Wananchi wamehimizwa kuachana na imani potofu kuwa Miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa skimu za umwagiliaji inayotekelezwa na Serikali kwenye maeneo yao ni matambiko. Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kuwa imani hizo zikiwemo za kutaka miradi hiyo isitishwe haikubaliki na kuwataka watanzania kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya skimu za umwagiliaji Bashe ameyaeleza hayo katika mwendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora ambapo ametembelea eneo la mradi wa Umwagiliaji wa Mwasimbo Igunga, Mwampuli, Mwanzugi na Makomero. Waziri Bashe, ameeleza kushangazwa na hatua ya baadhi ya wananchi wa halmashauri yaNzega vijijini kupinga utekelezaji wa miradi ya skimu za umwagiliaji unaohusisha ujenzi wa miundombinu ya bwawa la Nsembo, ujenzi wa barabara, madaraja madogo na mitaro ya kupitisha maji pembezoni mwa barabara. Wananchi wa eneo hilo wanapinga miradi hiyo kwa imani potofu ...
Marato tv - Sauti ya Jamii