Na MASHAKA MHANDO, Tanga MATUMIZI ya mitandao ya kijamii jijini Tanga yamechukua sura mpya ya kiuchumi, baada ya vijana zaidi ya 150 kunufaika na mradi maalum wa ujuzi wa kidijitali uliowatoa mitaani na kuwafanya kuwa watengeneza maudhui (Content Creators) wanaojitegemea na kujingizia kipato. Mradi huo umewasaidia vijana kuachana na dhana potofu kuwa mitandao ya kijamii haina faida, na badala yake wamepewa ujuzi wa kuandaa maudhui, kupiga picha, na kuhariri kazi zenye viwango vinavyokidhi masoko ya mtandaoni. Miongoni mwa shuhuda za kusisimua za mradi huu ni ya Peter Msuya, kijana ambaye awali alikuwa fundi stadi wa kutengeneza vitanda na makochi (Sofa). Peter anasema maisha yake yamebadilika kabisa baada ya kujiunga na mafunzo hayo ya kidijitali. "Nashukuru sana mafunzo niliyopata. Leo hii ukurasa wangu unafuatiliwa na watu milioni mbili! Kama siyo mradi wa 'Tanga Yetu', saa hii ningekuwa nagombana na wateja ambao sijawatengenezea vitanda vyao kwa wakati. Sasa naweza ku...
Marato tv - Sauti ya Jamii