Mkuu wa Mkoa Songwe Awataka Wananchi,Kamati ua Ulinzi na Usalama Kuwa Macho na Miradi ya Umwagiliaji *
NA MWANDISHI WETU MKUU wa Mkoa wa Songwe Jabir Makame, amewataka wananchi wa mkoa huo na kamati ya Ulinzi na Usalama kuwa macho na kutocheka na yeyote anayehujumu miradi ya Umwagiliaji. Amesema fedha zinazowekezwa na Serikali katika miradi hiyo ni nyingi na Imelenga kupunguza umaskini kwa wakulima hivyo anayehujumu miradi ya Umwagiliaji anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa analihujumu Taifa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir amesema hayo wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa mradi wa skimu ya Umwagiliaji Naming’ongo uliopo kata ya Chitete mkoani humo. Amesema mradi huwo wa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 24 utatekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambapo ndani ya mradi huo kutakuwa na ujenzi wa barabara za ndani, ajira zaidi ya 2000 huku wakulima zaidi ya 6000 wakiwa wanufaika wa eneo hilo. “Wananachi na kamati ya ulinzi na usalama tuchukue hatua kwa watu wanaoharibu miundombinu ya Umwagiliaji, kamati yetu ichukue hatua ili kukomesha tabia hizo, shughu...