Skip to main content

Posts

Showing posts from January 18, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Polisi Mwanza yaendeleza Elimu Visiwani Kukomesha Uhalifu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeendea kutoa elimu na kuimarisha hali ya ulinzi kwenye visiwa vya Yozu, Nyamango, Chembaya, Soswa, Zelagula Gembale na Kasalazi Halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoani humo. Akizungumza na wakazi wa Kisiwa cha Yozu, leo Jumamosi, Januari 18.2025 Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lwelwe Mpina amewataka wananchi kutojihusisha na uhalifu wa kuiba mazao uvuvi sambamba na kuacha uvuvi haramu. Aidha, ACP Mpina amewataka wananchi wa visiwa hivyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kufichua wahalifu wanaojificha kwenye visiwa hivyo. Kwa upande wao, wakazi visiwa hivyo, wamepongeza jitihada zinazofanywa na Jeshi  la Polisi za kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli za maendeleo bila kuwa na hofu yoyote ya kiusalama. *Kutoka Dawati la Habari Polisi Mwanza*

Steven Wasira achaguliwa kwa Kishindo kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara

Na Mwandishi Wetu, Dodoma Mwanasiasa Mkongwe nchini, Stephen Masatu Wasira amechaguliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho tawala - upande wa Tanzania Bara. Mkutano huo umefanyika leo Januari 18, 2025 jijini Dodoma, ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassam, ambapo Wasira amepigiwa kura za ndiyo 1,910 sawa na asilimia 99.42 ya kura halali 1,917 huku kura 7 zikimkataa. Jina la Wasira lilipendekezwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa jana, kisha kuwasilishwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambayo nayo kupitia kwa Mwenyekiti Rais Samia imeliwasilisha kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa leo kwa ajili ya kupigiwa kura za ndio, au hapana. Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Wasira amewashukuru wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa chini ya Mwenyekiti Rais Samia, kwa kumuamini na kumpa heshima ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara. Wasira ameahidi kuanza k...

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza Adrian Tizeba awaomba Wajumbe Kumchagua Tundu Lissu

 Anaandika Adrian Magoke Tizeba - Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Mkoa wa Mwanza, 0754841003. Wito kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu; Mchagueni Tundu Lissu Kukiongoza CHADEMA! Kwa nini? 1. Kwa sasa, CHADEMA ndiyo alama ya Upinzani katika Tanganyika na Taifa kwa ujumla. 2. Tanganyika na Watu wake, kwa sasa imekabwa kabali na Wezi na Wanyonyaji wa CCM ambao ni wabaya zaidi kuwahi kutokea, Hivyo inahitaji kukombolewa ! 3. Kwa sasa 2025 na Kuliko wakati mwingine wowote, CHADEMA kinamhitaji Kiongozi madhubuti (yaani Mwanaume, Mtanganyika, Mzalendo wa kweli aliye tayari hata kufa kwa ajili ya nchi yake, mzoefu wa mapambano dhidi ya CCM, anayefahamika vilivyo nchini na Mwenye hofu ya Mungu) atakayeongoza vita ya CHADEMA ama Upinzani, Kuing'oa CCM Madarakani ! 4. Kwa bahati mbaya sana, Mheshimiwa Freeman Mbowe sasa hivi, amepoteza sifa za Kuongoza Mapambano haya makali, mfano:  i. Ameishiwa pumzi na mbinu mpya hivyo lazima abadilishwe ii. Anashukiwa kuwa ni dalali wa CCM na hivyo kuwa msal...

Serikali yafanya Utafiti wa Hali Ya Upatikanaji na Matumizi ya Nishati Nchini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inafanya utafiti wa tatu wa hali ya upatikanaji na matumizi ya nishati katika mikoa yote ya Tanzania Bara.  Hayo yameelezwa Januari 17, 2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Godfrey Chibulunje. "Huu ni utafiti wa tatu kuwahi kufanywa na Wakala na hapa Serikali imelenga kubaini hali ya usambazaji na matumizi ya nishati ili kuboresha mipango yake katika sekta ya nishati kwa upana wake," alisema Mha. Chibulunje. Alisema ili kupata takwimu sahihi zenye uhalisia ambazo zitatumika kwenye uandaaji wa miradi ya usambazaji wa nishati mbalimbali ikiwemo ya umeme, kupikia na ujenzi wa vituo vya mafuta vijijini; Wakala kwa kushirikiana na NBS wapo katika hatua ya ukusanyaji wa taarifa katika mikoa yote Tanzania Bara. "Kwa sasa hatua inayoendelea kote nchini ni ukusanyaji wa taarifa ambao ni moja ya hatua muhimu katika utekelezaji wa ...