Skip to main content

Posts

Showing posts from April 7, 2026

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt.Mwigulu Afanya Mazungumzo na Balozu wa Qutar Nchini

 Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 8, 2026 amefanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini, Fahad Rashid Al-Marekhi, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Kiongozi wa Mila na Desturi za Kizanaki alaani Mapinduzi dhidi yake

  MVUTANO mkubwa umeibuka katika jamii ya Wazanaki kufuatia kile kinachodaiwa kuwa ni kusimikwa kwa kiongozi wa kimila (Omwami) kinyume na mila na desturi za kabila hilo, hatua iliyozua hofu ya kuvunjika kwa mshikamano wa kijamii. Kiongozi wa mila na desturi za Wazanaki, Omwami Mazila Marwa, ameibuka hadharani na kulaani vikali tukio hilo, akisisitiza kuwa utaratibu wa kumpata Omwami ni wa kurithi kutoka kwa mtangulizi, si kwa maamuzi ya ghafla au njama za kifamilia. Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake, Omwami huyo amesema yeye alirithi nafasi hiyo kutoka kwa baba yake mzazi, marehemu Edward Marwa Ihunyo, aliyefariki mwaka 2014, na kwamba utaratibu huo ndio unaotambulika rasmi katika mila za Kizanaki. Kutokana na hali hiyo, ameiiomba Serikali iingilie kati haraka iwezekanavyo ili kudhibiti mgogoro huo na kuwachukulia hatua wote waliohusika na mchakato huo unaodaiwa kukiuka mila. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa Butiama wameonyesha wasiwasi wao juu...

CCM yamlipua Heche:'Uchumi sio maneno ya kisiasa, lete takwimu

  Na,Saleh Lujuo-Dodoma KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amemshukia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche, akimtaka kuacha kutoa kauli za uchumi zisizo na takwimu. Akizungumza na waandishi wa habari leo  April 7,2026 jijini Dodoma, Kihongosi amesema kuwa mjadala wa uchumi, hususani suala la mafuta, hauhitaji siasa za majukwaani bali unahitaji uhalisia unaoongozwa na Takwimu na uelewa wa kina. Kwa msisitizo, Kihongosi Amesema kuwa kauli zisizo na uthibitisho zinaweza kupotosha umma na kuongeza hofu kwa wananchi, hasa katika kipindi ambacho gharama za maisha na bei ya mafuta vinajadiliwa kwa uzito mkubwa nchini. “Uchumi haujadiliwi kwa hisia au siasa nyepesi. Ni eneo linalohitaji takwimu, uchambuzi na uelewa wa kina kabla ya kuzungumza,” amesisitiza. Kadhalika, Ameongeza kuwa ni vyema kwa viongozi kutumia muda kujifunza na kufahamu hali halisi ya mambo kabla ya kujitokeza hadharani kutoa matamko yanayoweza kupotosh...

Waziri Mkuu ahani msiba wa Mstahiki Meya Mstaafu wa Jiji la Zanzibar

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Aprili 7, 2026, amehani msiba wa  Mstahiki Meya Mstaafu wa Jiji la Zanzibar, Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa, nyumbani kwa marehemu  Zanzibar. Marehemu Mahmoud Muhammed Mussa alifariki Aprili 6, 2026. Wakati wa uhai wake, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali, ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi (BLW).