Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo anatarajiwa kufanya ziara kwenye Kata ya Bukima yenye lengo la kufufua ari ya kuchangia miradi ya maendeleo. Ziara hiyo itafanyika baada ya kumalizika kwa ziara na mkesha wa Mwenge wa Uhuru utakaokuwa Bukima jumatano julai 31 Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge imesema baada ya mkesha huo wa Mwenge Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo atafanya ziara maalum kwenye Kata ya Bukima yenye malengo ya kufufua ari ya wananchi kujitolea kuchangia miradi yao ya maendeleo. Taarifa hiyo imesema ipo miradi iliyokwama zaidi ya miaka 5 Kata ya Bukima, ikiwemo kukosa maabara hata mmoja kwenye sekondari ya Kata huku vifaa vilivyochangwa na mbunge vikiwa stoo. Mradi mwingine uliokwama ni wodi ya mama mtoto kwenyez ahanati ya Bukima ikiwa inajengwa kwa zaidi ya miaka mitano ambapo mbunge wa jimbo alichangia saruji ya ujenzi. Katika Kijiji cha Butata ujenzi wa zahanati umesi...
Marato tv - Sauti ya Jamii