Skip to main content

Posts

Showing posts from January 21, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Bashungwa awasili Makao Makuu Ya Polisi, Ziara ya Kikazi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa leo tarehe 22 Januari 2025 amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP. Camillus Wambura pamoja na Makamishna wa Jeshi hilo.  Katika ziara hiyo ya kwanza ya Kikazi katika Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri Bashungwa amepokelewa kwa salamu ya gwaride la heshima (Mounted Guard). Pamoja na Mambo mengine, Waziri Bashungwa atafanya kikao na kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali na Watumishi wengine wa Jeshi la Polisi.

Kamati ya Bunge yawapa tano ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana,Ajira na wenye Ulemavu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa namna inavyowagusa wananchi, huku ikimpongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kukuza ustawi na maendeleo ya Watanzania. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Fatuma Toufiq, leo Januari 21, 2025, jijini Dodoma wakati ikipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024. Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete, amesema ofisi hiyo katika mwaka wa fedha 2024/2025 imepanga kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali, zikiwemo usimamizi wa kazi na huduma za ukaguzi, maendeleo ya vijana, kuratibu shughuli za ajira, utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu, hifadhi ya jamii, na ukuzaji wa tija. Ameahidi kuwa ofisi hiyo itatekeleza majukumu hayo kikamil...

CV ya Dkt. Nchimbi imeshiba Mno, anatosha Kwenda Kuwa Msaidizi wa Kwanza wa Rais Samia

Na Bwanku M Bwanku. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza Taifa Tanzania kimekua na wiki ya aina yake kuanzia Jumamosi na Jumapili Januari 18 na 19, 2025 kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. CCM imekua na Mkutano Mkuu wake Maalum ambao ulikua na ajenda mbalimbali kubwa ikiwa kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho baada ya aliyekua akishika nafasi hiyo Ndugu Abdulrahman Kinana kujiuzulu, hatimaye Ndugu Stephen Masatu Wasira akachaguliwa kuziba nafasi hiyo. Kwenye Mkutano Mkuu huu Maalum licha ya ajenda zake Mama zilizokua zinajulikana na shughuli zilizofanyika kama hiyo ya kumchagua Makamu Mwenyekiti, kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Chama na mabadiliko madogo kwenye Katiba yake, kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa CCM na Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Mgombea Urais wa CCM Zanzibar, Mkutano huu umefanya jambo lingine kubwa ambalo halikutarajiwa na yeyote na kutikisa Taifa wakati huu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu hapo baadae. Kwa mshanga...

Waziri Mkuu ateta na Mtendaji Mkuu wa Nmb

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 21, 2025 amekutana na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Januari 21, 2025.

Waziri Mkuu amesema Serikali imefanya Uwekezaji Mkubwa Kwa Tma

▪️Lengo ni kuwezesha utoaji wa utabiri na tahadhari za hali mbaya ya hewa SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ikiwemo upande wa miundombinu ya uangazi wa hali ya hewa na kujenga uwezo wa wafanyakazi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo (Jumanne, Januari 21, 2025) alipozindua Mradi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani wa “Systematic Observation Financing Facility (SOFF) - Project” katika Ukumbi wa Hotel ya Midland Inn View, Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la Serikali la kuendelea kufanya maboresho hayo ni kuwezesha utoaji wa utabiri wa hali ya hewa na tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa. Amesema miongoni mwa uwekezaji huo ni ununuzi wa rada saba za hali ya hewa, upanuzi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa na uboreshaji wa vifaa vya hali ya hewa kwa kuondoa vifaa vinavyotumia zebaki kwa mujibu wa matakwa ya Mkataba wa Minamata. Wazi...

Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Bukoba wapewe Onyo Kali

 Na Angela Sebastian; Bukoba WENYEVITI na wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wametakiwa kutowatoza wananchi kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kulipia huduma pale wanapofika katika ofisi za Serikali ya mitaa na kata bali fedha hiyo iwe inatambulika kisheria. Wito huo umetolewa na  Meya wa Manispaa hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Nshambya Godsoni Gibsoni wakati akiongea katika mafunzo aliyoyaanda yeye ya kuwajengea uwezo na kuwapa vitendea kazi  viongozi wa mitaa katika kukuza maendeleo ya wananchi na kuwapongeza kwa kuchaguliwa. Gibson amesema baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatozwa ela kiasi cha shilingi 5,000 wanapokwenda kupata huduma kwa wenyeviti,wajumbe na watendaji kwa ajili ya kupata huduma hivyo ndipo akaamua kutoa vitendea kazi ikiwemo karatasi kwasababu wapo wananchi ambao hawana ela hiyo.  "Inawezekana inatolewa hiyo ela wasababu ya ulipaji wa ada kwa ajili ya kununua karatas...

Serikali imefanya Uwekezaji Mkubwa kwa Tma-Majaliwa

▪️Lengo ni kuwezesha utoaji wa utabiri na tahadhari za hali mbaya ya hewa SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ikiwemo upande wa miundombinu ya uangazi wa hali ya hewa na kujenga uwezo wa wafanyakazi. Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo (Jumanne, Januari 21, 2025) alipozindua Mradi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani wa “Systematic Observation Financing Facility (SOFF) - Project” katika Ukumbi wa Hotel ya Midland Inn View, Dodoma. Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la Serikali la kuendelea kufanya maboresho hayo ni kuwezesha utoaji wa utabiri wa hali ya hewa na tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa. Amesema miongoni mwa uwekezaji huo ni ununuzi wa rada saba za hali ya hewa, upanuzi wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa na uboreshaji wa vifaa vya hali ya hewa kwa kuondoa vifaa vinavyotumia zebaki kwa mujibu wa matakwa ya Mkataba wa Minamata. Wazi...

Diwani Mariam aridhishwa Ukarabati Majengo ya Madarasa Shule Msingi Mwembeni

Na Shomari Binda-Musoma DIWANI wa Kata ya Mwigobero manispaa ya Musoma Mariam Sospeter ameridhishwa na ukarabati wa majengo unaofanywa kwenye shule ya msingi Mwembeni iliyo chini ya Kata hiyo. Akizungumza mara baada ya ziara ya Kamati ya Siasa ya Kata ya Mwigobero ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) iliyofanyika leo januari 21 ameona kazi nzuri inayofanyika. Amesema kama diwani wa Kata anayepigania miradi ya Kata kwenye vikao vya halmashauri na kuona kazi zinakwenda Mariam ambaye ni diwani pekee wa Kata Mwanamke kwenye baraza la madiwani amesema Mwigobero ipo salama na viongozi wa chama na serikali wanafanya kazi kwa ushirikiano. Amesema elimu ni suala la msingi kwenye suala la maendeleo hivyo kuwa na sehemu nzuri ya watoto kusomea ni jambo jema. Mariam amesema kama kiongozi kupitia ziara hiyo ya Kamati ya Siasa ameridhiswa na ukarabati unaoendelea kwenye majengo ya madarasa.  " Leo tumefanya ziara ya Kamati ya Siasa kwenye shule yetu ya Mwembeni  na moja ya maeneo tuliyopitia ni uk...