Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga. Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina ardhi kubwa na yenye retuba ya kutossha inayofaa kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuifanya wilaya hiyo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji katika kilimo na biashara. Hayo yameelezea na Mkurungenzi wa Halmashauri ya hiyo Naima Chondo kufuatia ushindi wa kitaifa waliopata katika maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya usagara jijini Tanga. Hivyo basi Chondo amewakaribisha wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo katika halmashauri hiyo ikiwemo katika sekta ya Kilimo kwa kuwekeza katika uzalishaji wa mazao ya kisasa na kujenga viwanda vya kuchakata mazao hayo ili kuongeza thamani na kipato kwa wakulima. Chondo ameendelea kusema kuwa maandalizi mazuri na juhudi za kuwawezesha wakulima wadogo kushiriki maonesho ya siku ya chakula duniania pamoja na kujifunza teknolojia mpya za kilimo na kupata fursa ya kuonesha ubora wa mazao wanayozalisha na mnyororo mzima wa thamani...
Na Ssgt Mawazo Mtondo - MBEYA. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, leo Oktoba 17, 2026, amefunga rasmi mafunzo ya awali ya Askari Wanafunzi wa Jeshi la Magereza, Kozi Na. 33, yaliyodumu kwa takribani miezi tisa katika Chuo cha Magereza Kiwira, jijini Mbeya. Jumla ya askari wanafunzi 1,561 wamehitimu mafunzo hayo, wakiwemo wanawake 367 na wanaume 1,194, kati ya wanafunzi 1,564 walioanza mafunzo. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Rwezimula amewataka wahitimu kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uadilifu na nidhamu, kwa kuzingatia sheria na taratibu za Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla, huku wakitanguliza maslahi ya Jeshi na Taifa. Pia, amewasisitiza kuzingatia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa hali ya hewa kuhusu mvua za El Nino. Baada ya kukagua gwaride la wahitimu, Dkt. Rwezimula alizindua nyumba tatu za makazi ya askari zenye uwezo wa kuhudumia familia sita. Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Magereza amemshukuru Rais wa Jamhu...