Skip to main content

Posts

Showing posts from February 3, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Makamu wa Rais Akutana na Waziri wa Fedha

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Mkoani Dodoma, leo tarehe 03 Februari 2025.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Awataka Watanzania Kushiriki Kudhibiti Silaha

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura amewataka watanzania wote kushiriki katika jukumu la udhibiti na usimamizi wa Silaha ili kulinda nchi yetu ikiwa ni utekelezaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. IGP Wambura ameyasema hayo Februari 3, 2026 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kamati ya Udhibiti na Usimamizi wa Silaha pamoja na kufungua Kikao cha kwanza cha Kamati hiyo kinachofanyika kwa siku tatu ambapo zitawasilishwa mada mbalimbali za  kuwajengea uwezo wana kamati ili kufahamu majukumu yao, sheria na kanuni,itifaki za kikanda na kimataifa zitakazo waongoza katika jukumu la kudhibiti na kusimamia silaha na risasi nchini. Amesema, changamoto ya uzagaaji wa silaha haramu kwa kiasi kikubwa ulitokana na migogoro kwa baadhi ya nchi zinazoizunguka Tanzania, kuwepo kwa mipaka isiyo rasmi na ukiukwaji wa sheria.  Aidha, alisema changamoto hiyo ilikuwa kubwa katika miaka ya 2000 kurudi nyuma kutokana na machafuko yaliyokuwa yanaendelea nchi jirani lakini...

Dkt. Mwigulu Akutana na Dkt. Biteko

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Doto Biteko, ofisini kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Februari  3, 2026.

Kiti cha Umeya Chamwenea Meya Alex,Akiongoza Kikao Cha Bajeti Halmashauri Manispaa ya Musoma

Februari 2, 2026, Baraza la Madiwani la Manispaa ya Musoma limefanya kikao cha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2026–2027 kwa lengo la kujadili ajenda mbalimbali zinazohusu mapato na matumizi ya Manispaa. Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Meya wa Manispaa ya Musoma, Mheshimiwa Alex Nyabiti, ambapo wajumbe wa Baraza walipata fursa ya kuchangia hoja mbalimbali zenye lengo la kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Manispaa. Katika michango yao, wajumbe walihoji hali ya ukusanyaji wa mapato kutoka vibanda vilivyopo maeneo mbalimbali ya Manispaa, wakibainisha kuwa makusanyo hayo bado ni madogo ukilinganisha na idadi halisi ya vibanda vilivyopo.  Aidha, ilielezwa kuwepo kwa tofauti za ulipaji kodi, ambapo baadhi ya vibanda hulipa kodi ndogo huku vingine vikitozwa kodi kubwa. Vilevile, suala la leseni za biashara kwa vibanda lilipewa uzito, ambapo ilisisitizwa kufuatiliwa kwa karibu ili kuongeza mapato ya Manispaa. Kufuatia hilo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma alieleza kuwa ameunda Tume y...

Majiko Banifu ya Ruzuku Yapiga hodi Shinyanga

  📌 *Majiko banifu 5,236 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Shinyanga*  📌 *Wilaya nne (4) kunufaika na mradi*  📍 *Shinyanga*  Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Katibu tawala msaidizi rasilimali watu, Ndugu David Lyamongi leo Februari 03, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedit Malulu amesema,Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao utasaidia kupunguza athari za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi ya nishati  isiyo salama ya kupikia. Aidha, usambazaji na uuzaji wa majiko haya banifu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia wenye dhima mpaka  ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania wawe wanatu...

Rais Samia Aanza Ziara Rasmi Dubai Uae Kwa Kukutana na Viongozi na Wadau wa Kimataifa

 Leo Jumanne, Februari 3, 2026, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameanza ziara ya kikazi Dubai, UAE kwa kufanya mazungumzo na viongozi na wadau wa kimataifa.  Katika ratiba ya leo, Rais Samia anakutana na Mhe. Gaston Browne, Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda, pamoja na kufanya mazungumzo ya pande mbili na Bi. Shaikha Al Nuwais, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha ushirikiano, diplomasia ya kiuchumi na kuvutia uwekezaji wa moja kwa moja nchini. Jioni ya leo, Rais Samia atashiriki uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS)— jukwaa la uwekezaji linalolenga kuoanisha miradi iliyo tayari kuwekezeka barani Afrika na wawekezaji wa kimataifa. GAIS ni mpango wa kimkakati unaoendeshwa sambamba na majadiliano ya sera ya World Governments Summit (WGS), kwa lengo la kubadili majadiliano ya sera kuwa uwekezaji halisi wenye matokeo. Tufuatilie kupitia akaunti rasmi za Ikul...

Serikali Kununua Matrekta 10,000-Dkt. Mwigulu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imepanga kununua matrekta 10,000 na kuanzisha vituo jumuishi 1,000 vya huduma za zana za kilimo katika ngazi ya Kata, hatua itakayoongeza tija, kupunguza gharama na kuwapa wakulima muda zaidi wa kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi. Ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Februari 3, wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Kikanda wa Afrika wa Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo unaofanyika katika Hotel ya Johari Rotana, Dar es Salaam ambao unalenga kuweka msingi wa ushirikiano wa kikanda katika kuendeleza Ajenda ya Mfumo wa Zana Endelevu za Kilimo Barani Afrika (F-SAMA). Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema ni muhimu kuimarisha uwekezaji katika zana za kilimo rafiki kwa mazingira na zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi. “Zana hizi zinapaswa kupunguza uzito wa kazi, kuongeza tija, kupunguza upotevu wa mazao, na wakati huo huo kulinda mazingira kwa kutumia teknolojia zinazohimili athari za tabianchi kama ukame na mabadiliko ya misimu.” “Tunapaswa ...

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete Akutana na Mfalme Mswati III

 -Kujadili upatikanaji wa fedha za miradi ya afya kwa nchi wanachama wa ECSA  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ameshiriki Mkutano wa 67 wa Mawaziri wa Afya kutoka nchi 9 wanachama za Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika  (ECSA-HC) unaofanyika Ezulwini, Ufalme wa Eswatini tarehe 2-3 Februari, 2026.  Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo umejadili mikakati ya kuimarisha mifumo ya afya ya nchi wanachama wa ECSA-HC, hususan kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea duniani kote yaliyopelekea kupungua au kusitishwa kabisa kwa upatikanaji wa fedha za kufadhili miradi ya afya kutoka kwa wafadhili waliozoeleka.  Katika hotuba akifungua Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa ECSA-HC, Dkt. Kikwete alitoa rai kwa nchi hizo kuwa wabunifu katika kubuni na kutafuta vyanzo mbadala vya rasilimali za kifedha ili kuhakikisha kuwa miradi il...