Skip to main content

Posts

Showing posts from January 13, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mchango wa GGM waibua tumaini kwa watoto 420 wenye matatizo ya moyo

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), inahitaji shilingi bilioni 1.6 kwaajili ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto 420 wanaougua maradhi ya moyo ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu yao. Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Heart Team Foundation Africa, Dk Naiz Majani, aliyezungumza kwa niaba ya JKCI wakati wa hafa ya kuupongeza mgodi wa madini wa Geita Gold Mine (GGM) kwa kusaidia upasuaji wa watoto 14 wanaougua moyo katika taasisi hiyo. Alisema HTFA kwa kushirikiana na JKCI mwaka jana walifanya harambee kukusanya fedha za matibabu kwa wagonjwa wa moyo ambapo GGM ni miongoni mwa wadau wengi waliotoa fedha kugharamia matibabu hayo. “Tulipowaomba GGM walichangia shilingi milioni 56, matibabu ya moyo ni gharama kubwa sana duniani kote na kwa hapa Tanzania  asilimia 70 ya matibabu hayo gharama inakuwa kwa serikali na asilimia 30 kwa wazazi lakini bado asilimia 30 ni kubwa sana kwa mtanzania wa kawaida,” alisema Alis...

Hakuna Taifa Endelevu Bila Usimamizi wa Haki - Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Taifa  lenye maendeleo  endelevu na ustawi   wa  watuwake bila usimamizi mzuri wa haki Dkt. Samia ameeleza hayo leo januari 13, 2026 wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha mahakama na majaji Tanzania (TMJA) uliofanyika viwanja vya makao makuu mahakama mkoani Dodoma Uwepo wa mahakama huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu  ya utawala  bora na msingi wa upatikanaji wa haki Serikali itaendelea kuulinda na kuuheshimu uhuru wa mahakama bila kujali itikadi.  Ametoa rai kwa majaji na mahakama  kuwa uhuru huu hamna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu, nidhamu na utii wa sheria na uzalendo kwa Taifa letu.  Aidha amesema Watanzania wanamatumaini makubwa sana na wangependa kuona mahakama inagosimamia haki kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya kikatiba sheria na utu.  Kwa Upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Ndg.George Masaju ameiomba...

Injini ya Chama Cha Mapinduzi Ipo Mashinani; Dkt.Migiro

-Asisitiza mabalozi kupandisha bendera za chama kwenye maeneo yao. -Asema chama kinawajali na kuwathamini mabalozi. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amesema maendeleo ya kweli kwa wananchi huanzia katika mashina ya Chama hicho, akisisitiza kuwa jitihada zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupata nguvu kupitia uongozi wa ngazi za chini. Dkt. Migiro ambaye ni Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke tangu chama hicho kianzishwe,  amesema hayo katika mkutano wake na Mabalozi wa Mashina wa CCM katika Wilaya ya Ilala, ikiwa ni hitimisho la ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam yenye lengo la kuimarisha uhai wa CCM kuanzia kwenye mashina Kwa kauli mbiu ya "Shina lako linakuita". Akizungumza na Mabalozi hao amesema mashina ndiyo sehemu ya kwanza ya wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo, kwa kuwa ndiko wanakotoka wananchi wenyewe na ndiko changamoto zao halisi zinapojadiliwa. Ameeleza kuwa mahusiano kati ya maendeleo ya jamii n...

Madiwani Tanzania Wamjia Juu "Kigogo"Kwa "Umbea" Wake

 Umoja wa Madiwani CCM umesikitishwa na kitendo cha kuchapishwa na kusambazwa kwa ujumbe unaohusu Posho za waheshimiwa Madiwani, Ujumbe uliochapishwa na kusambazwa kupitia Account ya Kigogo Kigogo katika Mtandao wa Facebook.  Aidha Umoja huo Umeutaarifu umma wa Tanzania kupuuza ujumbe huo wa upotoshaji na uchochezi unaolenga kuichafua serikali pamoja na Heshima ya Waheshimiwa Madiwani Nchini.  Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Karibu wa Madiwani wa CCM Tanzania Hilda kadunda pamoja na kulaani vikali tulip hilo imeviomba vyombo vya dola pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini kuwachukulia hatua wote wanaohusika ili kukomesha kabisa za Wanaharakati wachochezi na Wasiolitakia Mema Taifa.  "Madiwani wa Tanzania tunao utaratibu rasmi wa kuwasiliana na serikali yetu kwa Jambo lolote na kwa wakati wote, Hivyo Madiwani kwa umoja wetu Tunamshukuru kwa dhati Rais wetu Mpendwa Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa msikivu na Mwenye kujali maslahi ya Waheshimiwa Madiwani...

Rais Samia Kama Mwalimu Julius Nyerere

  Leo tarehe 13/1/2026 Rais wa jamuhuri ya Muungano wa tanzania amevunja rekodi kwa kuwa *Rais wa pili nchini tanzania* kufungua mkutano wa majaji na mahakama tangu mwaka 1984 ambapo *Hayati Mwl. Julius K nyerere* alihutubia mkutano huo. Katika mkutano huo Rais samia ameiomba mahakama kuwa chombo huru na chenye utoaji wa haki kama ilivyoainishwa kwenye *ibara ya 107 na 107B* ya katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia rais ameahidi kuwa serikali itaendelea kuuheshimu na kuulinda uhuru wa mahakama kama sheria za nchi zinavyotaka. Rais samia amepasua mwamba kwa kuwaomba majaji na mahakimu kutendea haki watu, amesema *sio sahihi watu kuwekwa mahabusu au kufungwa kwa makosa ya kubambikiwa,* amewaomba majaji kuwa huru na kufanya kazi kwa kujipima ili kuondoa uonevu kwa watu wasio na hatia. Rais samia amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya mahakama, mfano jengo la mahakama la pili kwa ukubwa zaidi barani afrika na la sita kwa ukubwa duniani la *Judiciary squ...