Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa (JKT)Dkt Rhimo Nyansaho ametoa Vizimba vitano vya ufugaji wa Samaki kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Mara ili kusaidia jumuiya kujiimarisha kiuchumi. Vizimba hivyo vitano ambavyo vitatumika kufugia samaki katika ziwa Victoria vina thamani ya shilingi Milioni 125. Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya uongozi ya UWT mkoa wa Mara mjini Musoma June 18 mwaka huu 2026 dkt Nyansaho amesema lazima jumuiya hiyo muhimu ya chama cha Mapinduzi iweze kuimarika kiuchumi. Waziri Nyansaho amesema kutokana na ukubwa wa Jumuiya hiyo inahitaji kuwa na mapato yake ili waweze kujitegemea katika uendeshaji wa shughuli zake na kujitegemea hasa nyakati za chaguzi. Amesema Jumuiya hiyo ni miongoni mwa Jumuia kubwa na muhimu ndani ya CCM hivyo wataendelea kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi ili kukuza uchumi wa Jumuia, familia na Taifa kwa ujumla. Sambamba na hilo Waziri huyo pia ameiahidi Jumuia hiyo kuwa ...
Marato tv - Sauti ya Jamii