Na Angela Sebastian-Bukoba MAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA ) imewashauri wananchi kutambua umuhimu wa faida za kudai na kutoa risiti pindi wanaponunua na kuuza bidhaa kwani hiyo inasaidia na kuwalinda pale ikatokea changamoto hususani wizi,pia inaongeza ulipaji kodi kwa ufanisi. Hayo yameelezwa na Afisa uhusiano mkuu kutoka TRA makao makuu Hudson Kamoga wakati akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera katika mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na mamlaka hiyo, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa elimu juu ya kazi zinazofanywa na TRA hususani wajibu wa ulipaji kodi kwa ihari. "Wanaponunua na kudai risiti wanatimiza wajibu wako kisheria,ni uzalendo kwa nchi yao pia ni ulinzi wa bidhaa waliyoinunua mfano amenua simu bila risiti ikatokea kuna mtu mwingine aliibwa simu kama ya kwako huwezi kujitetea kwamba hiyo ni mali yako kwasababu, huna uthibitisho ambao ni risiti inayoonyesha uhalali wa umiliki wa mali hiyo"anasema Kamoga Amesema waandishi wa habari wanao wajib...
Marato tv - Sauti ya Jamii