MFANYAKAZI WA PREMER CASKNO MWANZA AILILIA SERIKALI. Na Mwandishi Wetu, Mwanza MFANYAKAZI wa Premer Casino ya Mwanza katika Idara ya Ulinzi Bw Nassor Butondo amelalamikia kitendo cha kushambuliwa na wachina Agosti ak 30, mwaka huu, majira ya usiku wakati anatekeleza majukumu yake ya ulinzi, Jambo Digital imeelezwa. Aidha Butondo ameulalamikia uongozi wa Casino hiyo iliyoko katika Jengo la Rock City Mall Wilayani Ilemela kwa kushindwa kumhudumia kimatibabu mlinzi wao huku wakitumia fedha nyingi kuwatibisha wachina walioanzisha fujo ndani ya Casino. "Mwajili wangu anawathamini zaidi wachina kuliko mimi, ndio maana pengine ni kwasababu ndio wateja wa kamali, hivyo matusi yao ya nguoni inabidi wafanyakazi wayavumilie tu, wakati mwingine huwadhalilisha wafanyakazi wa kike kwa kuwaingizia vidole sehemu ambazo sio rasmi, Serikali itusaidie" alifafanua Butondo. Imedaiwa kuwa siku hiyo kulitokea kutoelewana kati ya mchina na mzungu baada ya mchina (jina tunalo) kuliwa kwenye ...
Marato tv - Sauti ya Jamii