Skip to main content

Posts

Showing posts from May 16, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mtendaji Mkuu Tarura:Mradi Wa Tactic Utainua Uchumi Na Kubadilisha Mandhari Jiji La Arusha

Arusha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji Tanzania kwa Awamu ya Pili (TACTIC) jijini Arusha kutabadilisha muonekano na mandhari ya jiji hilo kuendana na hadhi yake ya mkoa wa kitalii, kuongeza fursa za ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha hali ya biashara na hivyo pia kuchangia maendeleo ya kijamii. Mhandisi Seff amebainisha hayo hivi karibuni jijini Arusha wakati wa utiaji saini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo utakaohusisha ujenzi wa kituo kikuu cha Mabasi Bondeni city, Ujenzi soko kuu la Kilombero, Ujenzi soko la Morombo pamoja na uboreshaji wa bustani ya mapumziko ya Themi Living Garden, miradi itakayotekelezwa na mkandaradi M/s Mohammed Builders Limited kwa gharama ya 30,625,112,436.85 bila ya VAT. Kulingana na Mhandisi Seff kukamilika kwa Kituo kikuu cha Mabasi Jiji la Arusha kutawezesha uwepo wa vibanda vya wafanyabiashara 900 kutoka 250 v...

Luhemeja Kupambana na Gugu Maji Ziwa Victoria

 Na Ada Ouko, Mwanza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mha. Cyprian Luhemeja akifuatilia zoezi la usafishaji Ziwa Victoria katika eneo lililoathirika na Gugu Maji eneo la Busisi wilayani Sengerema hadi eneo la Kigongo Feri wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Mei 15, 2025. Zoezi hilo linaendelea kufanyika kwa njia mbalimbali kupitia vijana wanaokata kwa kutumia panga pamoja na Mtambo wa kusafisha na kuchimba kina cha maji ‘Watermaster’ ambao unauwezo wa kusafisha eka moja kwa siku. Wakati zoezi hilo likiendelea tayari hatua zaidi zimeendelea kuchukuliwa ikiwa pamoja na ununuzi wa mitambo mitatu ambayo ipo katika hatua za awali.

Jumuiya Ya Wazazi Mara Yasisitiza Usimamizi Wa Maadili Kwa Watoto

Na Shomari Binda-Rorya JUMUIYA ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara imesisitiza maadili mazuri kwa watoto ikiwemo usimamizi mzuri wa malezi kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili. Msisitizo huo umetolewa leo mei 16,2025 na Katibu wa jumuiya hiyo mkoa wa Mara Baraka Mwachula katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa huo kukagua uhai wa jumuiya na chama na masuala mengine. Akizungumza na Kamati za Utekeleza za Kata wilayani Rorya licha ya mambo mengine amesema suala la maadili ya watoto lina umuhimu mkubwa na kila mmoja anapaswa kulisimamia. Amesema mmomonyoko umekuwa mkubwa kwenye jamii na bila kuliangalia na kusimamia hali itakuwa mbaya zaidi. Baraka amesema jumuiya ya wazazi moja ya majukumu yake ni kusimamia malezi na maadili hivyo kila kiongozi na mwanacha atekeleze majukumu hayo. " Ndugu zangu wana Rorya leo ni siku ya kwanza ya ziara yangu wilaya za mkoa wa Mara na nimeanzia hapa wilayani Rorya na nimeona nianze na hilo la maadi...

Tanga Yetu kuwanufaisha kiuchumi vijana wa Tanga

Na Mashaka Mhando, Tanga SHIRIKA la Tanga Yetu Initiative imeanza kutekeleza miradi mbalimbali kwa vijana yenye lengo la kuwainua kiuchumi kupitia elimu, uvuvi, mazingira na teklonojia ya Mawasiliano ya Habari. Akizungumza wakati wakizindua miradi hiyo ya awamu ya pili, Mratibu wa miradi wa Tanga Yetu, Patrick Waziri alisema progamu hiyo itayodumu kwa miezi 21 inatekelezwa kwa mwamvuli wa miradi ya majiji inayofadhiliwa na shirika la nchini Uswisi la Botnar Foundation. Alisema lengo la kutekeleza miradi hiyo ni kuendeleza afya na ustawi wa watoto na vijana wa Jiji la Tanga ili kuwainua kiuchumi. Alisema awali walitekeleza miradi ya awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 2019 nakuishia 2023 ambayo walitekeleza miradi 20 ikiwemo kufanya utafiti uliozaa kupanuka kwa wigo na kuongeza miradi zaidi. "Leo tunazindua miradi ya elimu, mazingira kwa maana suala la ukusanyaji wa taka, uchumi wa blue kwa kufanya kilimo Cha kisasa kupitia bahari na vijana kufundishwa masuala la teklonojia," alis...

Serikali Kuchukua Hatua Kali Kwa Watoa Huduma Wasio Waaminifu Katika Sekta Nchini

 Serikari imesema haitamvumilia mfanyabiashara yeyote wa madini atakayefanya vitendo vya ubabaifu katika kazi kwa kusambaza bidhaa zisizo na ubora jambo ambalo hurudisha nyuma sekta ya madini na kupunguza uaminifu katika mzunguko wa biashara ya madini nchini. Kauli hiyo imetolewa mapema hii leo Mei 16 Mwaka 2025 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya I. Samamba akimwakilisha Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde Katika mkutano wa Jukwaa la watoa huduma na wadau wamiliki wa leseni nchini wenye lengo la uzinduzi wa Kamati ya Mawasiliano na Masoko kupitia chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA). Aidha, Katibu Mkuu huyo, amewataka wadau hao wa madini kuwa na ushirikiano kwani kufanya hivyo ni kutimiza maerekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha ufanisi katika maeneo ya kazi na kuboresha huduma wanazozitoa. Kwa Upande wake Kamishana wa Tume ya Madini, Bi. Theresia Numbi amesema kuwa jukwaa la mkutano wa wadau hao ni matunda ya kika...