Skip to main content

Posts

Showing posts from August 4, 2025

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Alex Msama Ampongeza Jerry Silaa Kushinda Kura za Maoni Ubunge Ukonga, Ushindani Sio Uadui

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Ndugu Alex Msama ambaye alitia nia Ubunge Kupitia CCM katika Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam amempongeza Ndugu Jerry Silaa kwa kuibuka mshidi wa kura za maoni katika jimbo hilo. Msama amesema Silaa ni rafiki yake, ndugu yake, mdogo wake na wamefahamiana kwa muda mrefu, hivyo kushindana kwao katika siasa sio uadui bali ndio ukomavu wa Demokrasia ndani ya Chama cha Mapinduzi na Taifa kwa ujumla na ameahidi kushiriki kumpigia Kampeni. Aidha, amewataka wote ambao majina yao yalikatwa na ambao hawajashinda kura za maoni, kusahau yaliyopita na kuwaunga mkono walioshinda na kuhakikisha CCM inashinda kwa Kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba.

Nsekela Aongoza Kura za Maoni Ubunge Jimbo la Kyerwa

 Na Angela Sebastian ;Kyerwa Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Khaldi Mussa Nsekela ameongoza kura za maoni katika jimbo la Kyerwa kwa kupata kura 5693 kati ya kura 8,134 zilizopigwa. Katibu wa CCM Wilaya hiyo Kisamba Kisando ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi akitangaza matokeo hayo amewataja wagombea wengine kuwa ni Innocent Bilakwate aliyekuwa mbunge kwa awamu iliyopita ambaye amepata kura 1567,Stephen Katemba kura 542 na Maxson Barthazary kura 152. Amewataja wengine kuwa ni Benedicto Mutungilehi kura 101 na Sperata Marco aliyepata kura 16 . Amesema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 8420 waliojitokeza kupiga kura ni 8134 zilizoharibika ni kura 63 na kura halali ni 8071 hivyo kumfanya Khald Nsekela kuongeza katika uchaguzi huo.

Bukombe Wamchagua Dkt. Doto Biteko Kwa 99.8%

Wajumbe wa Mkutano Mkuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe wamemchagua Dkt. Doto Mashaka Biteko kwa asilimia 99.8 baada ya kupata kura 7,441 kati ya kura 7,456 zilizopigwa ili apeperushe bendera ya Chama hicho. Akitangaza matokeo hayo August 04, 2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Jimbo la Bukombe linajumla ya wajumbe 7,835 na waliopiga kura ni 7,456 ambapo kura zilizoharibika ni 15, kura za hapana ni 0, kura halali zilizopigwa ni 7,441. Kwa matokeo hayo, Dkt. Doto Mashaka Biteko amepata kura 7,441 kati ya 7,456 sawa na wastani wa asilimia 99.8 uchaguzi uliofanyika katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

Rweikiza Aongoza Kura Za Maoni Bukoba Vijijini

 Na Angela Sebastian  ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Bakoba vijijini Mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dk Jason Rweikiza ameongoza kura za maoni kwa kupata kura 6,465 akifuatiwa na Faris Burham kura 4619. Akitangaza Matokeo hayo, Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba vijijini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jesca Ndyamukama amesema kuwa kura zilizopigwa ni 11,682 kura halali 11,582 na zilizoharibika ni kura 100 Katibu huyo amewatangaza Wagombea wengine ambao ni Fahami Mastawili kura 239,Asted Mpita kura 124,Edmund Rutaraka  kura 89 na  Philibart Bagenda kura 44.

Nishati Safi ya Rafiki Briquettes Yawa Mkombozi Kwa Wakulima na Wafanyakazi

●Inadumu zaidi ya masaa matatu ●Rafiki kwa mazingira ●Rafiki wa bei  *Dodoma* Katika mwendelezo wa kuwahimiza na kuhamasisha watanzania katika kutumia Nishati safi ya Rafiki Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imetumia maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma kutoa elimu ya  matumizi ya  nishati safi  ya Rafiki Briquettes. Akiongea  wakati wa kutoa elimu katika banda la STAMICO, Meneja Masoko na Uhusiano Bw. Deus Alex amezungumzia azma ya  kuhakikisha kuwa nishati hii inawafikia watu wengi ili kuweza kupunguza matumizi ya Kuni na Mkaa unaotokana na Miti.  Ameongeza pia, katika maonesho hayo STAMICO imeleta bidhaa za kokoto kwa ajili ya Watanzania wanaohitaji kwa ajili ya ujenzi mkubwa na mdogo. Uzalishaji huo wa Kokoto unapatikana eneo la Chigongwe barabara ya Singida. Akielezea kuhusu nishati hiyo, Deus amefafanua kuwa nishati hii utokana na mabaki ya makaa ya mawe yanayochimbwa katika mgodi wa Kabulo - Kiwira mkoani Songwe ambapo mabaki hayo...

Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi wa Sadc Waanza Madagascar Na Kikao cha Kujadili Mpango wa Maendeleo

Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umeanza Agosti 04, 2025 jijini Antananarivo, Madagascar na Kikao cha Wataalamu cha Maafisa Waandamizi cha kupitia Utekelezaji wa Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa Kikanda 2030 (Regional Indicative Strategic Development Plan 2030-RISDP). Tanzania inashiriki kikao hicho muhimu kwa maendeleo ya kikanda, huku ujumbe wake katika kikao hicho, ukiongozwa na Mkurugenzi wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri.  Akifungua kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Balozi Albert Chimbindi alisema lengo la kikao hicho ni kufanya tathimini ya utekelezaji wa mpango wa RISDP ili kujua hatua iliyofikiwa na kubaini vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wake na kuvitafutia ufumbuzi wa pamoja.  Alisema licha ya taarifa mbalimbali kuonesha kuwa mpango huo unapata mafanikio, lakini bado jitihada za pamoja ba...

Uongozi wa Shule za Kaizerege Wamshukuru Rais Samia

Na Angela Sebastian; Bukoba  UONGOZI wa shule za Kaizirege na Kemebos zilizopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamemshukuru Dk.Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya kugharamia masomo ya elimu ya juu ndani na nje ya nchi, wanafunzi wanne wa shule hiyo waliohitimu kidato cha sita mwaka huu kati ya 50 wa mchepue wa Sayansi nchi nzima. Wanafunzi hao waliopata matoke ya daraja la kwanza la alama tatu katika mchepuo wa Sayansi ni Anitha  Kulwa aliyekuwa akisoma PCM,Bright Yohana PCB pia Christopher Wambura na Cleophas Wambura ambao ni watoto mapacha waliosoma PCB. Wakato huohuo uongozi wa shule hiyo umetoa tuzo yenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa wanafunzi hao kama motisha na pongezi kwa matokeo hayo. Mkurugenzi wa shule za Kaizirege na Kemebos Eusto Ntagalinda akikabidhi tuzo hizo jana shuleni hapo Minispaa ya Bukoba ambapo alimshukuru Dk.Samia kwa kutoa ufadhili huo wa masomo kwa vijana hao wanne ambao walikuwa wakisoma mchepuo wa Sayansi hari itakayosababisha wengine kuiga m...

TARURA Yakamilisha Ujenzi wa Madaraja 439, ikiokoa Bilioni 75

‎WAKALA ya Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) umesema kuwa tangu kuanzishwa kwake, wamefanikiwa kujenga jumla ya madaraja 439 ya mawe yenye thamani ya bilioni 15, hatua ambayo imewezesha kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.  ‎Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Mhandisi Mshauri wa TARURA, Mhandisi Pharles Ngeleja, waziri mkuu wa habari katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani hapa. ‎Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mhandisi Ngeleja ameleza kuwa, ujenzi wa madaraja ya mawe unaotoa nafuu kubwa ya gharama, na unazingatia mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huathiri miti mingine. ‎"TARURA tumeona umuhimu wa kutumia teknolojia ya mawe, ambayo ni nafuu na inaendana na mazingira ya vijijini. Kwa madaraja haya 439, tumetumia bilioni 15. Ikiwa tungetumia njia ya ujenzi wa madaraja ya zege, tungeweza kutumia zaidi ya bilioni 90. Hivyo, ujenzi wa madaraja ya mawe umewezesha kutoa kiasi kikubwa cha fedha za serikali," amesema Mhandisi. ‎A Mhandisi Ngeleja amezungumzia umuhimu ...