Skip to main content

Posts

Showing posts from July 13, 2024

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Semfuko Awataka Watanzania Kutumia Fursa za Ufugaji Wanyama Pori

Na. Beatus Maganja  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini - TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa za ufugaji wa wanyamapori zinazopatikana katika Taasisi ya TAWA. Ameyasema hayo Julai 13, 2024 alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Katika Maonesho ya 48 ya biashara ya Kimataifa ambayo kwa Mwaka 2024 leo yamefikia tamati. "Sehemu kama Afrika ya Kusini ufugaji wa wanyamapori ni mkubwa sana, kwahiyo mimi natoa rai kwa wananchi hasa watanzania kuingia katika biashara hiyo ya ufugaji wa wanyamapori" amesema. Aidha Meja Jenarali (Mstaafu) Semfuko amesema ili watanzania waweze kupata kitoweo cha nyamapori kwa urahisi wanapaswa kuingia katika biashara ya ufugaji wa wanyamapori na kwakufanya hivyo wataziwezesha bucha za wanyamapori kufanya kazi vizuri. Sambamba na hilo, Semfuko amesema TAWA ina mipango mingi ya kuhakikisha  inapata wawekezaji wakubwa na wadogo ili wawekeze katika maeneo ...

Tanroads Mara Yatoa Elimu Kwa Wananchi Juu ya Utunzaji na Uhifadhi wa Barabara

Na Shomari Binda-Musoma WANANCHI wa eneo la Kariakoo Kata ya Bweri manispaa ya Musoma wamepewa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa barabara. Elimu hiyo imetolewa na Wakala wa Barabara Tanroads mkoa wa Mara jana julai 12 kwenye eneo hilo huku ikipangwa  kutolewa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara. Moja ya elimu iliyotolewa  ni kuacha kufanya biashara eneo la barabara kwani usababisha ajali kwa madereva kwa kupunguza upeo wa kuona. Meneja wa Tanroads mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amesema barabara ni kiungo muhimu cha mawasiliano kwa jamii katika sekta ya usafirishaji na ipo kwa mujibu wa Sheria ya Barabara ya mwaka 1932 na Sheria ya mwaka 1962 na Sheria mpya ya barabara ya mwaka 2007. Amesema baada ya kujenga barabara kulingana na mahitajj ya wakati huo eneo la hatua kadhaa uachwa kila upande wa barabara kwaajili ya upanuzi wa baadae wa barabara au kupisha barabara ya mchepuko pale panapokuwa na matengenezo kwenye barabara. Mhandisi Maribe amesema kwa kuzingatia Sheria ya ba...

Rais Dkt Samia Awataka Wananchi Kuacha Kuvamia Maeneo ya Hifadhi

Na Happiness Shayo - Katavi  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kuacha kuvunja sheria kwa kuvamia maeneo ya hifadhi na badala yake kutunza mazingira hayo. Kauli hiyo imekuja kutokana na maombi ya Mbunge wa Mlele, Mhe. Isack Kamwelwe aliyeomba kumegewa ardhi katika maeneo ya hifadhi ya mapori yaliyopo jimboni kwake. Ameyasema hayo leo Julai 13,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mlele, Kata ya Inyonga Mkoani Katavi. "Tunajua kuna uhaba wa Ardhi na kuna maeneo ya hifadhi mnayatamani lakini hayaendani na kuvunja sheria tukae tuzungumze tuangalie namna ya kuyamega na si kuvamia" amesisitiza Mhe. Rais Samia. Awali, akitoa ufafanuzi kuhusu ombi la Mhe. Kamwelwe  la kuongezewa hekta elfu 15 katika Pori la Akiba Inyonga,Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea maombi hayo na inaendelea kufanya tathimini kuangalia uhitaji halisi na kuyawasilis...