  Kigwangala amesema   Ikitokea TFF wakampa Simba ushindi wa mezani Simba akawa bingwa halafu Yanga wakaadhibiwa taifa litaingia kwenye sintofahamu kubwa na Inaweza kusababisha vurugu za mashabiki, maandamano, migomo, au hata usalama wa raia kutishiwa. Amesema serikali inaweza kukaa na pande zote na kuwa na mazungumzo ya kina na kufikia muafaka ili kuweza kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu. "Tulipofikia, mgogoro wa Yanga, Simba...

Serikali na Sekta Binafsi Kuanzisha Vituo Vya Kukodisha Mitambo ya Uchimbaji Madini

▪️Hatua hiyo kuongeza uzalishaji wa madini nchini ▪️Nyamongo kuanzishwa Kituo cha Elimu ya Uchenjuaji Madini ▪️Wachimbaji Wadogo wampongeza Rais Samia juu mafanikio sekta ya Madini ▪️Waziri Mavunde asisitiza juu ya uwezeshwaji Watanzania kimtaji *Musoma,Mara* Serikali kwa ushirikiano na sekta binafsi imejipanga kuanzisha vituo vya ukodishaji mitambo ya uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kutumia teknolojia za kisasa kufanya shughuli zao kwa tija. Hayo yamesemwa leo tarehe 06 Juni, 2025 na Waziri wa Madini, *Mh. Anthony  Mavunde (Mb)* wakati akihitimisha Kongamano la Maonesho ya Madini mkoani Mara kwenye viwanja vya Mukendo vilivyopo Manispaa ya Musoma. "Sote tunatambua kwamba wachimbaji wadogo  hawana uwezo wa kununua na kuihudumia mitambo ya kisasa kama kwa ajili ya uchimbaji.   Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuelekeza Wizara ya Madini kuja na mpango huu ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata fursa ya kutumia teknolojia ya kisasa kwenye sh...

Maonyesho ya Madini Mkoa wa Mara Yameuchangamsha Mji Wa Musoma" Mbunge Mathayo"

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa Jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema kongamano la maonyesho ya madini ya siku 4 mkoani Mara yameuchangamsha mji wa Musoma. Licha ya kuuchangamsha mji yamewawezesha wajasiliamali kufanya biashara na kuwaongezea kipato na kuendelea na maisha. Hayo yamesemwa na mbunge huyo wakati akitoa salamu kwenye kilele cha maonyesho hayo kilichofanyika leo juni 6,2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo. Amesema ofisi ya mkuu wa mkoa kupitia sekta ya madini imefanya jambo kubwa ambalo limefikisha ujumbe namna sekta hiyo ya madini inavyoupaisha mkoa wa Mara na mji wa Musoma  Mathayo amesema kama wabunge wamepitisha bajeti kubwa na nzuri kwa Wizara ya Madini kwa kutambua mchango wake katika kuinua uchumi ukiwemo wa vijana. Mbunge huyo amesema ametoka bungeni kuja kushiriki tukio hilo kwa kuwa linafanyika kwa wananchi anaowawakilisha bungeni na ni muhimu kujumuika nao. " Nishukuru sana ofisi ya mkuu wa mkoa na Wizara ya Madini kwa maonyesho haya...