Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Mlimba (CCM), Dk Kellen-Rose Rwakatare amewahimiza wazazi kushirikiana na walimu katika malezi ya watoto wao badala ya kuona jukumu hilo kama ni la walimu. Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa tamasha la kitaaluma na michezo kwa wanafunzi wa shule ya St Mary’s Tabata . Dk Rwakatare ambaye pia ni Mkurugenzi wa shule za St Mary’s alisema kama wazazi wanatona umuhimu wa kuzingatia malezi bora kwa watoto wao, basi kwa kushirikiana na walimu watapata taifa lenye nidhamu kubwa. “Tusione kuwa tunapolipa ada tunakuwa tumemaliza, mwalimu anasehemu yake ya malezi lakini mzazi anasehemu kubwa kwasababu muda mwingi anakuwa na mtoto nyumbani,” alisema Kwenye tamasha hilo, wanafunzi walionyesha umahiri wa vipaji mbalimbali kuanzia vipaji vya taaluma na vipaji vya michezo ya aina mbalimbali ambapo baadhi ya wanafunzi hao walimudu kuimba nyimbo mbalimbali kwa lugha ya kichina. Dk Rwakatare alisema kila mwaka wamekuwa wakiandaa matam...
Marato tv - Sauti ya Jamii